Psalms 120 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Katika dhiki yangu namwita BWANA,naye hunijibu. 2 Ee BWANA, uniokoe kutoka midomo ya uongona ndimi za udanganyifu. 3 Atakufanyia nini,au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? 4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6 Nimeishi muda mrefu mnomiongoni mwa wale wanaochukia amani. 7 Mimi ni mtu wa amani;lakini ninaposema, wao wanataka vita.