Psalms 131 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee BWANA,macho yangu hayajivuni;sijishughulishi na mambo makuu kunizidiwala mambo ya ajabu mno kwangu. 2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,kama mtoto aliyeachishwa kunyonyandivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu. 3 Ee Israeli, mtumaini BWANAtangu sasa na hata milele.