Psalms 133 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendezawakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,yakitiririka kwenye ndevu,yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 3 Ni kama vile umande wa Hermoniunavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.Kwa maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka yake,naam, hata uzima milele.