Psalms 82 (BOKCV)
undefined Zaburi ya Asafu. 1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu,anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: 2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio hakina kuonyesha upendeleo kwa waovu? 3 Teteeni wanyonge na yatima,tunzeni haki za maskini na walioonewa. 4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. 5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote.Wanatembea gizani;misingi yote ya dunia imetikisika. 6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ 7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” 8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.