2 Chronicles 13 (BOKCV)

1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 2 naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti Urieli wa Gibea.Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 3 Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo. 4 Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Israeli yote, nisikilizeni mimi! 5 Hamfahamu kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa Agano la chumvi? 6 Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Solomoni mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake. 7 Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Solomoni alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao. 8 “Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa BWANA ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. 9 Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu. 10 “Lakini kwetu sisi, BWANA ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia BWANA ni wana wa Aroni, nao Walawi wakiwasaidia. 11 Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa BWANA. Wao huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za BWANA Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu. 12 Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya BWANA, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.” 13 Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili kwamba akiwa mbele ya Yuda, jeshi liwavizie kwa nyuma. 14 Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia BWANA. Makuhani wakapiga tarumbeta zao, 15 nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. 16 Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao. 17 Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. 18 Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao. 19 Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo. 20 Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye BWANA akampiga Yeroboamu akafa. 21 Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita. 22 Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

In Other Versions

2 Chronicles 13 in the ANGEFD

2 Chronicles 13 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 13 in the AS21

2 Chronicles 13 in the BAGH

2 Chronicles 13 in the BBPNG

2 Chronicles 13 in the BBT1E

2 Chronicles 13 in the BDS

2 Chronicles 13 in the BEV

2 Chronicles 13 in the BHAD

2 Chronicles 13 in the BIB

2 Chronicles 13 in the BLPT

2 Chronicles 13 in the BNT

2 Chronicles 13 in the BNTABOOT

2 Chronicles 13 in the BNTLV

2 Chronicles 13 in the BOATCB

2 Chronicles 13 in the BOATCB2

2 Chronicles 13 in the BOBCV

2 Chronicles 13 in the BOCNT

2 Chronicles 13 in the BOECS

2 Chronicles 13 in the BOGWICC

2 Chronicles 13 in the BOHCB

2 Chronicles 13 in the BOHCV

2 Chronicles 13 in the BOHLNT

2 Chronicles 13 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 13 in the BOICB

2 Chronicles 13 in the BOILNTAP

2 Chronicles 13 in the BOITCV

2 Chronicles 13 in the BOKCV2

2 Chronicles 13 in the BOKHWOG

2 Chronicles 13 in the BOKSSV

2 Chronicles 13 in the BOLCB

2 Chronicles 13 in the BOLCB2

2 Chronicles 13 in the BOMCV

2 Chronicles 13 in the BONAV

2 Chronicles 13 in the BONCB

2 Chronicles 13 in the BONLT

2 Chronicles 13 in the BONUT2

2 Chronicles 13 in the BOPLNT

2 Chronicles 13 in the BOSCB

2 Chronicles 13 in the BOSNC

2 Chronicles 13 in the BOTLNT

2 Chronicles 13 in the BOVCB

2 Chronicles 13 in the BOYCB

2 Chronicles 13 in the BPBB

2 Chronicles 13 in the BPH

2 Chronicles 13 in the BSB

2 Chronicles 13 in the CCB

2 Chronicles 13 in the CUV

2 Chronicles 13 in the CUVS

2 Chronicles 13 in the DBT

2 Chronicles 13 in the DGDNT

2 Chronicles 13 in the DHNT

2 Chronicles 13 in the DNT

2 Chronicles 13 in the ELBE

2 Chronicles 13 in the EMTV

2 Chronicles 13 in the ESV

2 Chronicles 13 in the FBV

2 Chronicles 13 in the FEB

2 Chronicles 13 in the GGMNT

2 Chronicles 13 in the GNT

2 Chronicles 13 in the HARY

2 Chronicles 13 in the HNT

2 Chronicles 13 in the IRVA

2 Chronicles 13 in the IRVB

2 Chronicles 13 in the IRVG

2 Chronicles 13 in the IRVH

2 Chronicles 13 in the IRVK

2 Chronicles 13 in the IRVM

2 Chronicles 13 in the IRVM2

2 Chronicles 13 in the IRVO

2 Chronicles 13 in the IRVP

2 Chronicles 13 in the IRVT

2 Chronicles 13 in the IRVT2

2 Chronicles 13 in the IRVU

2 Chronicles 13 in the ISVN

2 Chronicles 13 in the JSNT

2 Chronicles 13 in the KAPI

2 Chronicles 13 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 13 in the KBV

2 Chronicles 13 in the KJV

2 Chronicles 13 in the KNFD

2 Chronicles 13 in the LBA

2 Chronicles 13 in the LBLA

2 Chronicles 13 in the LNT

2 Chronicles 13 in the LSV

2 Chronicles 13 in the MAAL

2 Chronicles 13 in the MBV

2 Chronicles 13 in the MBV2

2 Chronicles 13 in the MHNT

2 Chronicles 13 in the MKNFD

2 Chronicles 13 in the MNG

2 Chronicles 13 in the MNT

2 Chronicles 13 in the MNT2

2 Chronicles 13 in the MRS1T

2 Chronicles 13 in the NAA

2 Chronicles 13 in the NASB

2 Chronicles 13 in the NBLA

2 Chronicles 13 in the NBS

2 Chronicles 13 in the NBVTP

2 Chronicles 13 in the NET2

2 Chronicles 13 in the NIV11

2 Chronicles 13 in the NNT

2 Chronicles 13 in the NNT2

2 Chronicles 13 in the NNT3

2 Chronicles 13 in the PDDPT

2 Chronicles 13 in the PFNT

2 Chronicles 13 in the RMNT

2 Chronicles 13 in the SBIAS

2 Chronicles 13 in the SBIBS

2 Chronicles 13 in the SBIBS2

2 Chronicles 13 in the SBICS

2 Chronicles 13 in the SBIDS

2 Chronicles 13 in the SBIGS

2 Chronicles 13 in the SBIHS

2 Chronicles 13 in the SBIIS

2 Chronicles 13 in the SBIIS2

2 Chronicles 13 in the SBIIS3

2 Chronicles 13 in the SBIKS

2 Chronicles 13 in the SBIKS2

2 Chronicles 13 in the SBIMS

2 Chronicles 13 in the SBIOS

2 Chronicles 13 in the SBIPS

2 Chronicles 13 in the SBISS

2 Chronicles 13 in the SBITS

2 Chronicles 13 in the SBITS2

2 Chronicles 13 in the SBITS3

2 Chronicles 13 in the SBITS4

2 Chronicles 13 in the SBIUS

2 Chronicles 13 in the SBIVS

2 Chronicles 13 in the SBT

2 Chronicles 13 in the SBT1E

2 Chronicles 13 in the SCHL

2 Chronicles 13 in the SNT

2 Chronicles 13 in the SUSU

2 Chronicles 13 in the SUSU2

2 Chronicles 13 in the SYNO

2 Chronicles 13 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 13 in the TBT1E

2 Chronicles 13 in the TBT1E2

2 Chronicles 13 in the TFTIP

2 Chronicles 13 in the TFTU

2 Chronicles 13 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 13 in the THAI

2 Chronicles 13 in the TNFD

2 Chronicles 13 in the TNT

2 Chronicles 13 in the TNTIK

2 Chronicles 13 in the TNTIL

2 Chronicles 13 in the TNTIN

2 Chronicles 13 in the TNTIP

2 Chronicles 13 in the TNTIZ

2 Chronicles 13 in the TOMA

2 Chronicles 13 in the TTENT

2 Chronicles 13 in the UBG

2 Chronicles 13 in the UGV

2 Chronicles 13 in the UGV2

2 Chronicles 13 in the UGV3

2 Chronicles 13 in the VBL

2 Chronicles 13 in the VDCC

2 Chronicles 13 in the YALU

2 Chronicles 13 in the YAPE

2 Chronicles 13 in the YBVTP

2 Chronicles 13 in the ZBP