2 Thessalonians 2 (BOKCV)
1 Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, 2 msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako. 3 Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. 4 Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu. 5 Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 6 Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. 9 Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo, 10 na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11 Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, 12 na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu. 13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho kwa kuiamini kweli. 14 Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15 Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua. 16 Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, 17 awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.
In Other Versions
2 Thessalonians 2 in the ANGEFD
2 Thessalonians 2 in the ANTPNG2D
2 Thessalonians 2 in the BBPNG
2 Thessalonians 2 in the BBT1E
2 Thessalonians 2 in the BNTABOOT
2 Thessalonians 2 in the BNTLV
2 Thessalonians 2 in the BOATCB
2 Thessalonians 2 in the BOATCB2
2 Thessalonians 2 in the BOBCV
2 Thessalonians 2 in the BOCNT
2 Thessalonians 2 in the BOECS
2 Thessalonians 2 in the BOGWICC
2 Thessalonians 2 in the BOHCB
2 Thessalonians 2 in the BOHCV
2 Thessalonians 2 in the BOHLNT
2 Thessalonians 2 in the BOHNTLTAL
2 Thessalonians 2 in the BOICB
2 Thessalonians 2 in the BOILNTAP
2 Thessalonians 2 in the BOITCV
2 Thessalonians 2 in the BOKCV2
2 Thessalonians 2 in the BOKHWOG
2 Thessalonians 2 in the BOKSSV
2 Thessalonians 2 in the BOLCB
2 Thessalonians 2 in the BOLCB2
2 Thessalonians 2 in the BOMCV
2 Thessalonians 2 in the BONAV
2 Thessalonians 2 in the BONCB
2 Thessalonians 2 in the BONLT
2 Thessalonians 2 in the BONUT2
2 Thessalonians 2 in the BOPLNT
2 Thessalonians 2 in the BOSCB
2 Thessalonians 2 in the BOSNC
2 Thessalonians 2 in the BOTLNT
2 Thessalonians 2 in the BOVCB
2 Thessalonians 2 in the BOYCB
2 Thessalonians 2 in the DGDNT
2 Thessalonians 2 in the GGMNT
2 Thessalonians 2 in the IRVM2
2 Thessalonians 2 in the IRVT2
2 Thessalonians 2 in the KBT1ETNIK
2 Thessalonians 2 in the MKNFD
2 Thessalonians 2 in the MRS1T
2 Thessalonians 2 in the NBVTP
2 Thessalonians 2 in the NIV11
2 Thessalonians 2 in the PDDPT
2 Thessalonians 2 in the SBIAS
2 Thessalonians 2 in the SBIBS
2 Thessalonians 2 in the SBIBS2
2 Thessalonians 2 in the SBICS
2 Thessalonians 2 in the SBIDS
2 Thessalonians 2 in the SBIGS
2 Thessalonians 2 in the SBIHS
2 Thessalonians 2 in the SBIIS
2 Thessalonians 2 in the SBIIS2
2 Thessalonians 2 in the SBIIS3
2 Thessalonians 2 in the SBIKS
2 Thessalonians 2 in the SBIKS2
2 Thessalonians 2 in the SBIMS
2 Thessalonians 2 in the SBIOS
2 Thessalonians 2 in the SBIPS
2 Thessalonians 2 in the SBISS
2 Thessalonians 2 in the SBITS
2 Thessalonians 2 in the SBITS2
2 Thessalonians 2 in the SBITS3
2 Thessalonians 2 in the SBITS4
2 Thessalonians 2 in the SBIUS
2 Thessalonians 2 in the SBIVS
2 Thessalonians 2 in the SBT1E
2 Thessalonians 2 in the SUSU2
2 Thessalonians 2 in the TBIAOTANT
2 Thessalonians 2 in the TBT1E
2 Thessalonians 2 in the TBT1E2
2 Thessalonians 2 in the TFTIP
2 Thessalonians 2 in the TGNTATF3T
2 Thessalonians 2 in the TNTIK
2 Thessalonians 2 in the TNTIL
2 Thessalonians 2 in the TNTIN
2 Thessalonians 2 in the TNTIP
2 Thessalonians 2 in the TNTIZ
2 Thessalonians 2 in the TTENT