Exodus 15 (BOKCV)
1 Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia BWANA wimbo huu:“Nitamwimbia BWANA,kwa kuwa ametukuzwa sana.Farasi na mpanda farasiamewatosa baharini. 2 BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu;amekuwa wokovu wangu.Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 BWANA ni shujaa wa vita; BWANA ndilo jina lake. 4 Magari ya vita ya Farao na jeshi lakeamewatosa baharini.Maafisa wa Farao walio bora sanawamezamishwa katika Bahari ya Shamu. 5 Maji yenye kina yamewafunika,wamezama mpaka vilindini kama jiwe. 6 “Mkono wako wa kuume, Ee BWANAulitukuka kwa uweza.Mkono wako wa kuume, Ee BWANA,ukamponda adui. 7 Katika ukuu wa utukufu wako,ukawaangusha chini wale waliokupinga.Uliachia hasira yako kali,ikawateketeza kama kapi. 8 Kwa pumzi ya pua zakomaji yalijilundika.Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta,vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9 “Adui alijivuna,‘Nitawafuatia, nitawapata.Nitagawanya nyara;nitajishibisha kwa wao.Nitafuta upanga wanguna mkono wangu utawaangamiza.’ 10 Lakini ulipuliza kwa pumzi yako,bahari ikawafunika.Wakazama kama risasikwenye maji makuu. 11 “Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee BWANA?Ni nani kama Wewe:uliyetukuka katika utakatifu,utishaye katika utukufu,ukitenda maajabu? 12 Uliunyoosha mkono wako wa kuumena nchi ikawameza. 13 “Katika upendo wako usiokoma utawaongozawatu uliowakomboa.Katika nguvu zako utawaongozampaka makao yako matakatifu. 14 Mataifa watasikia na kutetemeka,uchungu utawakamata watu wa Ufilisti. 15 Wakuu wa Edomu wataogopa,viongozi wa Moabu watatetemeka kwa hofu,watu wa Kanaani watayeyuka, 16 vitisho na hofu vitawaangukia.Kwa nguvu ya mkono wakowatatulia kama jiwe,mpaka watu wako waishe kupita, Ee BWANA,mpaka watu uliowanunua wapite. 17 Utawaingiza na kuwapandikizajuu ya mlima wa urithi wako:hapo mahali, Ee BWANA, ulipopafanya kuwa makao yako,mahali patakatifu, Ee BWANA, ulipopajenga kwa mikono yako. 18 BWANA atatawalamilele na milele.” 19 Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, BWANA aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu. 20 Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. 21 Miriamu akawaimbia:“Mwimbieni BWANA,kwa maana ametukuka sana.Farasi na mpanda farasiamewatosa baharini.” 22 Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. 23 Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara) 24 Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?” 25 Ndipo Mose akamlilia BWANA, naye BWANA akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.Huko BWANA akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. 26 Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.” 27 Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.
In Other Versions
Exodus 15 in the ANGEFD
Exodus 15 in the ANTPNG2D
Exodus 15 in the AS21
Exodus 15 in the BAGH
Exodus 15 in the BBPNG
Exodus 15 in the BBT1E
Exodus 15 in the BDS
Exodus 15 in the BEV
Exodus 15 in the BHAD
Exodus 15 in the BIB
Exodus 15 in the BLPT
Exodus 15 in the BNT
Exodus 15 in the BNTABOOT
Exodus 15 in the BNTLV
Exodus 15 in the BOATCB
Exodus 15 in the BOATCB2
Exodus 15 in the BOBCV
Exodus 15 in the BOCNT
Exodus 15 in the BOECS
Exodus 15 in the BOGWICC
Exodus 15 in the BOHCB
Exodus 15 in the BOHCV
Exodus 15 in the BOHLNT
Exodus 15 in the BOHNTLTAL
Exodus 15 in the BOICB
Exodus 15 in the BOILNTAP
Exodus 15 in the BOITCV
Exodus 15 in the BOKCV2
Exodus 15 in the BOKHWOG
Exodus 15 in the BOKSSV
Exodus 15 in the BOLCB
Exodus 15 in the BOLCB2
Exodus 15 in the BOMCV
Exodus 15 in the BONAV
Exodus 15 in the BONCB
Exodus 15 in the BONLT
Exodus 15 in the BONUT2
Exodus 15 in the BOPLNT
Exodus 15 in the BOSCB
Exodus 15 in the BOSNC
Exodus 15 in the BOTLNT
Exodus 15 in the BOVCB
Exodus 15 in the BOYCB
Exodus 15 in the BPBB
Exodus 15 in the BPH
Exodus 15 in the BSB
Exodus 15 in the CCB
Exodus 15 in the CUV
Exodus 15 in the CUVS
Exodus 15 in the DBT
Exodus 15 in the DGDNT
Exodus 15 in the DHNT
Exodus 15 in the DNT
Exodus 15 in the ELBE
Exodus 15 in the EMTV
Exodus 15 in the ESV
Exodus 15 in the FBV
Exodus 15 in the FEB
Exodus 15 in the GGMNT
Exodus 15 in the GNT
Exodus 15 in the HARY
Exodus 15 in the HNT
Exodus 15 in the IRVA
Exodus 15 in the IRVB
Exodus 15 in the IRVG
Exodus 15 in the IRVH
Exodus 15 in the IRVK
Exodus 15 in the IRVM
Exodus 15 in the IRVM2
Exodus 15 in the IRVO
Exodus 15 in the IRVP
Exodus 15 in the IRVT
Exodus 15 in the IRVT2
Exodus 15 in the IRVU
Exodus 15 in the ISVN
Exodus 15 in the JSNT
Exodus 15 in the KAPI
Exodus 15 in the KBT1ETNIK
Exodus 15 in the KBV
Exodus 15 in the KJV
Exodus 15 in the KNFD
Exodus 15 in the LBA
Exodus 15 in the LBLA
Exodus 15 in the LNT
Exodus 15 in the LSV
Exodus 15 in the MAAL
Exodus 15 in the MBV
Exodus 15 in the MBV2
Exodus 15 in the MHNT
Exodus 15 in the MKNFD
Exodus 15 in the MNG
Exodus 15 in the MNT
Exodus 15 in the MNT2
Exodus 15 in the MRS1T
Exodus 15 in the NAA
Exodus 15 in the NASB
Exodus 15 in the NBLA
Exodus 15 in the NBS
Exodus 15 in the NBVTP
Exodus 15 in the NET2
Exodus 15 in the NIV11
Exodus 15 in the NNT
Exodus 15 in the NNT2
Exodus 15 in the NNT3
Exodus 15 in the PDDPT
Exodus 15 in the PFNT
Exodus 15 in the RMNT
Exodus 15 in the SBIAS
Exodus 15 in the SBIBS
Exodus 15 in the SBIBS2
Exodus 15 in the SBICS
Exodus 15 in the SBIDS
Exodus 15 in the SBIGS
Exodus 15 in the SBIHS
Exodus 15 in the SBIIS
Exodus 15 in the SBIIS2
Exodus 15 in the SBIIS3
Exodus 15 in the SBIKS
Exodus 15 in the SBIKS2
Exodus 15 in the SBIMS
Exodus 15 in the SBIOS
Exodus 15 in the SBIPS
Exodus 15 in the SBISS
Exodus 15 in the SBITS
Exodus 15 in the SBITS2
Exodus 15 in the SBITS3
Exodus 15 in the SBITS4
Exodus 15 in the SBIUS
Exodus 15 in the SBIVS
Exodus 15 in the SBT
Exodus 15 in the SBT1E
Exodus 15 in the SCHL
Exodus 15 in the SNT
Exodus 15 in the SUSU
Exodus 15 in the SUSU2
Exodus 15 in the SYNO
Exodus 15 in the TBIAOTANT
Exodus 15 in the TBT1E
Exodus 15 in the TBT1E2
Exodus 15 in the TFTIP
Exodus 15 in the TFTU
Exodus 15 in the TGNTATF3T
Exodus 15 in the THAI
Exodus 15 in the TNFD
Exodus 15 in the TNT
Exodus 15 in the TNTIK
Exodus 15 in the TNTIL
Exodus 15 in the TNTIN
Exodus 15 in the TNTIP
Exodus 15 in the TNTIZ
Exodus 15 in the TOMA
Exodus 15 in the TTENT
Exodus 15 in the UBG
Exodus 15 in the UGV
Exodus 15 in the UGV2
Exodus 15 in the UGV3
Exodus 15 in the VBL
Exodus 15 in the VDCC
Exodus 15 in the YALU
Exodus 15 in the YAPE
Exodus 15 in the YBVTP
Exodus 15 in the ZBP