Hebrews 6 (BOKCV)
1 Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tukisonga mbele ili tufikie utimilifu, sio kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, 2 mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. 3 Mungu akitujalia tutafanya hivyo. 4 Kwa kuwa ni vigumu kwa wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu, 5 ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, 6 kisha wakianguka, kuwarejesha tena katika toba. Kwa kuwa wanamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili na kumdhalilisha hadharani, nayo ikawa hasara kwao. 7 Ardhi ile ipokeayo mvua inyeshayo juu yake mara kwa mara hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao kwa ajili yao yalimwa, nayo nchi hiyo hupokea baraka kutoka kwa Mungu. 8 Lakini ardhi ikizaa miiba na mibaruti, haina thamani na iko hatarini ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuchomwa moto. 9 Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu. 10 Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia. 11 Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 12 ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi. 13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 14 akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 15 Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa. 16 Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 17 Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti. 19 Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho iliyo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika sehemu takatifu iliyopo nyuma ya pazia, 20 mahali ambapo Yesu mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki.
In Other Versions
Hebrews 6 in the ANGEFD
Hebrews 6 in the ANTPNG2D
Hebrews 6 in the AS21
Hebrews 6 in the BAGH
Hebrews 6 in the BBPNG
Hebrews 6 in the BBT1E
Hebrews 6 in the BDS
Hebrews 6 in the BEV
Hebrews 6 in the BHAD
Hebrews 6 in the BIB
Hebrews 6 in the BLPT
Hebrews 6 in the BNT
Hebrews 6 in the BNTABOOT
Hebrews 6 in the BNTLV
Hebrews 6 in the BOATCB
Hebrews 6 in the BOATCB2
Hebrews 6 in the BOBCV
Hebrews 6 in the BOCNT
Hebrews 6 in the BOECS
Hebrews 6 in the BOGWICC
Hebrews 6 in the BOHCB
Hebrews 6 in the BOHCV
Hebrews 6 in the BOHLNT
Hebrews 6 in the BOHNTLTAL
Hebrews 6 in the BOICB
Hebrews 6 in the BOILNTAP
Hebrews 6 in the BOITCV
Hebrews 6 in the BOKCV2
Hebrews 6 in the BOKHWOG
Hebrews 6 in the BOKSSV
Hebrews 6 in the BOLCB
Hebrews 6 in the BOLCB2
Hebrews 6 in the BOMCV
Hebrews 6 in the BONAV
Hebrews 6 in the BONCB
Hebrews 6 in the BONLT
Hebrews 6 in the BONUT2
Hebrews 6 in the BOPLNT
Hebrews 6 in the BOSCB
Hebrews 6 in the BOSNC
Hebrews 6 in the BOTLNT
Hebrews 6 in the BOVCB
Hebrews 6 in the BOYCB
Hebrews 6 in the BPBB
Hebrews 6 in the BPH
Hebrews 6 in the BSB
Hebrews 6 in the CCB
Hebrews 6 in the CUV
Hebrews 6 in the CUVS
Hebrews 6 in the DBT
Hebrews 6 in the DGDNT
Hebrews 6 in the DHNT
Hebrews 6 in the DNT
Hebrews 6 in the ELBE
Hebrews 6 in the EMTV
Hebrews 6 in the ESV
Hebrews 6 in the FBV
Hebrews 6 in the FEB
Hebrews 6 in the GGMNT
Hebrews 6 in the GNT
Hebrews 6 in the HARY
Hebrews 6 in the HNT
Hebrews 6 in the IRVA
Hebrews 6 in the IRVB
Hebrews 6 in the IRVG
Hebrews 6 in the IRVH
Hebrews 6 in the IRVK
Hebrews 6 in the IRVM
Hebrews 6 in the IRVM2
Hebrews 6 in the IRVO
Hebrews 6 in the IRVP
Hebrews 6 in the IRVT
Hebrews 6 in the IRVT2
Hebrews 6 in the IRVU
Hebrews 6 in the ISVN
Hebrews 6 in the JSNT
Hebrews 6 in the KAPI
Hebrews 6 in the KBT1ETNIK
Hebrews 6 in the KBV
Hebrews 6 in the KJV
Hebrews 6 in the KNFD
Hebrews 6 in the LBA
Hebrews 6 in the LBLA
Hebrews 6 in the LNT
Hebrews 6 in the LSV
Hebrews 6 in the MAAL
Hebrews 6 in the MBV
Hebrews 6 in the MBV2
Hebrews 6 in the MHNT
Hebrews 6 in the MKNFD
Hebrews 6 in the MNG
Hebrews 6 in the MNT
Hebrews 6 in the MNT2
Hebrews 6 in the MRS1T
Hebrews 6 in the NAA
Hebrews 6 in the NASB
Hebrews 6 in the NBLA
Hebrews 6 in the NBS
Hebrews 6 in the NBVTP
Hebrews 6 in the NET2
Hebrews 6 in the NIV11
Hebrews 6 in the NNT
Hebrews 6 in the NNT2
Hebrews 6 in the NNT3
Hebrews 6 in the PDDPT
Hebrews 6 in the PFNT
Hebrews 6 in the RMNT
Hebrews 6 in the SBIAS
Hebrews 6 in the SBIBS
Hebrews 6 in the SBIBS2
Hebrews 6 in the SBICS
Hebrews 6 in the SBIDS
Hebrews 6 in the SBIGS
Hebrews 6 in the SBIHS
Hebrews 6 in the SBIIS
Hebrews 6 in the SBIIS2
Hebrews 6 in the SBIIS3
Hebrews 6 in the SBIKS
Hebrews 6 in the SBIKS2
Hebrews 6 in the SBIMS
Hebrews 6 in the SBIOS
Hebrews 6 in the SBIPS
Hebrews 6 in the SBISS
Hebrews 6 in the SBITS
Hebrews 6 in the SBITS2
Hebrews 6 in the SBITS3
Hebrews 6 in the SBITS4
Hebrews 6 in the SBIUS
Hebrews 6 in the SBIVS
Hebrews 6 in the SBT
Hebrews 6 in the SBT1E
Hebrews 6 in the SCHL
Hebrews 6 in the SNT
Hebrews 6 in the SUSU
Hebrews 6 in the SUSU2
Hebrews 6 in the SYNO
Hebrews 6 in the TBIAOTANT
Hebrews 6 in the TBT1E
Hebrews 6 in the TBT1E2
Hebrews 6 in the TFTIP
Hebrews 6 in the TFTU
Hebrews 6 in the TGNTATF3T
Hebrews 6 in the THAI
Hebrews 6 in the TNFD
Hebrews 6 in the TNT
Hebrews 6 in the TNTIK
Hebrews 6 in the TNTIL
Hebrews 6 in the TNTIN
Hebrews 6 in the TNTIP
Hebrews 6 in the TNTIZ
Hebrews 6 in the TOMA
Hebrews 6 in the TTENT
Hebrews 6 in the UBG
Hebrews 6 in the UGV
Hebrews 6 in the UGV2
Hebrews 6 in the UGV3
Hebrews 6 in the VBL
Hebrews 6 in the VDCC
Hebrews 6 in the YALU
Hebrews 6 in the YAPE
Hebrews 6 in the YBVTP
Hebrews 6 in the ZBP