Isaiah 28 (BOKCV)

1 Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo! 2 Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,atakiangusha chini kwa nguvu. 3 Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,kitakanyagwa chini ya nyayo. 4 Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:mara mtu aionapo, huichuma na kuila. 5 Katika siku ile, BWANA Mwenye Nguvu Zoteatakuwa taji la utukufu,taji zuri la mauakwa mabaki ya watu wake. 6 Atakuwa roho ya hakikwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,chanzo cha nguvukwa wale wazuiao vita langoni. 7 Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;wanapepesuka wanapoona maono,wanajikwaa wanapotoa maamuzi. 8 Meza zote zimejawa na matapishiwala hakuna sehemu hata ndogoisiyokuwa na uchafu. 9 “Yeye anajaribu kumfundisha nani?Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini? 10 Kwa maana ni:Amri juu ya amri, amri juu ya amri,kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;hapa kidogo, kule kidogo.” 11 Sawa kabisa, kwa midomo migenina kwa lugha ngeni,Mungu atasema na watu hawa, 12 wale ambao aliwaambia,“Hapa ni mahali pa kupumzika,waliochoka na wapumzike,”na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”lakini hawakutaka kusikiliza. 13 Hivyo basi, neno la BWANA kwao litakuwa:Amri juu ya amri, amri juu ya amri,kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,hapa kidogo, kule kidogo:ili waende na kuanguka chali,wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa. 14 Kwa hiyo sikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharaumnaotawala watu hawa wa Yerusalemu. 15 Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,tumefanya mapatano na kuzimu.Wakati pigo lifurikalo litakapopita,haliwezi kutugusa sisi,kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letuna miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.” 16 Kwa hiyo hivi ndivyo BWANA Mwenyezi asemavyo:“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,jiwe lililojaribiwa,jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu. 17 Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimiana uadilifu kuwa timazi;mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 18 Agano lenu na kifo litabatilishwa,patano lenu na kuzimu halitasimama.Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,litawaangusha chini. 19 Kila mara lijapo litawachukua,asubuhi baada ya asubuhi,wakati wa mchana na wakati wa usiku,litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.” Kuuelewa ujumbe huuutaleta hofu tupu. 20 Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,nguo ya kujifunikia ni nyembamba mnomtu hawezi kujifunikia. 21 BWANA atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni. 22 Sasa acheni dharau zenu,la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, ameniambiahabari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote. 23 Sikilizeni msikie sauti yangu,tegeni masikio na msikie niyasemayo. 24 Wakati mkulima alimapo ili apande,je, hulima siku zote?Je, huendelea kubomoa ardhina kusawazisha udongo? 25 Akiisha kusawazisha shamba,je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?Je, hapandi ngano katika sehemu yake,shayiri katika eneo lake,na nafaka nyingine katika shamba lake? 26 Mungu wake humwelekezana kumfundisha njia iliyo sahihi. 27 Iliki haipurwi kwa nyundo,wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;iliki hupurwa kwa fimbo,na jira kwa ufito. 28 Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,farasi wake hawasagi. 29 Haya yote pia hutoka kwa BWANA Mwenye Nguvu Zote,mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.

In Other Versions

Isaiah 28 in the ANGEFD

Isaiah 28 in the ANTPNG2D

Isaiah 28 in the AS21

Isaiah 28 in the BAGH

Isaiah 28 in the BBPNG

Isaiah 28 in the BBT1E

Isaiah 28 in the BDS

Isaiah 28 in the BEV

Isaiah 28 in the BHAD

Isaiah 28 in the BIB

Isaiah 28 in the BLPT

Isaiah 28 in the BNT

Isaiah 28 in the BNTABOOT

Isaiah 28 in the BNTLV

Isaiah 28 in the BOATCB

Isaiah 28 in the BOATCB2

Isaiah 28 in the BOBCV

Isaiah 28 in the BOCNT

Isaiah 28 in the BOECS

Isaiah 28 in the BOGWICC

Isaiah 28 in the BOHCB

Isaiah 28 in the BOHCV

Isaiah 28 in the BOHLNT

Isaiah 28 in the BOHNTLTAL

Isaiah 28 in the BOICB

Isaiah 28 in the BOILNTAP

Isaiah 28 in the BOITCV

Isaiah 28 in the BOKCV2

Isaiah 28 in the BOKHWOG

Isaiah 28 in the BOKSSV

Isaiah 28 in the BOLCB

Isaiah 28 in the BOLCB2

Isaiah 28 in the BOMCV

Isaiah 28 in the BONAV

Isaiah 28 in the BONCB

Isaiah 28 in the BONLT

Isaiah 28 in the BONUT2

Isaiah 28 in the BOPLNT

Isaiah 28 in the BOSCB

Isaiah 28 in the BOSNC

Isaiah 28 in the BOTLNT

Isaiah 28 in the BOVCB

Isaiah 28 in the BOYCB

Isaiah 28 in the BPBB

Isaiah 28 in the BPH

Isaiah 28 in the BSB

Isaiah 28 in the CCB

Isaiah 28 in the CUV

Isaiah 28 in the CUVS

Isaiah 28 in the DBT

Isaiah 28 in the DGDNT

Isaiah 28 in the DHNT

Isaiah 28 in the DNT

Isaiah 28 in the ELBE

Isaiah 28 in the EMTV

Isaiah 28 in the ESV

Isaiah 28 in the FBV

Isaiah 28 in the FEB

Isaiah 28 in the GGMNT

Isaiah 28 in the GNT

Isaiah 28 in the HARY

Isaiah 28 in the HNT

Isaiah 28 in the IRVA

Isaiah 28 in the IRVB

Isaiah 28 in the IRVG

Isaiah 28 in the IRVH

Isaiah 28 in the IRVK

Isaiah 28 in the IRVM

Isaiah 28 in the IRVM2

Isaiah 28 in the IRVO

Isaiah 28 in the IRVP

Isaiah 28 in the IRVT

Isaiah 28 in the IRVT2

Isaiah 28 in the IRVU

Isaiah 28 in the ISVN

Isaiah 28 in the JSNT

Isaiah 28 in the KAPI

Isaiah 28 in the KBT1ETNIK

Isaiah 28 in the KBV

Isaiah 28 in the KJV

Isaiah 28 in the KNFD

Isaiah 28 in the LBA

Isaiah 28 in the LBLA

Isaiah 28 in the LNT

Isaiah 28 in the LSV

Isaiah 28 in the MAAL

Isaiah 28 in the MBV

Isaiah 28 in the MBV2

Isaiah 28 in the MHNT

Isaiah 28 in the MKNFD

Isaiah 28 in the MNG

Isaiah 28 in the MNT

Isaiah 28 in the MNT2

Isaiah 28 in the MRS1T

Isaiah 28 in the NAA

Isaiah 28 in the NASB

Isaiah 28 in the NBLA

Isaiah 28 in the NBS

Isaiah 28 in the NBVTP

Isaiah 28 in the NET2

Isaiah 28 in the NIV11

Isaiah 28 in the NNT

Isaiah 28 in the NNT2

Isaiah 28 in the NNT3

Isaiah 28 in the PDDPT

Isaiah 28 in the PFNT

Isaiah 28 in the RMNT

Isaiah 28 in the SBIAS

Isaiah 28 in the SBIBS

Isaiah 28 in the SBIBS2

Isaiah 28 in the SBICS

Isaiah 28 in the SBIDS

Isaiah 28 in the SBIGS

Isaiah 28 in the SBIHS

Isaiah 28 in the SBIIS

Isaiah 28 in the SBIIS2

Isaiah 28 in the SBIIS3

Isaiah 28 in the SBIKS

Isaiah 28 in the SBIKS2

Isaiah 28 in the SBIMS

Isaiah 28 in the SBIOS

Isaiah 28 in the SBIPS

Isaiah 28 in the SBISS

Isaiah 28 in the SBITS

Isaiah 28 in the SBITS2

Isaiah 28 in the SBITS3

Isaiah 28 in the SBITS4

Isaiah 28 in the SBIUS

Isaiah 28 in the SBIVS

Isaiah 28 in the SBT

Isaiah 28 in the SBT1E

Isaiah 28 in the SCHL

Isaiah 28 in the SNT

Isaiah 28 in the SUSU

Isaiah 28 in the SUSU2

Isaiah 28 in the SYNO

Isaiah 28 in the TBIAOTANT

Isaiah 28 in the TBT1E

Isaiah 28 in the TBT1E2

Isaiah 28 in the TFTIP

Isaiah 28 in the TFTU

Isaiah 28 in the TGNTATF3T

Isaiah 28 in the THAI

Isaiah 28 in the TNFD

Isaiah 28 in the TNT

Isaiah 28 in the TNTIK

Isaiah 28 in the TNTIL

Isaiah 28 in the TNTIN

Isaiah 28 in the TNTIP

Isaiah 28 in the TNTIZ

Isaiah 28 in the TOMA

Isaiah 28 in the TTENT

Isaiah 28 in the UBG

Isaiah 28 in the UGV

Isaiah 28 in the UGV2

Isaiah 28 in the UGV3

Isaiah 28 in the VBL

Isaiah 28 in the VDCC

Isaiah 28 in the YALU

Isaiah 28 in the YAPE

Isaiah 28 in the YBVTP

Isaiah 28 in the ZBP