Isaiah 30 (BOKCV)

1 BWANA asema,“Ole kwa watoto wakaidi,kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,wakilundika dhambi juu ya dhambi, 2 wale washukao kwenda Misribila kutaka shauri langu,wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio. 3 Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,kivuli cha Misri kitawaletea fedheha. 4 Ingawa wana maafisa katika Soanina wajumbe wamewasili katika Hanesi, 5 kila mmoja ataaibishwakwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,ambalo haliwaletei msaada wala faida,bali aibu tu na fedheha.” 6 Neno kuhusu wanyama wa Negebu:Katika nchi ya taabu na shida,ya simba za dume na jike,ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,hazina zao juu ya nundu za ngamia,kwa lile taifa lisilokuwa na faida, 7 kuvipeleka Misri,ambaye msaada wake haufai kabisa.Kwa hiyo nimemwita “Rahabu Asiyefanya Chochote.” 8 Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,liandike kwenye kitabu,ili liweze kuwa shahidi milelekwa ajili ya siku zijazo. 9 Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya BWANA. 10 Wanawaambia waonaji,“Msione maono tena!”Nako kwa manabii wanasema,“Msiendelee kutupatia maonoambayo ni ya kweli!Tuambieni mambo ya kupendeza,tabirini mambo ya uongo. 11 Acheni njia hii,ondokeni katika mapito haya,nanyi acheni kutukabili pamojana yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!” 12 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu, 13 dhambi hii itakuwa kwenukama ukuta mrefu,wenye ufa na wenye kubetuka,ambao unaanguka ghafula,mara moja. 14 Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongoukipasuka pasipo hurumaambapo katika vipande vyakehakuna kipande kitakachopatikanakwa kuukulia makaa kutoka jikoniau kuchotea maji kisimani.” 15 Hili ndilo BWANA Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,lakini hamkutaka. 16 Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’Kwa hiyo mtakimbia!Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi! 17 Watu 1,000 watakimbiakwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,kwa vitishio vya watu watanowote mtakimbia,hadi mtakapoachwa kama mlingoti wa benderajuu ya kilele cha mlima,kama bendera juu ya kilima.” 18 Hata hivyo BWANA anatamani kutupatia neema,anainuka ili kuwaonyesha huruma.Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa haki.Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye! 19 Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu. 20 Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona. 21 Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.” 22 Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha, na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!” 23 Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ngʼombe wenu watalisha katika shamba pana la majani. 24 Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto. 25 Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila mlima mrefu na kila kilima kilichoinuka sana. 26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utangʼaa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati BWANA atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia. 27 Tazama, Jina la BWANA linakuja kutoka mbali,likiwa na hasira kali inayowakapamoja na wingu zito la moshi,midomo yake imejaa ghadhabuna ulimi wake ni moto ulao. 28 Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,yakipanda hadi shingoni.Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,huweka lijamu katika mataya ya mataifaambayo huwaongoza upotevuni. 29 Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimishasikukuu takatifu.Mioyo yenu itashangiliakama vile watu wanapokwea na filimbikwenye mlima wa BWANA,kwa Mwamba wa Israeli. 30 BWANA atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,naye atawafanya wauone mkono wake ukishukapamoja na hasira yake kali na moto ulao,kukiwa na tufani ya mvua,ngurumo za radi na mvua ya mawe. 31 Sauti ya BWANA itaivunjavunja Ashuru,kwa fimbo yake ya utawala atawapiga. 32 Kila pigo BWANA atakaloliweka juu yaokwa fimbo yake ya kuadhibu,litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,anapopigana nao katika vitakwa mapigo ya mkono wake. 33 Tofethi imeandaliwa toka zamani,imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefuna kwa upana mkubwa,likiwa na moto na kuni tele;pumzi ya BWANA,kama kijito cha kiberiti,huuwasha moto.

In Other Versions

Isaiah 30 in the ANGEFD

Isaiah 30 in the ANTPNG2D

Isaiah 30 in the AS21

Isaiah 30 in the BAGH

Isaiah 30 in the BBPNG

Isaiah 30 in the BBT1E

Isaiah 30 in the BDS

Isaiah 30 in the BEV

Isaiah 30 in the BHAD

Isaiah 30 in the BIB

Isaiah 30 in the BLPT

Isaiah 30 in the BNT

Isaiah 30 in the BNTABOOT

Isaiah 30 in the BNTLV

Isaiah 30 in the BOATCB

Isaiah 30 in the BOATCB2

Isaiah 30 in the BOBCV

Isaiah 30 in the BOCNT

Isaiah 30 in the BOECS

Isaiah 30 in the BOGWICC

Isaiah 30 in the BOHCB

Isaiah 30 in the BOHCV

Isaiah 30 in the BOHLNT

Isaiah 30 in the BOHNTLTAL

Isaiah 30 in the BOICB

Isaiah 30 in the BOILNTAP

Isaiah 30 in the BOITCV

Isaiah 30 in the BOKCV2

Isaiah 30 in the BOKHWOG

Isaiah 30 in the BOKSSV

Isaiah 30 in the BOLCB

Isaiah 30 in the BOLCB2

Isaiah 30 in the BOMCV

Isaiah 30 in the BONAV

Isaiah 30 in the BONCB

Isaiah 30 in the BONLT

Isaiah 30 in the BONUT2

Isaiah 30 in the BOPLNT

Isaiah 30 in the BOSCB

Isaiah 30 in the BOSNC

Isaiah 30 in the BOTLNT

Isaiah 30 in the BOVCB

Isaiah 30 in the BOYCB

Isaiah 30 in the BPBB

Isaiah 30 in the BPH

Isaiah 30 in the BSB

Isaiah 30 in the CCB

Isaiah 30 in the CUV

Isaiah 30 in the CUVS

Isaiah 30 in the DBT

Isaiah 30 in the DGDNT

Isaiah 30 in the DHNT

Isaiah 30 in the DNT

Isaiah 30 in the ELBE

Isaiah 30 in the EMTV

Isaiah 30 in the ESV

Isaiah 30 in the FBV

Isaiah 30 in the FEB

Isaiah 30 in the GGMNT

Isaiah 30 in the GNT

Isaiah 30 in the HARY

Isaiah 30 in the HNT

Isaiah 30 in the IRVA

Isaiah 30 in the IRVB

Isaiah 30 in the IRVG

Isaiah 30 in the IRVH

Isaiah 30 in the IRVK

Isaiah 30 in the IRVM

Isaiah 30 in the IRVM2

Isaiah 30 in the IRVO

Isaiah 30 in the IRVP

Isaiah 30 in the IRVT

Isaiah 30 in the IRVT2

Isaiah 30 in the IRVU

Isaiah 30 in the ISVN

Isaiah 30 in the JSNT

Isaiah 30 in the KAPI

Isaiah 30 in the KBT1ETNIK

Isaiah 30 in the KBV

Isaiah 30 in the KJV

Isaiah 30 in the KNFD

Isaiah 30 in the LBA

Isaiah 30 in the LBLA

Isaiah 30 in the LNT

Isaiah 30 in the LSV

Isaiah 30 in the MAAL

Isaiah 30 in the MBV

Isaiah 30 in the MBV2

Isaiah 30 in the MHNT

Isaiah 30 in the MKNFD

Isaiah 30 in the MNG

Isaiah 30 in the MNT

Isaiah 30 in the MNT2

Isaiah 30 in the MRS1T

Isaiah 30 in the NAA

Isaiah 30 in the NASB

Isaiah 30 in the NBLA

Isaiah 30 in the NBS

Isaiah 30 in the NBVTP

Isaiah 30 in the NET2

Isaiah 30 in the NIV11

Isaiah 30 in the NNT

Isaiah 30 in the NNT2

Isaiah 30 in the NNT3

Isaiah 30 in the PDDPT

Isaiah 30 in the PFNT

Isaiah 30 in the RMNT

Isaiah 30 in the SBIAS

Isaiah 30 in the SBIBS

Isaiah 30 in the SBIBS2

Isaiah 30 in the SBICS

Isaiah 30 in the SBIDS

Isaiah 30 in the SBIGS

Isaiah 30 in the SBIHS

Isaiah 30 in the SBIIS

Isaiah 30 in the SBIIS2

Isaiah 30 in the SBIIS3

Isaiah 30 in the SBIKS

Isaiah 30 in the SBIKS2

Isaiah 30 in the SBIMS

Isaiah 30 in the SBIOS

Isaiah 30 in the SBIPS

Isaiah 30 in the SBISS

Isaiah 30 in the SBITS

Isaiah 30 in the SBITS2

Isaiah 30 in the SBITS3

Isaiah 30 in the SBITS4

Isaiah 30 in the SBIUS

Isaiah 30 in the SBIVS

Isaiah 30 in the SBT

Isaiah 30 in the SBT1E

Isaiah 30 in the SCHL

Isaiah 30 in the SNT

Isaiah 30 in the SUSU

Isaiah 30 in the SUSU2

Isaiah 30 in the SYNO

Isaiah 30 in the TBIAOTANT

Isaiah 30 in the TBT1E

Isaiah 30 in the TBT1E2

Isaiah 30 in the TFTIP

Isaiah 30 in the TFTU

Isaiah 30 in the TGNTATF3T

Isaiah 30 in the THAI

Isaiah 30 in the TNFD

Isaiah 30 in the TNT

Isaiah 30 in the TNTIK

Isaiah 30 in the TNTIL

Isaiah 30 in the TNTIN

Isaiah 30 in the TNTIP

Isaiah 30 in the TNTIZ

Isaiah 30 in the TOMA

Isaiah 30 in the TTENT

Isaiah 30 in the UBG

Isaiah 30 in the UGV

Isaiah 30 in the UGV2

Isaiah 30 in the UGV3

Isaiah 30 in the VBL

Isaiah 30 in the VDCC

Isaiah 30 in the YALU

Isaiah 30 in the YAPE

Isaiah 30 in the YBVTP

Isaiah 30 in the ZBP