Isaiah 5 (BOKCV)

1 Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,kuhusu shamba lake la mizabibu:Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibukwenye kilima chenye rutuba. 2 Alililima na kuondoa mawena akaliotesha mizabibu bora sana.Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,lakini lilizaa matunda mabaya tu. 3 “Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu. 4 Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibukuliko yale niliyofanya?Nilipotazamia kupata zabibu nzuri,kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu? 5 Sasa nitawaambia lile nitakalolitendeashamba langu la mizabibu:Nitaondoa uzio wake,nalo litaharibiwa,nitabomoa ukuta wake,nalo litakanyagwa. 6 Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,halitakatiwa matawi wala kulimwa,nayo michongoma na miiba itamea huko,nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.” 7 Shamba la mzabibu la BWANA Mwenye Nguvu Zoteni nyumba ya Israeli,na watu wa Yudani bustani yake ya kumpendeza.Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu. 8 Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumbana kuunganisha mashamba baada ya mashambahadi hakuna nafasi iliyobaki,nanyi mnaishi peke yenu katika nchi. 9 BWANA Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia:“Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa,nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 10 Shamba la mizabibu la eka kumilitatoa bathi moja ya divai,na homeri ya mbegu zilizopandwaitatoa efa moja tu ya nafaka.” 11 Ole wao wale waamkao asubuhi na mapemawakikimbilia kunywa vileo,wale wakawiao sana mpaka usiku,mpaka wamewaka kwa mvinyo. 12 Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao,matari, filimbi na mvinyo,lakini hawayajali matendo ya BWANA,wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake. 13 Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishonikwa sababu ya kukosa ufahamu,watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaana watu wao wengi watakauka kwa kiu. 14 Kwa hiyo kaburi limeongeza hamu yakena kupanua mdomo wake bila kikomo,ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu,pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote. 15 Hivyo mwanadamu atashushwa,na binadamu kunyenyekezwa,macho ya wenye majivuno yatanyenyekezwa. 16 Lakini BWANA Mwenye Nguvu Zote atatukuzwakwa ajili ya haki yake,naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewekuwa mtakatifu kwa haki yake. 17 Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe,wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri. 18 Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifuna uovu kama kwa kamba za mkokoteni, 19 kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka,aharakishe kazi yake ili tupate kuiona.Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike,tena udhihirike ili tupate kuujua.” 20 Ole wao wanaoita ubaya ni wema,na wema ni ubaya,wawekao giza badala ya nuru,na nuru badala ya giza,wawekao uchungu badala ya utamu,na utamu badala ya uchungu. 21 Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. 22 Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo,nao walio hodari katika kuchanganya vileo, 23 wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo,lakini huwanyima haki wasio na hatia. 24 Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi,na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto,ndivyo mizizi yao itakavyoozana maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi;kwa kuwa wameikataa sheria ya BWANA Mwenye Nguvu Zotena kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. 25 Kwa hiyo hasira ya BWANA inawaka dhidi ya watu wake,mkono wake umeinuliwa na anawapiga.Milima inatetemeka,maiti ni kama takataka kwenye barabara. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,mkono wake bado umeinuliwa juu. 26 Yeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali,anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia.Tazama wamekuja,kwa kasi na kwa haraka! 27 Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa,hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala,hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni,hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika. 28 Mishale yao ni mikali,pinde zao zote zimevutwa,kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume,magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli. 29 Ngurumo yao ni kama ile ya simba,wananguruma kama wana simba,wanakoroma wanapokamata mawindo yao,na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa. 30 Katika siku ile watanguruma juu yakekama ngurumo za bahari.Kama mtu akiitazama nchi,ataona giza na dhiki;hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.

In Other Versions

Isaiah 5 in the ANGEFD

Isaiah 5 in the ANTPNG2D

Isaiah 5 in the AS21

Isaiah 5 in the BAGH

Isaiah 5 in the BBPNG

Isaiah 5 in the BBT1E

Isaiah 5 in the BDS

Isaiah 5 in the BEV

Isaiah 5 in the BHAD

Isaiah 5 in the BIB

Isaiah 5 in the BLPT

Isaiah 5 in the BNT

Isaiah 5 in the BNTABOOT

Isaiah 5 in the BNTLV

Isaiah 5 in the BOATCB

Isaiah 5 in the BOATCB2

Isaiah 5 in the BOBCV

Isaiah 5 in the BOCNT

Isaiah 5 in the BOECS

Isaiah 5 in the BOGWICC

Isaiah 5 in the BOHCB

Isaiah 5 in the BOHCV

Isaiah 5 in the BOHLNT

Isaiah 5 in the BOHNTLTAL

Isaiah 5 in the BOICB

Isaiah 5 in the BOILNTAP

Isaiah 5 in the BOITCV

Isaiah 5 in the BOKCV2

Isaiah 5 in the BOKHWOG

Isaiah 5 in the BOKSSV

Isaiah 5 in the BOLCB

Isaiah 5 in the BOLCB2

Isaiah 5 in the BOMCV

Isaiah 5 in the BONAV

Isaiah 5 in the BONCB

Isaiah 5 in the BONLT

Isaiah 5 in the BONUT2

Isaiah 5 in the BOPLNT

Isaiah 5 in the BOSCB

Isaiah 5 in the BOSNC

Isaiah 5 in the BOTLNT

Isaiah 5 in the BOVCB

Isaiah 5 in the BOYCB

Isaiah 5 in the BPBB

Isaiah 5 in the BPH

Isaiah 5 in the BSB

Isaiah 5 in the CCB

Isaiah 5 in the CUV

Isaiah 5 in the CUVS

Isaiah 5 in the DBT

Isaiah 5 in the DGDNT

Isaiah 5 in the DHNT

Isaiah 5 in the DNT

Isaiah 5 in the ELBE

Isaiah 5 in the EMTV

Isaiah 5 in the ESV

Isaiah 5 in the FBV

Isaiah 5 in the FEB

Isaiah 5 in the GGMNT

Isaiah 5 in the GNT

Isaiah 5 in the HARY

Isaiah 5 in the HNT

Isaiah 5 in the IRVA

Isaiah 5 in the IRVB

Isaiah 5 in the IRVG

Isaiah 5 in the IRVH

Isaiah 5 in the IRVK

Isaiah 5 in the IRVM

Isaiah 5 in the IRVM2

Isaiah 5 in the IRVO

Isaiah 5 in the IRVP

Isaiah 5 in the IRVT

Isaiah 5 in the IRVT2

Isaiah 5 in the IRVU

Isaiah 5 in the ISVN

Isaiah 5 in the JSNT

Isaiah 5 in the KAPI

Isaiah 5 in the KBT1ETNIK

Isaiah 5 in the KBV

Isaiah 5 in the KJV

Isaiah 5 in the KNFD

Isaiah 5 in the LBA

Isaiah 5 in the LBLA

Isaiah 5 in the LNT

Isaiah 5 in the LSV

Isaiah 5 in the MAAL

Isaiah 5 in the MBV

Isaiah 5 in the MBV2

Isaiah 5 in the MHNT

Isaiah 5 in the MKNFD

Isaiah 5 in the MNG

Isaiah 5 in the MNT

Isaiah 5 in the MNT2

Isaiah 5 in the MRS1T

Isaiah 5 in the NAA

Isaiah 5 in the NASB

Isaiah 5 in the NBLA

Isaiah 5 in the NBS

Isaiah 5 in the NBVTP

Isaiah 5 in the NET2

Isaiah 5 in the NIV11

Isaiah 5 in the NNT

Isaiah 5 in the NNT2

Isaiah 5 in the NNT3

Isaiah 5 in the PDDPT

Isaiah 5 in the PFNT

Isaiah 5 in the RMNT

Isaiah 5 in the SBIAS

Isaiah 5 in the SBIBS

Isaiah 5 in the SBIBS2

Isaiah 5 in the SBICS

Isaiah 5 in the SBIDS

Isaiah 5 in the SBIGS

Isaiah 5 in the SBIHS

Isaiah 5 in the SBIIS

Isaiah 5 in the SBIIS2

Isaiah 5 in the SBIIS3

Isaiah 5 in the SBIKS

Isaiah 5 in the SBIKS2

Isaiah 5 in the SBIMS

Isaiah 5 in the SBIOS

Isaiah 5 in the SBIPS

Isaiah 5 in the SBISS

Isaiah 5 in the SBITS

Isaiah 5 in the SBITS2

Isaiah 5 in the SBITS3

Isaiah 5 in the SBITS4

Isaiah 5 in the SBIUS

Isaiah 5 in the SBIVS

Isaiah 5 in the SBT

Isaiah 5 in the SBT1E

Isaiah 5 in the SCHL

Isaiah 5 in the SNT

Isaiah 5 in the SUSU

Isaiah 5 in the SUSU2

Isaiah 5 in the SYNO

Isaiah 5 in the TBIAOTANT

Isaiah 5 in the TBT1E

Isaiah 5 in the TBT1E2

Isaiah 5 in the TFTIP

Isaiah 5 in the TFTU

Isaiah 5 in the TGNTATF3T

Isaiah 5 in the THAI

Isaiah 5 in the TNFD

Isaiah 5 in the TNT

Isaiah 5 in the TNTIK

Isaiah 5 in the TNTIL

Isaiah 5 in the TNTIN

Isaiah 5 in the TNTIP

Isaiah 5 in the TNTIZ

Isaiah 5 in the TOMA

Isaiah 5 in the TTENT

Isaiah 5 in the UBG

Isaiah 5 in the UGV

Isaiah 5 in the UGV2

Isaiah 5 in the UGV3

Isaiah 5 in the VBL

Isaiah 5 in the VDCC

Isaiah 5 in the YALU

Isaiah 5 in the YAPE

Isaiah 5 in the YBVTP

Isaiah 5 in the ZBP