James 2 (BOKCV)

1 Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu. 2 Kwa maana kama akija mtu katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia mtu maskini mwenye mavazi yaliyochakaa, 3 nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,” 4 je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu? 5 Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao? 6 Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani? 7 Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa? 8 Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. 9 Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10 Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria. 12 Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. 13 Kwa kuwa hukumu bila huruma itatolewa kwa mtu yeyote asiyekuwa na huruma. Huruma huishinda hukumu. 14 Ndugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa? 15 Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, 16 mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? 17 Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa. 18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.”Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo. 19 Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka. 20 Ewe mpumbavu! Je, wataka kujua kwamba imani bila matendo haifai kitu? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesabiwa haki kwa kile alichotenda, alipomtoa mwanawe Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani yake na matendo yake vilikuwa vinatenda kazi pamoja, nayo imani yake ikakamilishwa na kile alichotenda. 23 Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu. 24 Mnaona ya kwamba mtu huhesabiwa haki kwa yale anayotenda wala si kwa imani peke yake. 25 Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.

In Other Versions

James 2 in the ANGEFD

James 2 in the ANTPNG2D

James 2 in the AS21

James 2 in the BAGH

James 2 in the BBPNG

James 2 in the BBT1E

James 2 in the BDS

James 2 in the BEV

James 2 in the BHAD

James 2 in the BIB

James 2 in the BLPT

James 2 in the BNT

James 2 in the BNTABOOT

James 2 in the BNTLV

James 2 in the BOATCB

James 2 in the BOATCB2

James 2 in the BOBCV

James 2 in the BOCNT

James 2 in the BOECS

James 2 in the BOGWICC

James 2 in the BOHCB

James 2 in the BOHCV

James 2 in the BOHLNT

James 2 in the BOHNTLTAL

James 2 in the BOICB

James 2 in the BOILNTAP

James 2 in the BOITCV

James 2 in the BOKCV2

James 2 in the BOKHWOG

James 2 in the BOKSSV

James 2 in the BOLCB

James 2 in the BOLCB2

James 2 in the BOMCV

James 2 in the BONAV

James 2 in the BONCB

James 2 in the BONLT

James 2 in the BONUT2

James 2 in the BOPLNT

James 2 in the BOSCB

James 2 in the BOSNC

James 2 in the BOTLNT

James 2 in the BOVCB

James 2 in the BOYCB

James 2 in the BPBB

James 2 in the BPH

James 2 in the BSB

James 2 in the CCB

James 2 in the CUV

James 2 in the CUVS

James 2 in the DBT

James 2 in the DGDNT

James 2 in the DHNT

James 2 in the DNT

James 2 in the ELBE

James 2 in the EMTV

James 2 in the ESV

James 2 in the FBV

James 2 in the FEB

James 2 in the GGMNT

James 2 in the GNT

James 2 in the HARY

James 2 in the HNT

James 2 in the IRVA

James 2 in the IRVB

James 2 in the IRVG

James 2 in the IRVH

James 2 in the IRVK

James 2 in the IRVM

James 2 in the IRVM2

James 2 in the IRVO

James 2 in the IRVP

James 2 in the IRVT

James 2 in the IRVT2

James 2 in the IRVU

James 2 in the ISVN

James 2 in the JSNT

James 2 in the KAPI

James 2 in the KBT1ETNIK

James 2 in the KBV

James 2 in the KJV

James 2 in the KNFD

James 2 in the LBA

James 2 in the LBLA

James 2 in the LNT

James 2 in the LSV

James 2 in the MAAL

James 2 in the MBV

James 2 in the MBV2

James 2 in the MHNT

James 2 in the MKNFD

James 2 in the MNG

James 2 in the MNT

James 2 in the MNT2

James 2 in the MRS1T

James 2 in the NAA

James 2 in the NASB

James 2 in the NBLA

James 2 in the NBS

James 2 in the NBVTP

James 2 in the NET2

James 2 in the NIV11

James 2 in the NNT

James 2 in the NNT2

James 2 in the NNT3

James 2 in the PDDPT

James 2 in the PFNT

James 2 in the RMNT

James 2 in the SBIAS

James 2 in the SBIBS

James 2 in the SBIBS2

James 2 in the SBICS

James 2 in the SBIDS

James 2 in the SBIGS

James 2 in the SBIHS

James 2 in the SBIIS

James 2 in the SBIIS2

James 2 in the SBIIS3

James 2 in the SBIKS

James 2 in the SBIKS2

James 2 in the SBIMS

James 2 in the SBIOS

James 2 in the SBIPS

James 2 in the SBISS

James 2 in the SBITS

James 2 in the SBITS2

James 2 in the SBITS3

James 2 in the SBITS4

James 2 in the SBIUS

James 2 in the SBIVS

James 2 in the SBT

James 2 in the SBT1E

James 2 in the SCHL

James 2 in the SNT

James 2 in the SUSU

James 2 in the SUSU2

James 2 in the SYNO

James 2 in the TBIAOTANT

James 2 in the TBT1E

James 2 in the TBT1E2

James 2 in the TFTIP

James 2 in the TFTU

James 2 in the TGNTATF3T

James 2 in the THAI

James 2 in the TNFD

James 2 in the TNT

James 2 in the TNTIK

James 2 in the TNTIL

James 2 in the TNTIN

James 2 in the TNTIP

James 2 in the TNTIZ

James 2 in the TOMA

James 2 in the TTENT

James 2 in the UBG

James 2 in the UGV

James 2 in the UGV2

James 2 in the UGV3

James 2 in the VBL

James 2 in the VDCC

James 2 in the YALU

James 2 in the YAPE

James 2 in the YBVTP

James 2 in the ZBP