Jeremiah 13 (BOKCV)
1 Hili ndilo BWANA aliloniambia: “Nenda ununue mkanda wa kitani, ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.” 2 Kwa hiyo nikanunua mkanda, kama BWANA alivyoniagiza, nikajivika kiunoni. 3 Ndipo neno la BWANA likanijia kwa mara ya pili: 4 “Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Frati uufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.” 5 Ndipo nikaenda na kuuficha ule mkanda huko Frati, kama BWANA alivyoniamuru. 6 Baada ya siku nyingi BWANA akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.” 7 Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa. 8 Ndipo neno la BWANA likanijia: 9 “Hili ndilo BWANA asemalo: ‘Vivyo hivyo ndivyo nitakavyokiharibu kiburi cha Yuda na kiburi kikuu cha Yerusalemu. 10 Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mkanda huu ambao haufai kabisa! 11 Kwa maana kama vile mkanda ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyojifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda,’ asema BWANA, ‘ili wawe watu wangu kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu. Lakini hawajasikiliza.’ 12 “Waambie: ‘Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, asemalo: kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo.’ Kama wao wakikuambia, ‘Kwani hatujui kwamba kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo?’ 13 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: nitawajaza ulevi wote waishio katika nchi hii, pamoja na wafalme waketio juu ya kiti cha enzi cha Daudi, makuhani, manabii na wale wote waishio Yerusalemu. 14 Nitawagonganisha kila mmoja na mwenzake, baba na wana wao, asema BWANA. Sitawarehemu wala kuwahurumia ili niache kuwaangamiza.’ ” 15 Sikieni na mzingatie,msiwe na kiburi,kwa kuwa BWANA amenena. 16 Mpeni utukufu BWANA Mungu wenu,kabla hajaleta giza,kabla miguu yenu haijajikwaajuu ya vilima vitakavyotiwa giza.Mlitarajia nuru,lakini ataifanya kuwa giza nenena kuibadili kuwa huzuni kubwa. 17 Lakini kama hamtasikiliza,nitalia sirinikwa ajili ya kiburi chenu;macho yangu yatalia kwa uchungu,yakitiririka machozi,kwa sababu kundi la kondoo la BWANAlitachukuliwa mateka. 18 Mwambie mfalme na mamaye,“Shukeni kutoka kwenye viti vyenu vya enzi,kwa kuwa taji zenu za utukufuzitaanguka kutoka vichwani mwenu.” 19 Miji iliyoko Negebu itafungwa,wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua.Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni,wakichukuliwa kabisa waende mbali. 20 Inua macho yako uonewale wanaokuja kutoka kaskazini.Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa,kondoo wale uliojivunia? 21 Utasema nini BWANA atakapowaweka juu yakowale ulioungana nao kama marafiki wako maalum?Je, hutapatwa na utungu kama mwanamkealiye katika utungu wa kuzaa? 22 Nawe kama ukijiuliza,“Kwa nini haya yamenitokea?”Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingindipo marinda yako yameraruliwana mwili wako umetendewa vibaya. 23 Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yakeau chui kubadili madoadoa yake?Vivyo hivyo nawe huwezi kufanya memawewe uliyezoea kutenda mabaya. 24 “Nitawatawanya kama makapiyapeperushwayo na upepo wa jangwani. 25 Hii ndiyo kura yako,fungu nililokuamuria,”asema BWANA,“kwa sababu umenisahau mimina kuamini miungu ya uongo. 26 Nitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wakoili aibu yako ionekane: 27 uzinzi wako na kulia kwako kama farasi kulikojaa tamaa,ukahaba wako usio na aibu!Nimeyaona matendo yako ya machukizojuu ya vilima na mashambani.Ole wako, ee Yerusalemu!Utaendelea kuwa najisi mpaka lini?”
In Other Versions
Jeremiah 13 in the ANGEFD
Jeremiah 13 in the ANTPNG2D
Jeremiah 13 in the AS21
Jeremiah 13 in the BAGH
Jeremiah 13 in the BBPNG
Jeremiah 13 in the BBT1E
Jeremiah 13 in the BDS
Jeremiah 13 in the BEV
Jeremiah 13 in the BHAD
Jeremiah 13 in the BIB
Jeremiah 13 in the BLPT
Jeremiah 13 in the BNT
Jeremiah 13 in the BNTABOOT
Jeremiah 13 in the BNTLV
Jeremiah 13 in the BOATCB
Jeremiah 13 in the BOATCB2
Jeremiah 13 in the BOBCV
Jeremiah 13 in the BOCNT
Jeremiah 13 in the BOECS
Jeremiah 13 in the BOGWICC
Jeremiah 13 in the BOHCB
Jeremiah 13 in the BOHCV
Jeremiah 13 in the BOHLNT
Jeremiah 13 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 13 in the BOICB
Jeremiah 13 in the BOILNTAP
Jeremiah 13 in the BOITCV
Jeremiah 13 in the BOKCV2
Jeremiah 13 in the BOKHWOG
Jeremiah 13 in the BOKSSV
Jeremiah 13 in the BOLCB
Jeremiah 13 in the BOLCB2
Jeremiah 13 in the BOMCV
Jeremiah 13 in the BONAV
Jeremiah 13 in the BONCB
Jeremiah 13 in the BONLT
Jeremiah 13 in the BONUT2
Jeremiah 13 in the BOPLNT
Jeremiah 13 in the BOSCB
Jeremiah 13 in the BOSNC
Jeremiah 13 in the BOTLNT
Jeremiah 13 in the BOVCB
Jeremiah 13 in the BOYCB
Jeremiah 13 in the BPBB
Jeremiah 13 in the BPH
Jeremiah 13 in the BSB
Jeremiah 13 in the CCB
Jeremiah 13 in the CUV
Jeremiah 13 in the CUVS
Jeremiah 13 in the DBT
Jeremiah 13 in the DGDNT
Jeremiah 13 in the DHNT
Jeremiah 13 in the DNT
Jeremiah 13 in the ELBE
Jeremiah 13 in the EMTV
Jeremiah 13 in the ESV
Jeremiah 13 in the FBV
Jeremiah 13 in the FEB
Jeremiah 13 in the GGMNT
Jeremiah 13 in the GNT
Jeremiah 13 in the HARY
Jeremiah 13 in the HNT
Jeremiah 13 in the IRVA
Jeremiah 13 in the IRVB
Jeremiah 13 in the IRVG
Jeremiah 13 in the IRVH
Jeremiah 13 in the IRVK
Jeremiah 13 in the IRVM
Jeremiah 13 in the IRVM2
Jeremiah 13 in the IRVO
Jeremiah 13 in the IRVP
Jeremiah 13 in the IRVT
Jeremiah 13 in the IRVT2
Jeremiah 13 in the IRVU
Jeremiah 13 in the ISVN
Jeremiah 13 in the JSNT
Jeremiah 13 in the KAPI
Jeremiah 13 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 13 in the KBV
Jeremiah 13 in the KJV
Jeremiah 13 in the KNFD
Jeremiah 13 in the LBA
Jeremiah 13 in the LBLA
Jeremiah 13 in the LNT
Jeremiah 13 in the LSV
Jeremiah 13 in the MAAL
Jeremiah 13 in the MBV
Jeremiah 13 in the MBV2
Jeremiah 13 in the MHNT
Jeremiah 13 in the MKNFD
Jeremiah 13 in the MNG
Jeremiah 13 in the MNT
Jeremiah 13 in the MNT2
Jeremiah 13 in the MRS1T
Jeremiah 13 in the NAA
Jeremiah 13 in the NASB
Jeremiah 13 in the NBLA
Jeremiah 13 in the NBS
Jeremiah 13 in the NBVTP
Jeremiah 13 in the NET2
Jeremiah 13 in the NIV11
Jeremiah 13 in the NNT
Jeremiah 13 in the NNT2
Jeremiah 13 in the NNT3
Jeremiah 13 in the PDDPT
Jeremiah 13 in the PFNT
Jeremiah 13 in the RMNT
Jeremiah 13 in the SBIAS
Jeremiah 13 in the SBIBS
Jeremiah 13 in the SBIBS2
Jeremiah 13 in the SBICS
Jeremiah 13 in the SBIDS
Jeremiah 13 in the SBIGS
Jeremiah 13 in the SBIHS
Jeremiah 13 in the SBIIS
Jeremiah 13 in the SBIIS2
Jeremiah 13 in the SBIIS3
Jeremiah 13 in the SBIKS
Jeremiah 13 in the SBIKS2
Jeremiah 13 in the SBIMS
Jeremiah 13 in the SBIOS
Jeremiah 13 in the SBIPS
Jeremiah 13 in the SBISS
Jeremiah 13 in the SBITS
Jeremiah 13 in the SBITS2
Jeremiah 13 in the SBITS3
Jeremiah 13 in the SBITS4
Jeremiah 13 in the SBIUS
Jeremiah 13 in the SBIVS
Jeremiah 13 in the SBT
Jeremiah 13 in the SBT1E
Jeremiah 13 in the SCHL
Jeremiah 13 in the SNT
Jeremiah 13 in the SUSU
Jeremiah 13 in the SUSU2
Jeremiah 13 in the SYNO
Jeremiah 13 in the TBIAOTANT
Jeremiah 13 in the TBT1E
Jeremiah 13 in the TBT1E2
Jeremiah 13 in the TFTIP
Jeremiah 13 in the TFTU
Jeremiah 13 in the TGNTATF3T
Jeremiah 13 in the THAI
Jeremiah 13 in the TNFD
Jeremiah 13 in the TNT
Jeremiah 13 in the TNTIK
Jeremiah 13 in the TNTIL
Jeremiah 13 in the TNTIN
Jeremiah 13 in the TNTIP
Jeremiah 13 in the TNTIZ
Jeremiah 13 in the TOMA
Jeremiah 13 in the TTENT
Jeremiah 13 in the UBG
Jeremiah 13 in the UGV
Jeremiah 13 in the UGV2
Jeremiah 13 in the UGV3
Jeremiah 13 in the VBL
Jeremiah 13 in the VDCC
Jeremiah 13 in the YALU
Jeremiah 13 in the YAPE
Jeremiah 13 in the YBVTP
Jeremiah 13 in the ZBP