Jeremiah 23 (BOKCV)

1 “Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asema BWANA. 2 Kwa hiyo hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema BWANA. 3 “Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao. 4 Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema BWANA. 5 BWANA asema, “Siku zinakuja,nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,Mfalme atakayetawala kwa hekima,na kutenda lililo haki na sawa katika nchi. 6 Katika siku zake, Yuda ataokolewana Israeli ataishi salama.Hili ndilo jina atakaloitwa: BWANA Haki Yetu. 7 “Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama BWANA aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ 8 bali watasema, ‘Hakika kama BWANA aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema BWANA. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.” 9 Kuhusu manabii:Moyo wangu umevunjika ndani yangu;mifupa yangu yote inatetemeka.Nimekuwa kama mtu aliyelewa,kama mtu aliyelemewa na divai,kwa sababu ya BWANAna maneno yake matakatifu. 10 Nchi imejaa wazinzi;kwa sababu ya laana, nchi imekaukana malisho yaliyoko nyikani yamekauka.Mwenendo wa manabii ni mbayana mamlaka yao si ya haki. 11 “Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”asema BWANA. 12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,watafukuziwa mbali gizanina huko wataanguka.Nitaleta maafa juu yaokatika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”asema BWANA. 13 “Miongoni mwa manabii wa Samarianililiona jambo la kuchukiza:Walitabiri kwa Baalina kuwapotosha Israeli watu wangu. 14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemunimeona jambo baya sana:Wanafanya uzinzina kuenenda katika uongo.Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,kwa ajili hiyo hakuna yeyoteanayeachana na uovu wake.Wote wako kama Sodoma kwangu;watu na Yerusalemu wako kama Gomora.” 15 Kwa hiyo, hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:“Nitawafanya wale chakula kichunguna kunywa maji yaliyotiwa sumu,kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemukutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.” 16 Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo:“Msisikilize wanachowatabiria manabii,wanawajaza matumaini ya uongo.Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,hayatoki katika kinywa cha BWANA. 17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,‘BWANA asema: Mtakuwa na amani.’Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’ 18 Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la BWANAili kuona au kusikia neno lake?Ni nani aliyesikilizana kusikia neno lake? 19 Tazama, dhoruba ya BWANAitapasuka kwa ghadhabu,kisulisuli kitazunguka na kuangukavichwani vya waovu. 20 Hasira ya BWANA haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi. 21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.Mimi sikusema nao,lakini wametabiri. 22 Lakini kama wangesimama barazani mwangu,wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,nao wangewageuza kutoka njia zao mbayana kutoka matendo yao maovu.” 23 “Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,” BWANA asema,“wala si Mungu aliyeko pia mbali? 24 Je, mtu yeyote aweza kujifichamahali pa siri ili nisiweze kumwona?” BWANA asema.“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?” BWANA asema. 25 “Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ 26 Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? 27 Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali. 28 Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema BWANA. 29 “Je, neno langu si kama moto,” asema BWANA, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande? 30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema BWANA. 31 “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘BWANA asema.’ 32 Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asema BWANA. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asema BWANA. 33 “Wakati watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo wa BWANA ni nini?’ wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asema BWANA.’ 34 Nabii, kuhani, au mtu yeyote akisema, ‘Huu ndio mzigo wa BWANA,’ nitamwadhibu huyo na nyumba yake. 35 Hivyo mnaambiana kila mmoja na mwenzake, au kwa mtu wa nyumba yao: ‘BWANA amejibu nini?’ au ‘BWANA amesema nini?’ 36 Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa BWANA,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu. 37 Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘BWANA amekujibu nini?’ au ‘Je, BWANA amesema nini?’ 38 Ingawa unadai, ‘Huu ndio mzigo wa BWANA,’ hili ndilo BWANA asemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo wa BWANA,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo wa BWANA.’ 39 Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu. 40 Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”

In Other Versions

Jeremiah 23 in the ANGEFD

Jeremiah 23 in the ANTPNG2D

Jeremiah 23 in the AS21

Jeremiah 23 in the BAGH

Jeremiah 23 in the BBPNG

Jeremiah 23 in the BBT1E

Jeremiah 23 in the BDS

Jeremiah 23 in the BEV

Jeremiah 23 in the BHAD

Jeremiah 23 in the BIB

Jeremiah 23 in the BLPT

Jeremiah 23 in the BNT

Jeremiah 23 in the BNTABOOT

Jeremiah 23 in the BNTLV

Jeremiah 23 in the BOATCB

Jeremiah 23 in the BOATCB2

Jeremiah 23 in the BOBCV

Jeremiah 23 in the BOCNT

Jeremiah 23 in the BOECS

Jeremiah 23 in the BOGWICC

Jeremiah 23 in the BOHCB

Jeremiah 23 in the BOHCV

Jeremiah 23 in the BOHLNT

Jeremiah 23 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 23 in the BOICB

Jeremiah 23 in the BOILNTAP

Jeremiah 23 in the BOITCV

Jeremiah 23 in the BOKCV2

Jeremiah 23 in the BOKHWOG

Jeremiah 23 in the BOKSSV

Jeremiah 23 in the BOLCB

Jeremiah 23 in the BOLCB2

Jeremiah 23 in the BOMCV

Jeremiah 23 in the BONAV

Jeremiah 23 in the BONCB

Jeremiah 23 in the BONLT

Jeremiah 23 in the BONUT2

Jeremiah 23 in the BOPLNT

Jeremiah 23 in the BOSCB

Jeremiah 23 in the BOSNC

Jeremiah 23 in the BOTLNT

Jeremiah 23 in the BOVCB

Jeremiah 23 in the BOYCB

Jeremiah 23 in the BPBB

Jeremiah 23 in the BPH

Jeremiah 23 in the BSB

Jeremiah 23 in the CCB

Jeremiah 23 in the CUV

Jeremiah 23 in the CUVS

Jeremiah 23 in the DBT

Jeremiah 23 in the DGDNT

Jeremiah 23 in the DHNT

Jeremiah 23 in the DNT

Jeremiah 23 in the ELBE

Jeremiah 23 in the EMTV

Jeremiah 23 in the ESV

Jeremiah 23 in the FBV

Jeremiah 23 in the FEB

Jeremiah 23 in the GGMNT

Jeremiah 23 in the GNT

Jeremiah 23 in the HARY

Jeremiah 23 in the HNT

Jeremiah 23 in the IRVA

Jeremiah 23 in the IRVB

Jeremiah 23 in the IRVG

Jeremiah 23 in the IRVH

Jeremiah 23 in the IRVK

Jeremiah 23 in the IRVM

Jeremiah 23 in the IRVM2

Jeremiah 23 in the IRVO

Jeremiah 23 in the IRVP

Jeremiah 23 in the IRVT

Jeremiah 23 in the IRVT2

Jeremiah 23 in the IRVU

Jeremiah 23 in the ISVN

Jeremiah 23 in the JSNT

Jeremiah 23 in the KAPI

Jeremiah 23 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 23 in the KBV

Jeremiah 23 in the KJV

Jeremiah 23 in the KNFD

Jeremiah 23 in the LBA

Jeremiah 23 in the LBLA

Jeremiah 23 in the LNT

Jeremiah 23 in the LSV

Jeremiah 23 in the MAAL

Jeremiah 23 in the MBV

Jeremiah 23 in the MBV2

Jeremiah 23 in the MHNT

Jeremiah 23 in the MKNFD

Jeremiah 23 in the MNG

Jeremiah 23 in the MNT

Jeremiah 23 in the MNT2

Jeremiah 23 in the MRS1T

Jeremiah 23 in the NAA

Jeremiah 23 in the NASB

Jeremiah 23 in the NBLA

Jeremiah 23 in the NBS

Jeremiah 23 in the NBVTP

Jeremiah 23 in the NET2

Jeremiah 23 in the NIV11

Jeremiah 23 in the NNT

Jeremiah 23 in the NNT2

Jeremiah 23 in the NNT3

Jeremiah 23 in the PDDPT

Jeremiah 23 in the PFNT

Jeremiah 23 in the RMNT

Jeremiah 23 in the SBIAS

Jeremiah 23 in the SBIBS

Jeremiah 23 in the SBIBS2

Jeremiah 23 in the SBICS

Jeremiah 23 in the SBIDS

Jeremiah 23 in the SBIGS

Jeremiah 23 in the SBIHS

Jeremiah 23 in the SBIIS

Jeremiah 23 in the SBIIS2

Jeremiah 23 in the SBIIS3

Jeremiah 23 in the SBIKS

Jeremiah 23 in the SBIKS2

Jeremiah 23 in the SBIMS

Jeremiah 23 in the SBIOS

Jeremiah 23 in the SBIPS

Jeremiah 23 in the SBISS

Jeremiah 23 in the SBITS

Jeremiah 23 in the SBITS2

Jeremiah 23 in the SBITS3

Jeremiah 23 in the SBITS4

Jeremiah 23 in the SBIUS

Jeremiah 23 in the SBIVS

Jeremiah 23 in the SBT

Jeremiah 23 in the SBT1E

Jeremiah 23 in the SCHL

Jeremiah 23 in the SNT

Jeremiah 23 in the SUSU

Jeremiah 23 in the SUSU2

Jeremiah 23 in the SYNO

Jeremiah 23 in the TBIAOTANT

Jeremiah 23 in the TBT1E

Jeremiah 23 in the TBT1E2

Jeremiah 23 in the TFTIP

Jeremiah 23 in the TFTU

Jeremiah 23 in the TGNTATF3T

Jeremiah 23 in the THAI

Jeremiah 23 in the TNFD

Jeremiah 23 in the TNT

Jeremiah 23 in the TNTIK

Jeremiah 23 in the TNTIL

Jeremiah 23 in the TNTIN

Jeremiah 23 in the TNTIP

Jeremiah 23 in the TNTIZ

Jeremiah 23 in the TOMA

Jeremiah 23 in the TTENT

Jeremiah 23 in the UBG

Jeremiah 23 in the UGV

Jeremiah 23 in the UGV2

Jeremiah 23 in the UGV3

Jeremiah 23 in the VBL

Jeremiah 23 in the VDCC

Jeremiah 23 in the YALU

Jeremiah 23 in the YAPE

Jeremiah 23 in the YBVTP

Jeremiah 23 in the ZBP