Jeremiah 4 (BOKCV)

1 “Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli,nirudie mimi,”asema BWANA.“Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yanguna usiendelee kutangatanga, 2 ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa,‘Kwa hakika kama vile BWANA aishivyo,’ndipo mataifa yatakapobarikiwa nayena katika yeye watajitukuza.” 3 Hili ndilo asemalo BWANA kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu:“Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu,wala msipande katikati ya miiba. 4 Jitahirini katika BWANA,tahirini mioyo yenu,enyi wanaume wa Yudana watu wa Yerusalemu,la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvuna kuwaka kama motokwa sababu ya uovu mliotenda,ikiwaka pasipo wa kuizima. 5 “Tangaza katika Yuda na upige mbiu katika Yerusalemu na kusema:‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’Piga kelele na kusema:‘Kusanyikeni pamoja!Tukimbilie katika miji yenye maboma!’ 6 Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni!Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa!Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini,maangamizi ya kutisha.” 7 Simba ametoka nje ya pango lake,mharabu wa mataifa amejipanga.Ametoka mahali pakeili aangamize nchi yenu.Miji yenu itakuwa magofupasipo mtu wa kuishi humo. 8 Hivyo vaeni nguo za magunia,ombolezeni na kulia kwa huzuni,kwa kuwa hasira kali ya BWANAhaijaondolewa kwetu. 9 “Katika siku ile,” asema BWANA“mfalme na maafisa watakata tamaa,makuhani watafadhaika,na manabii watashangazwa mno.” 10 Ndipo niliposema, “Aa, BWANA Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!” 11 Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa, 12 upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.” 13 Tazama! Anakuja kama mawingu,magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,farasi wake wana mbio kuliko tai.Ole wetu! Tunaangamia! 14 Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini? 15 Sauti inatangaza kutoka Dani,ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu. 16 “Waambie mataifa jambo hili,piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu:‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali,likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda. 17 Wamemzunguka kama watu walindao shamba,kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ”asema BWANA. 18 “Mwenendo wako na matendo yako mwenyeweyameleta haya juu yako.Hii ndiyo adhabu yako.Tazama jinsi ilivyo chungu!Tazama jinsi inavyochoma moyo!” 19 Ee mtima wangu, mtima wangu!Ninagaagaa kwa maumivu.Ee maumivu makuu ya moyo wangu!Moyo wangu umefadhaika ndani yangu,siwezi kunyamaza.Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta,nimesikia kelele ya vita. 20 Maafa baada ya maafa,nchi yote imekuwa magofu.Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa,makazi yangu kwa muda mfupi. 21 Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vitana kusikia sauti za tarumbeta? 22 “Watu wangu ni wapumbavu,hawanijui mimi.Ni watoto wasio na akili,hawana ufahamu.Ni hodari kutenda mabaya,hawajui kutenda yaliyo mema.” 23 Niliitazama dunia,nayo haikuwa na umbo tena ni tupu;niliziangalia mbingu,mianga ilikuwa imetoweka. 24 Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka,vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba. 25 Nilitazama, wala watu hawakuwepo;kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. 26 Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,miji yake yote ilikuwa magofumbele za BWANA,mbele ya hasira yake kali. 27 Hivi ndivyo BWANA asemavyo:“Nchi yote itaharibiwa,ingawa sitaiangamiza kabisa. 28 Kwa hiyo dunia itaombolezana mbingu zilizo juu zitakuwa giza,kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,nimeamua na wala sitageuka.” 29 Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upindekila mji unakimbia.Baadhi wanakimbilia vichakani,baadhi wanapanda juu ya miamba.Miji yote imeachwa,hakuna aishiye ndani yake. 30 Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa?Kwa nini unajivika vazi jekunduna kuvaa vito vya dhahabu?Kwa nini unapaka macho yako rangi?Unajipamba bure.Wapenzi wako wanakudharau,wanautafuta uhai wako. 31 Nasikia kilio kama cha mwanamkekatika utungu wa kuzaa,kilio cha uchungu kama cha anayemzaamtoto wake wa kwanza:kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua,akiinua mikono yake, akisema,“Ole wangu! Ninazimia;maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”

In Other Versions

Jeremiah 4 in the ANGEFD

Jeremiah 4 in the ANTPNG2D

Jeremiah 4 in the AS21

Jeremiah 4 in the BAGH

Jeremiah 4 in the BBPNG

Jeremiah 4 in the BBT1E

Jeremiah 4 in the BDS

Jeremiah 4 in the BEV

Jeremiah 4 in the BHAD

Jeremiah 4 in the BIB

Jeremiah 4 in the BLPT

Jeremiah 4 in the BNT

Jeremiah 4 in the BNTABOOT

Jeremiah 4 in the BNTLV

Jeremiah 4 in the BOATCB

Jeremiah 4 in the BOATCB2

Jeremiah 4 in the BOBCV

Jeremiah 4 in the BOCNT

Jeremiah 4 in the BOECS

Jeremiah 4 in the BOGWICC

Jeremiah 4 in the BOHCB

Jeremiah 4 in the BOHCV

Jeremiah 4 in the BOHLNT

Jeremiah 4 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 4 in the BOICB

Jeremiah 4 in the BOILNTAP

Jeremiah 4 in the BOITCV

Jeremiah 4 in the BOKCV2

Jeremiah 4 in the BOKHWOG

Jeremiah 4 in the BOKSSV

Jeremiah 4 in the BOLCB

Jeremiah 4 in the BOLCB2

Jeremiah 4 in the BOMCV

Jeremiah 4 in the BONAV

Jeremiah 4 in the BONCB

Jeremiah 4 in the BONLT

Jeremiah 4 in the BONUT2

Jeremiah 4 in the BOPLNT

Jeremiah 4 in the BOSCB

Jeremiah 4 in the BOSNC

Jeremiah 4 in the BOTLNT

Jeremiah 4 in the BOVCB

Jeremiah 4 in the BOYCB

Jeremiah 4 in the BPBB

Jeremiah 4 in the BPH

Jeremiah 4 in the BSB

Jeremiah 4 in the CCB

Jeremiah 4 in the CUV

Jeremiah 4 in the CUVS

Jeremiah 4 in the DBT

Jeremiah 4 in the DGDNT

Jeremiah 4 in the DHNT

Jeremiah 4 in the DNT

Jeremiah 4 in the ELBE

Jeremiah 4 in the EMTV

Jeremiah 4 in the ESV

Jeremiah 4 in the FBV

Jeremiah 4 in the FEB

Jeremiah 4 in the GGMNT

Jeremiah 4 in the GNT

Jeremiah 4 in the HARY

Jeremiah 4 in the HNT

Jeremiah 4 in the IRVA

Jeremiah 4 in the IRVB

Jeremiah 4 in the IRVG

Jeremiah 4 in the IRVH

Jeremiah 4 in the IRVK

Jeremiah 4 in the IRVM

Jeremiah 4 in the IRVM2

Jeremiah 4 in the IRVO

Jeremiah 4 in the IRVP

Jeremiah 4 in the IRVT

Jeremiah 4 in the IRVT2

Jeremiah 4 in the IRVU

Jeremiah 4 in the ISVN

Jeremiah 4 in the JSNT

Jeremiah 4 in the KAPI

Jeremiah 4 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 4 in the KBV

Jeremiah 4 in the KJV

Jeremiah 4 in the KNFD

Jeremiah 4 in the LBA

Jeremiah 4 in the LBLA

Jeremiah 4 in the LNT

Jeremiah 4 in the LSV

Jeremiah 4 in the MAAL

Jeremiah 4 in the MBV

Jeremiah 4 in the MBV2

Jeremiah 4 in the MHNT

Jeremiah 4 in the MKNFD

Jeremiah 4 in the MNG

Jeremiah 4 in the MNT

Jeremiah 4 in the MNT2

Jeremiah 4 in the MRS1T

Jeremiah 4 in the NAA

Jeremiah 4 in the NASB

Jeremiah 4 in the NBLA

Jeremiah 4 in the NBS

Jeremiah 4 in the NBVTP

Jeremiah 4 in the NET2

Jeremiah 4 in the NIV11

Jeremiah 4 in the NNT

Jeremiah 4 in the NNT2

Jeremiah 4 in the NNT3

Jeremiah 4 in the PDDPT

Jeremiah 4 in the PFNT

Jeremiah 4 in the RMNT

Jeremiah 4 in the SBIAS

Jeremiah 4 in the SBIBS

Jeremiah 4 in the SBIBS2

Jeremiah 4 in the SBICS

Jeremiah 4 in the SBIDS

Jeremiah 4 in the SBIGS

Jeremiah 4 in the SBIHS

Jeremiah 4 in the SBIIS

Jeremiah 4 in the SBIIS2

Jeremiah 4 in the SBIIS3

Jeremiah 4 in the SBIKS

Jeremiah 4 in the SBIKS2

Jeremiah 4 in the SBIMS

Jeremiah 4 in the SBIOS

Jeremiah 4 in the SBIPS

Jeremiah 4 in the SBISS

Jeremiah 4 in the SBITS

Jeremiah 4 in the SBITS2

Jeremiah 4 in the SBITS3

Jeremiah 4 in the SBITS4

Jeremiah 4 in the SBIUS

Jeremiah 4 in the SBIVS

Jeremiah 4 in the SBT

Jeremiah 4 in the SBT1E

Jeremiah 4 in the SCHL

Jeremiah 4 in the SNT

Jeremiah 4 in the SUSU

Jeremiah 4 in the SUSU2

Jeremiah 4 in the SYNO

Jeremiah 4 in the TBIAOTANT

Jeremiah 4 in the TBT1E

Jeremiah 4 in the TBT1E2

Jeremiah 4 in the TFTIP

Jeremiah 4 in the TFTU

Jeremiah 4 in the TGNTATF3T

Jeremiah 4 in the THAI

Jeremiah 4 in the TNFD

Jeremiah 4 in the TNT

Jeremiah 4 in the TNTIK

Jeremiah 4 in the TNTIL

Jeremiah 4 in the TNTIN

Jeremiah 4 in the TNTIP

Jeremiah 4 in the TNTIZ

Jeremiah 4 in the TOMA

Jeremiah 4 in the TTENT

Jeremiah 4 in the UBG

Jeremiah 4 in the UGV

Jeremiah 4 in the UGV2

Jeremiah 4 in the UGV3

Jeremiah 4 in the VBL

Jeremiah 4 in the VDCC

Jeremiah 4 in the YALU

Jeremiah 4 in the YAPE

Jeremiah 4 in the YBVTP

Jeremiah 4 in the ZBP