Matthew 14 (BOKCV)
1 Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Yesu, 2 akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” 3 Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 4 kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 5 Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. 6 Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, 7 kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. 8 Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9 Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 10 Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. 11 Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. 12 Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu. 13 Yesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 14 Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao. 15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.” 16 Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 19 Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 20 Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto. 22 Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ngʼambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 23 Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake. 24 Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. 25 Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa. 27 Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.” 28 Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29 Yesu akamwambia, “Njoo.”Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!” 31 Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?” 32 Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. 33 Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.” 34 Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti. 35 Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, 36 wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa.
In Other Versions
Matthew 14 in the ANGEFD
Matthew 14 in the ANTPNG2D
Matthew 14 in the AS21
Matthew 14 in the BAGH
Matthew 14 in the BBPNG
Matthew 14 in the BBT1E
Matthew 14 in the BDS
Matthew 14 in the BEV
Matthew 14 in the BHAD
Matthew 14 in the BIB
Matthew 14 in the BLPT
Matthew 14 in the BNT
Matthew 14 in the BNTABOOT
Matthew 14 in the BNTLV
Matthew 14 in the BOATCB
Matthew 14 in the BOATCB2
Matthew 14 in the BOBCV
Matthew 14 in the BOCNT
Matthew 14 in the BOECS
Matthew 14 in the BOGWICC
Matthew 14 in the BOHCB
Matthew 14 in the BOHCV
Matthew 14 in the BOHLNT
Matthew 14 in the BOHNTLTAL
Matthew 14 in the BOICB
Matthew 14 in the BOILNTAP
Matthew 14 in the BOITCV
Matthew 14 in the BOKCV2
Matthew 14 in the BOKHWOG
Matthew 14 in the BOKSSV
Matthew 14 in the BOLCB
Matthew 14 in the BOLCB2
Matthew 14 in the BOMCV
Matthew 14 in the BONAV
Matthew 14 in the BONCB
Matthew 14 in the BONLT
Matthew 14 in the BONUT2
Matthew 14 in the BOPLNT
Matthew 14 in the BOSCB
Matthew 14 in the BOSNC
Matthew 14 in the BOTLNT
Matthew 14 in the BOVCB
Matthew 14 in the BOYCB
Matthew 14 in the BPBB
Matthew 14 in the BPH
Matthew 14 in the BSB
Matthew 14 in the CCB
Matthew 14 in the CUV
Matthew 14 in the CUVS
Matthew 14 in the DBT
Matthew 14 in the DGDNT
Matthew 14 in the DHNT
Matthew 14 in the DNT
Matthew 14 in the ELBE
Matthew 14 in the EMTV
Matthew 14 in the ESV
Matthew 14 in the FBV
Matthew 14 in the FEB
Matthew 14 in the GGMNT
Matthew 14 in the GNT
Matthew 14 in the HARY
Matthew 14 in the HNT
Matthew 14 in the IRVA
Matthew 14 in the IRVB
Matthew 14 in the IRVG
Matthew 14 in the IRVH
Matthew 14 in the IRVK
Matthew 14 in the IRVM
Matthew 14 in the IRVM2
Matthew 14 in the IRVO
Matthew 14 in the IRVP
Matthew 14 in the IRVT
Matthew 14 in the IRVT2
Matthew 14 in the IRVU
Matthew 14 in the ISVN
Matthew 14 in the JSNT
Matthew 14 in the KAPI
Matthew 14 in the KBT1ETNIK
Matthew 14 in the KBV
Matthew 14 in the KJV
Matthew 14 in the KNFD
Matthew 14 in the LBA
Matthew 14 in the LBLA
Matthew 14 in the LNT
Matthew 14 in the LSV
Matthew 14 in the MAAL
Matthew 14 in the MBV
Matthew 14 in the MBV2
Matthew 14 in the MHNT
Matthew 14 in the MKNFD
Matthew 14 in the MNG
Matthew 14 in the MNT
Matthew 14 in the MNT2
Matthew 14 in the MRS1T
Matthew 14 in the NAA
Matthew 14 in the NASB
Matthew 14 in the NBLA
Matthew 14 in the NBS
Matthew 14 in the NBVTP
Matthew 14 in the NET2
Matthew 14 in the NIV11
Matthew 14 in the NNT
Matthew 14 in the NNT2
Matthew 14 in the NNT3
Matthew 14 in the PDDPT
Matthew 14 in the PFNT
Matthew 14 in the RMNT
Matthew 14 in the SBIAS
Matthew 14 in the SBIBS
Matthew 14 in the SBIBS2
Matthew 14 in the SBICS
Matthew 14 in the SBIDS
Matthew 14 in the SBIGS
Matthew 14 in the SBIHS
Matthew 14 in the SBIIS
Matthew 14 in the SBIIS2
Matthew 14 in the SBIIS3
Matthew 14 in the SBIKS
Matthew 14 in the SBIKS2
Matthew 14 in the SBIMS
Matthew 14 in the SBIOS
Matthew 14 in the SBIPS
Matthew 14 in the SBISS
Matthew 14 in the SBITS
Matthew 14 in the SBITS2
Matthew 14 in the SBITS3
Matthew 14 in the SBITS4
Matthew 14 in the SBIUS
Matthew 14 in the SBIVS
Matthew 14 in the SBT
Matthew 14 in the SBT1E
Matthew 14 in the SCHL
Matthew 14 in the SNT
Matthew 14 in the SUSU
Matthew 14 in the SUSU2
Matthew 14 in the SYNO
Matthew 14 in the TBIAOTANT
Matthew 14 in the TBT1E
Matthew 14 in the TBT1E2
Matthew 14 in the TFTIP
Matthew 14 in the TFTU
Matthew 14 in the TGNTATF3T
Matthew 14 in the THAI
Matthew 14 in the TNFD
Matthew 14 in the TNT
Matthew 14 in the TNTIK
Matthew 14 in the TNTIL
Matthew 14 in the TNTIN
Matthew 14 in the TNTIP
Matthew 14 in the TNTIZ
Matthew 14 in the TOMA
Matthew 14 in the TTENT
Matthew 14 in the UBG
Matthew 14 in the UGV
Matthew 14 in the UGV2
Matthew 14 in the UGV3
Matthew 14 in the VBL
Matthew 14 in the VDCC
Matthew 14 in the YALU
Matthew 14 in the YAPE
Matthew 14 in the YBVTP
Matthew 14 in the ZBP