Psalms 127 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. 1 BWANA asipoijenga nyumba,wajengao hufanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji,walinzi wakesha bure. 2 Mnajisumbua bure kuamka mapemana kuchelewa kulala,mkitaabikia chakula:kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake. 3 Wana ni urithi utokao kwa BWANA,watoto ni zawadi kutoka kwake. 4 Kama mishale mikononi mwa shujaandivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. 5 Heri mtu ambaye podo lakelimejazwa nao.Hawataaibishwa wanaposhindanana adui zao langoni.