Acts 11 (BOKCV)

1 Mitume na ndugu walioamini waliokuwa huko Uyahudi wakasikia kuwa watu wa Mataifa nao wamepokea neno la Mungu. 2 Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, wale wa tohara waliokuwa wameamini wakamshutumu, 3 wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” 4 Ndipo Petro akaanza kuwaeleza kuhusu mambo yote yalivyotokea hatua kwa hatua akisema, 5 “Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia. 6 Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama wa mwitu, watambaao na ndege wa angani. 7 Ndipo nikasikia sauti ikiniambia, ‘Petro, ondoka uchinje na ule.’ 8 “Nikajibu, ‘La hasha Bwana! Kitu chochote kilicho najisi hakijaingia kinywani mwangu.’ 9 “Sauti ikasema kutoka mbinguni mara ya pili, ‘Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.’ 10 Jambo hili lilitokea mara tatu, ndipo kile kitu kikavutwa tena mbinguni. 11 “Wakati ule ule watu watatu, waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria waliwasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. 12 Roho Mtakatifu akaniambia niende nao bila kuwa na ubaguzi kati yao na sisi. Hawa ndugu sita pia walifuatana nami, nasi tukaingia nyumbani mwa huyo Kornelio. 13 Akatuambia jinsi alivyoona malaika aliyekuwa amesimama katika nyumba yake na kusema, ‘Tuma watu waende Yafa wakamlete Simoni aitwaye Petro. 14 Yeye atakupa ujumbe ambao kwa huo wewe na wa nyumbani mwako wote mtaokoka.’ 15 “Nami nilipoanza kusema, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama vile alivyotushukia sisi hapo mwanzo. 16 Nami nikakumbuka neno la Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu.’ 17 Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?” 18 Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.” 19 Basi wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, wakasafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Nao hawakuhubiri lile Neno kwa mtu yeyote isipokuwa Wayahudi. 20 Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Yesu. 21 Mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana. 22 Habari hizi zilipofika masikioni mwa kanisa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba aende Antiokia. 23 Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote. 24 Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana. 25 Kisha Barnaba akaenda Tarso kumtafuta Sauli, 26 naye alipompata akamleta Antiokia. Hivyo kwa mwaka mzima Barnaba na Sauli wakakutana na kanisa na kufundisha idadi kubwa ya watu. Ilikuwa ni katika kanisa la Antiokia kwa mara ya kwanza wanafunzi waliitwa Wakristo. 27 Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia. 28 Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio. 29 Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Uyahudi. 30 Wakafanya hivyo, misaada yao ikapelekwa kwa wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.

In Other Versions

Acts 11 in the ANGEFD

Acts 11 in the ANTPNG2D

Acts 11 in the AS21

Acts 11 in the BAGH

Acts 11 in the BBPNG

Acts 11 in the BBT1E

Acts 11 in the BDS

Acts 11 in the BEV

Acts 11 in the BHAD

Acts 11 in the BIB

Acts 11 in the BLPT

Acts 11 in the BNT

Acts 11 in the BNTABOOT

Acts 11 in the BNTLV

Acts 11 in the BOATCB

Acts 11 in the BOATCB2

Acts 11 in the BOBCV

Acts 11 in the BOCNT

Acts 11 in the BOECS

Acts 11 in the BOGWICC

Acts 11 in the BOHCB

Acts 11 in the BOHCV

Acts 11 in the BOHLNT

Acts 11 in the BOHNTLTAL

Acts 11 in the BOICB

Acts 11 in the BOILNTAP

Acts 11 in the BOITCV

Acts 11 in the BOKCV2

Acts 11 in the BOKHWOG

Acts 11 in the BOKSSV

Acts 11 in the BOLCB

Acts 11 in the BOLCB2

Acts 11 in the BOMCV

Acts 11 in the BONAV

Acts 11 in the BONCB

Acts 11 in the BONLT

Acts 11 in the BONUT2

Acts 11 in the BOPLNT

Acts 11 in the BOSCB

Acts 11 in the BOSNC

Acts 11 in the BOTLNT

Acts 11 in the BOVCB

Acts 11 in the BOYCB

Acts 11 in the BPBB

Acts 11 in the BPH

Acts 11 in the BSB

Acts 11 in the CCB

Acts 11 in the CUV

Acts 11 in the CUVS

Acts 11 in the DBT

Acts 11 in the DGDNT

Acts 11 in the DHNT

Acts 11 in the DNT

Acts 11 in the ELBE

Acts 11 in the EMTV

Acts 11 in the ESV

Acts 11 in the FBV

Acts 11 in the FEB

Acts 11 in the GGMNT

Acts 11 in the GNT

Acts 11 in the HARY

Acts 11 in the HNT

Acts 11 in the IRVA

Acts 11 in the IRVB

Acts 11 in the IRVG

Acts 11 in the IRVH

Acts 11 in the IRVK

Acts 11 in the IRVM

Acts 11 in the IRVM2

Acts 11 in the IRVO

Acts 11 in the IRVP

Acts 11 in the IRVT

Acts 11 in the IRVT2

Acts 11 in the IRVU

Acts 11 in the ISVN

Acts 11 in the JSNT

Acts 11 in the KAPI

Acts 11 in the KBT1ETNIK

Acts 11 in the KBV

Acts 11 in the KJV

Acts 11 in the KNFD

Acts 11 in the LBA

Acts 11 in the LBLA

Acts 11 in the LNT

Acts 11 in the LSV

Acts 11 in the MAAL

Acts 11 in the MBV

Acts 11 in the MBV2

Acts 11 in the MHNT

Acts 11 in the MKNFD

Acts 11 in the MNG

Acts 11 in the MNT

Acts 11 in the MNT2

Acts 11 in the MRS1T

Acts 11 in the NAA

Acts 11 in the NASB

Acts 11 in the NBLA

Acts 11 in the NBS

Acts 11 in the NBVTP

Acts 11 in the NET2

Acts 11 in the NIV11

Acts 11 in the NNT

Acts 11 in the NNT2

Acts 11 in the NNT3

Acts 11 in the PDDPT

Acts 11 in the PFNT

Acts 11 in the RMNT

Acts 11 in the SBIAS

Acts 11 in the SBIBS

Acts 11 in the SBIBS2

Acts 11 in the SBICS

Acts 11 in the SBIDS

Acts 11 in the SBIGS

Acts 11 in the SBIHS

Acts 11 in the SBIIS

Acts 11 in the SBIIS2

Acts 11 in the SBIIS3

Acts 11 in the SBIKS

Acts 11 in the SBIKS2

Acts 11 in the SBIMS

Acts 11 in the SBIOS

Acts 11 in the SBIPS

Acts 11 in the SBISS

Acts 11 in the SBITS

Acts 11 in the SBITS2

Acts 11 in the SBITS3

Acts 11 in the SBITS4

Acts 11 in the SBIUS

Acts 11 in the SBIVS

Acts 11 in the SBT

Acts 11 in the SBT1E

Acts 11 in the SCHL

Acts 11 in the SNT

Acts 11 in the SUSU

Acts 11 in the SUSU2

Acts 11 in the SYNO

Acts 11 in the TBIAOTANT

Acts 11 in the TBT1E

Acts 11 in the TBT1E2

Acts 11 in the TFTIP

Acts 11 in the TFTU

Acts 11 in the TGNTATF3T

Acts 11 in the THAI

Acts 11 in the TNFD

Acts 11 in the TNT

Acts 11 in the TNTIK

Acts 11 in the TNTIL

Acts 11 in the TNTIN

Acts 11 in the TNTIP

Acts 11 in the TNTIZ

Acts 11 in the TOMA

Acts 11 in the TTENT

Acts 11 in the UBG

Acts 11 in the UGV

Acts 11 in the UGV2

Acts 11 in the UGV3

Acts 11 in the VBL

Acts 11 in the VDCC

Acts 11 in the YALU

Acts 11 in the YAPE

Acts 11 in the YBVTP

Acts 11 in the ZBP