Ezekiel 7 (BOKCV)

1 Neno la BWANA likanijia kusema: 2 “Mwanadamu, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kwa nchi ya Israeli: Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi. 3 Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. 4 Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA. 5 “Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa yanakuja. 6 Mwisho umewadia! Mwisho umewadia! Umejiinua wenyewe dhidi yenu. Umewadia! 7 Maangamizi yamekuja juu yenu, ninyi mnaoishi katika nchi. Wakati umewadia, siku imekaribia, kuna hofu kuu ya ghafula, wala si furaha, juu ya milima. 8 Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu na kumaliza hasira yangu dhidi yenu, nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo. 9 Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA ambaye huwapiga kwa mapigo. 10 “Siku imefika! Imewadia! Maangamizi yamezuka ghafula, fimbo imechanua majivuno yamechipua! 11 Jeuri imeinuka kuwa fimbo ya kuadhibu uovu, hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, hata mmoja wa kundi lile, hakuna utajiri, hakuna chenye thamani. 12 Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na asifurahi wala muuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote. 13 Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai, kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake. 14 Wajapopiga tarumbeta na kuweka kila kitu tayari, hakuna hata mmoja atakayekwenda vitani, kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote. 15 “Nje ni upanga, ndani ni tauni na njaa, wale walioko shambani watakufa kwa upanga, nao wale waliomo mjini njaa na tauni vitawala. 16 Wale wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake. 17 Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. 18 Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa. 19 Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya BWANA. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini. 20 Walijivunia vito vyao vizuri na kuvitumia kufanya sanamu za machukizo na vinyago vya upotovu. Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao. 21 Nitavitia vyote mikononi mwa wageni kuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia, nao watavinajisi. 22 Nitageuza uso wangu mbali nao, nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani, wanyangʼanyi watapaingia na kupanajisi. 23 “Andaa minyororo, kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu na mji umejaa udhalimu. 24 Nitaleta taifa ovu kuliko yote ili kumiliki nyumba zao, nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi. 25 Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitakuwepo. 26 Maafa juu ya maafa yatakuja, tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii, mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee. 27 Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi BWANA.”

In Other Versions

Ezekiel 7 in the ANGEFD

Ezekiel 7 in the ANTPNG2D

Ezekiel 7 in the AS21

Ezekiel 7 in the BAGH

Ezekiel 7 in the BBPNG

Ezekiel 7 in the BBT1E

Ezekiel 7 in the BDS

Ezekiel 7 in the BEV

Ezekiel 7 in the BHAD

Ezekiel 7 in the BIB

Ezekiel 7 in the BLPT

Ezekiel 7 in the BNT

Ezekiel 7 in the BNTABOOT

Ezekiel 7 in the BNTLV

Ezekiel 7 in the BOATCB

Ezekiel 7 in the BOATCB2

Ezekiel 7 in the BOBCV

Ezekiel 7 in the BOCNT

Ezekiel 7 in the BOECS

Ezekiel 7 in the BOGWICC

Ezekiel 7 in the BOHCB

Ezekiel 7 in the BOHCV

Ezekiel 7 in the BOHLNT

Ezekiel 7 in the BOHNTLTAL

Ezekiel 7 in the BOICB

Ezekiel 7 in the BOILNTAP

Ezekiel 7 in the BOITCV

Ezekiel 7 in the BOKCV2

Ezekiel 7 in the BOKHWOG

Ezekiel 7 in the BOKSSV

Ezekiel 7 in the BOLCB

Ezekiel 7 in the BOLCB2

Ezekiel 7 in the BOMCV

Ezekiel 7 in the BONAV

Ezekiel 7 in the BONCB

Ezekiel 7 in the BONLT

Ezekiel 7 in the BONUT2

Ezekiel 7 in the BOPLNT

Ezekiel 7 in the BOSCB

Ezekiel 7 in the BOSNC

Ezekiel 7 in the BOTLNT

Ezekiel 7 in the BOVCB

Ezekiel 7 in the BOYCB

Ezekiel 7 in the BPBB

Ezekiel 7 in the BPH

Ezekiel 7 in the BSB

Ezekiel 7 in the CCB

Ezekiel 7 in the CUV

Ezekiel 7 in the CUVS

Ezekiel 7 in the DBT

Ezekiel 7 in the DGDNT

Ezekiel 7 in the DHNT

Ezekiel 7 in the DNT

Ezekiel 7 in the ELBE

Ezekiel 7 in the EMTV

Ezekiel 7 in the ESV

Ezekiel 7 in the FBV

Ezekiel 7 in the FEB

Ezekiel 7 in the GGMNT

Ezekiel 7 in the GNT

Ezekiel 7 in the HARY

Ezekiel 7 in the HNT

Ezekiel 7 in the IRVA

Ezekiel 7 in the IRVB

Ezekiel 7 in the IRVG

Ezekiel 7 in the IRVH

Ezekiel 7 in the IRVK

Ezekiel 7 in the IRVM

Ezekiel 7 in the IRVM2

Ezekiel 7 in the IRVO

Ezekiel 7 in the IRVP

Ezekiel 7 in the IRVT

Ezekiel 7 in the IRVT2

Ezekiel 7 in the IRVU

Ezekiel 7 in the ISVN

Ezekiel 7 in the JSNT

Ezekiel 7 in the KAPI

Ezekiel 7 in the KBT1ETNIK

Ezekiel 7 in the KBV

Ezekiel 7 in the KJV

Ezekiel 7 in the KNFD

Ezekiel 7 in the LBA

Ezekiel 7 in the LBLA

Ezekiel 7 in the LNT

Ezekiel 7 in the LSV

Ezekiel 7 in the MAAL

Ezekiel 7 in the MBV

Ezekiel 7 in the MBV2

Ezekiel 7 in the MHNT

Ezekiel 7 in the MKNFD

Ezekiel 7 in the MNG

Ezekiel 7 in the MNT

Ezekiel 7 in the MNT2

Ezekiel 7 in the MRS1T

Ezekiel 7 in the NAA

Ezekiel 7 in the NASB

Ezekiel 7 in the NBLA

Ezekiel 7 in the NBS

Ezekiel 7 in the NBVTP

Ezekiel 7 in the NET2

Ezekiel 7 in the NIV11

Ezekiel 7 in the NNT

Ezekiel 7 in the NNT2

Ezekiel 7 in the NNT3

Ezekiel 7 in the PDDPT

Ezekiel 7 in the PFNT

Ezekiel 7 in the RMNT

Ezekiel 7 in the SBIAS

Ezekiel 7 in the SBIBS

Ezekiel 7 in the SBIBS2

Ezekiel 7 in the SBICS

Ezekiel 7 in the SBIDS

Ezekiel 7 in the SBIGS

Ezekiel 7 in the SBIHS

Ezekiel 7 in the SBIIS

Ezekiel 7 in the SBIIS2

Ezekiel 7 in the SBIIS3

Ezekiel 7 in the SBIKS

Ezekiel 7 in the SBIKS2

Ezekiel 7 in the SBIMS

Ezekiel 7 in the SBIOS

Ezekiel 7 in the SBIPS

Ezekiel 7 in the SBISS

Ezekiel 7 in the SBITS

Ezekiel 7 in the SBITS2

Ezekiel 7 in the SBITS3

Ezekiel 7 in the SBITS4

Ezekiel 7 in the SBIUS

Ezekiel 7 in the SBIVS

Ezekiel 7 in the SBT

Ezekiel 7 in the SBT1E

Ezekiel 7 in the SCHL

Ezekiel 7 in the SNT

Ezekiel 7 in the SUSU

Ezekiel 7 in the SUSU2

Ezekiel 7 in the SYNO

Ezekiel 7 in the TBIAOTANT

Ezekiel 7 in the TBT1E

Ezekiel 7 in the TBT1E2

Ezekiel 7 in the TFTIP

Ezekiel 7 in the TFTU

Ezekiel 7 in the TGNTATF3T

Ezekiel 7 in the THAI

Ezekiel 7 in the TNFD

Ezekiel 7 in the TNT

Ezekiel 7 in the TNTIK

Ezekiel 7 in the TNTIL

Ezekiel 7 in the TNTIN

Ezekiel 7 in the TNTIP

Ezekiel 7 in the TNTIZ

Ezekiel 7 in the TOMA

Ezekiel 7 in the TTENT

Ezekiel 7 in the UBG

Ezekiel 7 in the UGV

Ezekiel 7 in the UGV2

Ezekiel 7 in the UGV3

Ezekiel 7 in the VBL

Ezekiel 7 in the VDCC

Ezekiel 7 in the YALU

Ezekiel 7 in the YAPE

Ezekiel 7 in the YBVTP

Ezekiel 7 in the ZBP