Hebrews 13 (BOKCV)
1 Endeleeni kupendana kama ndugu. 2 Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua. 3 Wakumbukeni wale waliofungwa gerezani kana kwamba ninyi mmefungwa pamoja nao. Pia wakumbukeni wale wanaotendewa vibaya, kana kwamba ni ninyi wenyewe mnateswa. 4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote. 5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,“Kamwe sitakuacha,wala sitakupungukia.” 6 Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,“Bwana ni msaada wangu; sitaogopa.Mwanadamu anaweza kunitenda nini?” 7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao. 8 Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. 9 Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria. 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema hawana haki ya kula vile vitu vilivyowekwa juu yake. 11 Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. 12 Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe. 13 Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. 14 Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao. 15 Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake. 16 Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu. 17 Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu. 18 Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia. 19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi. 20 Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, 21 awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen. 22 Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu. 23 Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona. 24 Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu. 25 Neema iwe nanyi nyote. Amen.
In Other Versions
Hebrews 13 in the ANGEFD
Hebrews 13 in the ANTPNG2D
Hebrews 13 in the AS21
Hebrews 13 in the BAGH
Hebrews 13 in the BBPNG
Hebrews 13 in the BBT1E
Hebrews 13 in the BDS
Hebrews 13 in the BEV
Hebrews 13 in the BHAD
Hebrews 13 in the BIB
Hebrews 13 in the BLPT
Hebrews 13 in the BNT
Hebrews 13 in the BNTABOOT
Hebrews 13 in the BNTLV
Hebrews 13 in the BOATCB
Hebrews 13 in the BOATCB2
Hebrews 13 in the BOBCV
Hebrews 13 in the BOCNT
Hebrews 13 in the BOECS
Hebrews 13 in the BOGWICC
Hebrews 13 in the BOHCB
Hebrews 13 in the BOHCV
Hebrews 13 in the BOHLNT
Hebrews 13 in the BOHNTLTAL
Hebrews 13 in the BOICB
Hebrews 13 in the BOILNTAP
Hebrews 13 in the BOITCV
Hebrews 13 in the BOKCV2
Hebrews 13 in the BOKHWOG
Hebrews 13 in the BOKSSV
Hebrews 13 in the BOLCB
Hebrews 13 in the BOLCB2
Hebrews 13 in the BOMCV
Hebrews 13 in the BONAV
Hebrews 13 in the BONCB
Hebrews 13 in the BONLT
Hebrews 13 in the BONUT2
Hebrews 13 in the BOPLNT
Hebrews 13 in the BOSCB
Hebrews 13 in the BOSNC
Hebrews 13 in the BOTLNT
Hebrews 13 in the BOVCB
Hebrews 13 in the BOYCB
Hebrews 13 in the BPBB
Hebrews 13 in the BPH
Hebrews 13 in the BSB
Hebrews 13 in the CCB
Hebrews 13 in the CUV
Hebrews 13 in the CUVS
Hebrews 13 in the DBT
Hebrews 13 in the DGDNT
Hebrews 13 in the DHNT
Hebrews 13 in the DNT
Hebrews 13 in the ELBE
Hebrews 13 in the EMTV
Hebrews 13 in the ESV
Hebrews 13 in the FBV
Hebrews 13 in the FEB
Hebrews 13 in the GGMNT
Hebrews 13 in the GNT
Hebrews 13 in the HARY
Hebrews 13 in the HNT
Hebrews 13 in the IRVA
Hebrews 13 in the IRVB
Hebrews 13 in the IRVG
Hebrews 13 in the IRVH
Hebrews 13 in the IRVK
Hebrews 13 in the IRVM
Hebrews 13 in the IRVM2
Hebrews 13 in the IRVO
Hebrews 13 in the IRVP
Hebrews 13 in the IRVT
Hebrews 13 in the IRVT2
Hebrews 13 in the IRVU
Hebrews 13 in the ISVN
Hebrews 13 in the JSNT
Hebrews 13 in the KAPI
Hebrews 13 in the KBT1ETNIK
Hebrews 13 in the KBV
Hebrews 13 in the KJV
Hebrews 13 in the KNFD
Hebrews 13 in the LBA
Hebrews 13 in the LBLA
Hebrews 13 in the LNT
Hebrews 13 in the LSV
Hebrews 13 in the MAAL
Hebrews 13 in the MBV
Hebrews 13 in the MBV2
Hebrews 13 in the MHNT
Hebrews 13 in the MKNFD
Hebrews 13 in the MNG
Hebrews 13 in the MNT
Hebrews 13 in the MNT2
Hebrews 13 in the MRS1T
Hebrews 13 in the NAA
Hebrews 13 in the NASB
Hebrews 13 in the NBLA
Hebrews 13 in the NBS
Hebrews 13 in the NBVTP
Hebrews 13 in the NET2
Hebrews 13 in the NIV11
Hebrews 13 in the NNT
Hebrews 13 in the NNT2
Hebrews 13 in the NNT3
Hebrews 13 in the PDDPT
Hebrews 13 in the PFNT
Hebrews 13 in the RMNT
Hebrews 13 in the SBIAS
Hebrews 13 in the SBIBS
Hebrews 13 in the SBIBS2
Hebrews 13 in the SBICS
Hebrews 13 in the SBIDS
Hebrews 13 in the SBIGS
Hebrews 13 in the SBIHS
Hebrews 13 in the SBIIS
Hebrews 13 in the SBIIS2
Hebrews 13 in the SBIIS3
Hebrews 13 in the SBIKS
Hebrews 13 in the SBIKS2
Hebrews 13 in the SBIMS
Hebrews 13 in the SBIOS
Hebrews 13 in the SBIPS
Hebrews 13 in the SBISS
Hebrews 13 in the SBITS
Hebrews 13 in the SBITS2
Hebrews 13 in the SBITS3
Hebrews 13 in the SBITS4
Hebrews 13 in the SBIUS
Hebrews 13 in the SBIVS
Hebrews 13 in the SBT
Hebrews 13 in the SBT1E
Hebrews 13 in the SCHL
Hebrews 13 in the SNT
Hebrews 13 in the SUSU
Hebrews 13 in the SUSU2
Hebrews 13 in the SYNO
Hebrews 13 in the TBIAOTANT
Hebrews 13 in the TBT1E
Hebrews 13 in the TBT1E2
Hebrews 13 in the TFTIP
Hebrews 13 in the TFTU
Hebrews 13 in the TGNTATF3T
Hebrews 13 in the THAI
Hebrews 13 in the TNFD
Hebrews 13 in the TNT
Hebrews 13 in the TNTIK
Hebrews 13 in the TNTIL
Hebrews 13 in the TNTIN
Hebrews 13 in the TNTIP
Hebrews 13 in the TNTIZ
Hebrews 13 in the TOMA
Hebrews 13 in the TTENT
Hebrews 13 in the UBG
Hebrews 13 in the UGV
Hebrews 13 in the UGV2
Hebrews 13 in the UGV3
Hebrews 13 in the VBL
Hebrews 13 in the VDCC
Hebrews 13 in the YALU
Hebrews 13 in the YAPE
Hebrews 13 in the YBVTP
Hebrews 13 in the ZBP