Isaiah 63 (BOKCV)
1 Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu,kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu?Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari,anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki,mwenye nguvu wa kuokoa.” 2 Kwa nini mavazi yako ni mekundu,kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu? 3 “Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.Nimewaponda kwa miguu katika hasira yanguna kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,na kutia madoa nguo zangu zote. 4 Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,mwaka wa ukombozi wangu umefika. 5 Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza. 6 Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,katika ghadhabu yangu niliwalewesha,na kumwaga damu yao juu ya ardhi.” 7 Nitasimulia juu ya wema wa BWANA,kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,sawasawa na yote ambayo BWANAametenda kwa ajili yetu:naam, mambo mengi mema aliyoyatendakwa ajili ya nyumba ya Israeli,sawasawa na huruma zakena wema wake mwingi. 8 Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,wana ambao hawatanidanganya”;hivyo akawa Mwokozi wao. 9 Katika taabu zao zote naye alitaabika,na malaika wa uso wake akawaokoa.Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa,akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita. 10 Lakini waliasi,na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.Hivyo aligeuka na kuwa adui yao,na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao. 11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita,siku za Mose na watu wake:yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari,pamoja na wachungaji wa kundi lake?Yuko wapi yule aliyewekaRoho wake Mtakatifu katikati yao, 12 aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvukuwa katika mkono wa kuume wa Mose,aliyegawa maji ya bahari mbele yao,ili kujipatia jina milele, 13 aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi?Kama farasi katika nchi iliyo wazi,wao hawakujikwaa, 14 kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho,walipewa pumziko na Roho wa BWANA.Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wakoili kujipatia mwenyewe jina tukufu. 15 Tazama chini kutoka mbinguni ukaonekutoka kiti chako cha enzikilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu.Uko wapi wivu wako na uweza wako?Umetuzuilia wema wako na huruma zako. 16 Lakini wewe ni Baba yetu,ingawa Abrahamu hatufahamu sisiwala Israeli hatutambui;wewe, Ee BWANA, ndiwe Baba yetu,Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako. 17 Ee BWANA, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako,na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu?Rudi kwa ajili ya watumishi wako,yale makabila ambayo ni urithi wako. 18 Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu,lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako. 19 Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe,kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.
In Other Versions
Isaiah 63 in the ANGEFD
Isaiah 63 in the ANTPNG2D
Isaiah 63 in the AS21
Isaiah 63 in the BAGH
Isaiah 63 in the BBPNG
Isaiah 63 in the BBT1E
Isaiah 63 in the BDS
Isaiah 63 in the BEV
Isaiah 63 in the BHAD
Isaiah 63 in the BIB
Isaiah 63 in the BLPT
Isaiah 63 in the BNT
Isaiah 63 in the BNTABOOT
Isaiah 63 in the BNTLV
Isaiah 63 in the BOATCB
Isaiah 63 in the BOATCB2
Isaiah 63 in the BOBCV
Isaiah 63 in the BOCNT
Isaiah 63 in the BOECS
Isaiah 63 in the BOGWICC
Isaiah 63 in the BOHCB
Isaiah 63 in the BOHCV
Isaiah 63 in the BOHLNT
Isaiah 63 in the BOHNTLTAL
Isaiah 63 in the BOICB
Isaiah 63 in the BOILNTAP
Isaiah 63 in the BOITCV
Isaiah 63 in the BOKCV2
Isaiah 63 in the BOKHWOG
Isaiah 63 in the BOKSSV
Isaiah 63 in the BOLCB
Isaiah 63 in the BOLCB2
Isaiah 63 in the BOMCV
Isaiah 63 in the BONAV
Isaiah 63 in the BONCB
Isaiah 63 in the BONLT
Isaiah 63 in the BONUT2
Isaiah 63 in the BOPLNT
Isaiah 63 in the BOSCB
Isaiah 63 in the BOSNC
Isaiah 63 in the BOTLNT
Isaiah 63 in the BOVCB
Isaiah 63 in the BOYCB
Isaiah 63 in the BPBB
Isaiah 63 in the BPH
Isaiah 63 in the BSB
Isaiah 63 in the CCB
Isaiah 63 in the CUV
Isaiah 63 in the CUVS
Isaiah 63 in the DBT
Isaiah 63 in the DGDNT
Isaiah 63 in the DHNT
Isaiah 63 in the DNT
Isaiah 63 in the ELBE
Isaiah 63 in the EMTV
Isaiah 63 in the ESV
Isaiah 63 in the FBV
Isaiah 63 in the FEB
Isaiah 63 in the GGMNT
Isaiah 63 in the GNT
Isaiah 63 in the HARY
Isaiah 63 in the HNT
Isaiah 63 in the IRVA
Isaiah 63 in the IRVB
Isaiah 63 in the IRVG
Isaiah 63 in the IRVH
Isaiah 63 in the IRVK
Isaiah 63 in the IRVM
Isaiah 63 in the IRVM2
Isaiah 63 in the IRVO
Isaiah 63 in the IRVP
Isaiah 63 in the IRVT
Isaiah 63 in the IRVT2
Isaiah 63 in the IRVU
Isaiah 63 in the ISVN
Isaiah 63 in the JSNT
Isaiah 63 in the KAPI
Isaiah 63 in the KBT1ETNIK
Isaiah 63 in the KBV
Isaiah 63 in the KJV
Isaiah 63 in the KNFD
Isaiah 63 in the LBA
Isaiah 63 in the LBLA
Isaiah 63 in the LNT
Isaiah 63 in the LSV
Isaiah 63 in the MAAL
Isaiah 63 in the MBV
Isaiah 63 in the MBV2
Isaiah 63 in the MHNT
Isaiah 63 in the MKNFD
Isaiah 63 in the MNG
Isaiah 63 in the MNT
Isaiah 63 in the MNT2
Isaiah 63 in the MRS1T
Isaiah 63 in the NAA
Isaiah 63 in the NASB
Isaiah 63 in the NBLA
Isaiah 63 in the NBS
Isaiah 63 in the NBVTP
Isaiah 63 in the NET2
Isaiah 63 in the NIV11
Isaiah 63 in the NNT
Isaiah 63 in the NNT2
Isaiah 63 in the NNT3
Isaiah 63 in the PDDPT
Isaiah 63 in the PFNT
Isaiah 63 in the RMNT
Isaiah 63 in the SBIAS
Isaiah 63 in the SBIBS
Isaiah 63 in the SBIBS2
Isaiah 63 in the SBICS
Isaiah 63 in the SBIDS
Isaiah 63 in the SBIGS
Isaiah 63 in the SBIHS
Isaiah 63 in the SBIIS
Isaiah 63 in the SBIIS2
Isaiah 63 in the SBIIS3
Isaiah 63 in the SBIKS
Isaiah 63 in the SBIKS2
Isaiah 63 in the SBIMS
Isaiah 63 in the SBIOS
Isaiah 63 in the SBIPS
Isaiah 63 in the SBISS
Isaiah 63 in the SBITS
Isaiah 63 in the SBITS2
Isaiah 63 in the SBITS3
Isaiah 63 in the SBITS4
Isaiah 63 in the SBIUS
Isaiah 63 in the SBIVS
Isaiah 63 in the SBT
Isaiah 63 in the SBT1E
Isaiah 63 in the SCHL
Isaiah 63 in the SNT
Isaiah 63 in the SUSU
Isaiah 63 in the SUSU2
Isaiah 63 in the SYNO
Isaiah 63 in the TBIAOTANT
Isaiah 63 in the TBT1E
Isaiah 63 in the TBT1E2
Isaiah 63 in the TFTIP
Isaiah 63 in the TFTU
Isaiah 63 in the TGNTATF3T
Isaiah 63 in the THAI
Isaiah 63 in the TNFD
Isaiah 63 in the TNT
Isaiah 63 in the TNTIK
Isaiah 63 in the TNTIL
Isaiah 63 in the TNTIN
Isaiah 63 in the TNTIP
Isaiah 63 in the TNTIZ
Isaiah 63 in the TOMA
Isaiah 63 in the TTENT
Isaiah 63 in the UBG
Isaiah 63 in the UGV
Isaiah 63 in the UGV2
Isaiah 63 in the UGV3
Isaiah 63 in the VBL
Isaiah 63 in the VDCC
Isaiah 63 in the YALU
Isaiah 63 in the YAPE
Isaiah 63 in the YBVTP
Isaiah 63 in the ZBP