Jeremiah 3 (BOKCV)

1 “Kama mtu akimpa talaka mkewe,naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine,je, huyo mume aweza kumrudia tena?Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa?Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi:je, sasa utanirudia tena?”asema BWANA. 2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe?Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi,ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani.Umeinajisi nchikwa ukahaba wako na uovu wako. 3 Kwa hiyo mvua imezuiliwa,nazo mvua za vuli hazikunyesha.Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba;unakataa kutahayari kwa aibu. 4 Je, wewe hujaniita hivi punde tu:‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu, 5 je, utakasirika siku zote?Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’Hivi ndivyo unavyozungumza,lakini unafanya maovu yote uwezayo.” 6 Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, BWANA aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko. 7 Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili. 8 Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi. 9 Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti. 10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema BWANA. 11 BWANA akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu. 12 Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini:“ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ asema BWANA,‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana,kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ asema BWANA,‘Sitashika hasira yangu milele. 13 Ungama dhambi zako tu:kwamba umemwasi BWANA Mungu wako,umetapanya wema wako kwa miungu ya kigenichini ya kila mti unaotanda,nawe hukunitii mimi,’ ”asema BWANA. 14 “Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema BWANA. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni. 15 Kisha nitawapeni wachungaji wanipendezao moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu. 16 Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la BWANA,’ ” asema BWANA. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine. 17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha BWANA, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la BWANA. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. 18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi. 19 “Mimi mwenyewe nilisema,“ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wanana kuwapa nchi nzuri,urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’Nilidhani mngeniita ‘Baba,’na msingegeuka, mkaacha kunifuata. 20 Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu pia, ee nyumba ya Israeli,”asema BWANA. 21 Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli,kwa sababu wamepotoka katika njia zaona wamemsahau BWANA Mungu wao. 22 “Rudini, enyi watu msio waaminifu,nami nitawaponya ukengeufu wenu.” “Naam, tutakuja kwako,kwa maana wewe ni BWANA Mungu wetu. 23 Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilimana milimani ni udanganyifu;hakika katika BWANA, Mungu wetu,uko wokovu wa Israeli. 24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyalamatunda ya kazi za baba zetu:makundi yao ya kondoo na ngʼombe,wana wao na binti zao. 25 Sisi na tulale chini katika aibu yetu,na fedheha yetu itufunike.Tumetenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wetu,sisi na mababa zetu;tangu ujana wetu hadi leohatukumtii BWANA Mungu wetu.”

In Other Versions

Jeremiah 3 in the ANGEFD

Jeremiah 3 in the ANTPNG2D

Jeremiah 3 in the AS21

Jeremiah 3 in the BAGH

Jeremiah 3 in the BBPNG

Jeremiah 3 in the BBT1E

Jeremiah 3 in the BDS

Jeremiah 3 in the BEV

Jeremiah 3 in the BHAD

Jeremiah 3 in the BIB

Jeremiah 3 in the BLPT

Jeremiah 3 in the BNT

Jeremiah 3 in the BNTABOOT

Jeremiah 3 in the BNTLV

Jeremiah 3 in the BOATCB

Jeremiah 3 in the BOATCB2

Jeremiah 3 in the BOBCV

Jeremiah 3 in the BOCNT

Jeremiah 3 in the BOECS

Jeremiah 3 in the BOGWICC

Jeremiah 3 in the BOHCB

Jeremiah 3 in the BOHCV

Jeremiah 3 in the BOHLNT

Jeremiah 3 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 3 in the BOICB

Jeremiah 3 in the BOILNTAP

Jeremiah 3 in the BOITCV

Jeremiah 3 in the BOKCV2

Jeremiah 3 in the BOKHWOG

Jeremiah 3 in the BOKSSV

Jeremiah 3 in the BOLCB

Jeremiah 3 in the BOLCB2

Jeremiah 3 in the BOMCV

Jeremiah 3 in the BONAV

Jeremiah 3 in the BONCB

Jeremiah 3 in the BONLT

Jeremiah 3 in the BONUT2

Jeremiah 3 in the BOPLNT

Jeremiah 3 in the BOSCB

Jeremiah 3 in the BOSNC

Jeremiah 3 in the BOTLNT

Jeremiah 3 in the BOVCB

Jeremiah 3 in the BOYCB

Jeremiah 3 in the BPBB

Jeremiah 3 in the BPH

Jeremiah 3 in the BSB

Jeremiah 3 in the CCB

Jeremiah 3 in the CUV

Jeremiah 3 in the CUVS

Jeremiah 3 in the DBT

Jeremiah 3 in the DGDNT

Jeremiah 3 in the DHNT

Jeremiah 3 in the DNT

Jeremiah 3 in the ELBE

Jeremiah 3 in the EMTV

Jeremiah 3 in the ESV

Jeremiah 3 in the FBV

Jeremiah 3 in the FEB

Jeremiah 3 in the GGMNT

Jeremiah 3 in the GNT

Jeremiah 3 in the HARY

Jeremiah 3 in the HNT

Jeremiah 3 in the IRVA

Jeremiah 3 in the IRVB

Jeremiah 3 in the IRVG

Jeremiah 3 in the IRVH

Jeremiah 3 in the IRVK

Jeremiah 3 in the IRVM

Jeremiah 3 in the IRVM2

Jeremiah 3 in the IRVO

Jeremiah 3 in the IRVP

Jeremiah 3 in the IRVT

Jeremiah 3 in the IRVT2

Jeremiah 3 in the IRVU

Jeremiah 3 in the ISVN

Jeremiah 3 in the JSNT

Jeremiah 3 in the KAPI

Jeremiah 3 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 3 in the KBV

Jeremiah 3 in the KJV

Jeremiah 3 in the KNFD

Jeremiah 3 in the LBA

Jeremiah 3 in the LBLA

Jeremiah 3 in the LNT

Jeremiah 3 in the LSV

Jeremiah 3 in the MAAL

Jeremiah 3 in the MBV

Jeremiah 3 in the MBV2

Jeremiah 3 in the MHNT

Jeremiah 3 in the MKNFD

Jeremiah 3 in the MNG

Jeremiah 3 in the MNT

Jeremiah 3 in the MNT2

Jeremiah 3 in the MRS1T

Jeremiah 3 in the NAA

Jeremiah 3 in the NASB

Jeremiah 3 in the NBLA

Jeremiah 3 in the NBS

Jeremiah 3 in the NBVTP

Jeremiah 3 in the NET2

Jeremiah 3 in the NIV11

Jeremiah 3 in the NNT

Jeremiah 3 in the NNT2

Jeremiah 3 in the NNT3

Jeremiah 3 in the PDDPT

Jeremiah 3 in the PFNT

Jeremiah 3 in the RMNT

Jeremiah 3 in the SBIAS

Jeremiah 3 in the SBIBS

Jeremiah 3 in the SBIBS2

Jeremiah 3 in the SBICS

Jeremiah 3 in the SBIDS

Jeremiah 3 in the SBIGS

Jeremiah 3 in the SBIHS

Jeremiah 3 in the SBIIS

Jeremiah 3 in the SBIIS2

Jeremiah 3 in the SBIIS3

Jeremiah 3 in the SBIKS

Jeremiah 3 in the SBIKS2

Jeremiah 3 in the SBIMS

Jeremiah 3 in the SBIOS

Jeremiah 3 in the SBIPS

Jeremiah 3 in the SBISS

Jeremiah 3 in the SBITS

Jeremiah 3 in the SBITS2

Jeremiah 3 in the SBITS3

Jeremiah 3 in the SBITS4

Jeremiah 3 in the SBIUS

Jeremiah 3 in the SBIVS

Jeremiah 3 in the SBT

Jeremiah 3 in the SBT1E

Jeremiah 3 in the SCHL

Jeremiah 3 in the SNT

Jeremiah 3 in the SUSU

Jeremiah 3 in the SUSU2

Jeremiah 3 in the SYNO

Jeremiah 3 in the TBIAOTANT

Jeremiah 3 in the TBT1E

Jeremiah 3 in the TBT1E2

Jeremiah 3 in the TFTIP

Jeremiah 3 in the TFTU

Jeremiah 3 in the TGNTATF3T

Jeremiah 3 in the THAI

Jeremiah 3 in the TNFD

Jeremiah 3 in the TNT

Jeremiah 3 in the TNTIK

Jeremiah 3 in the TNTIL

Jeremiah 3 in the TNTIN

Jeremiah 3 in the TNTIP

Jeremiah 3 in the TNTIZ

Jeremiah 3 in the TOMA

Jeremiah 3 in the TTENT

Jeremiah 3 in the UBG

Jeremiah 3 in the UGV

Jeremiah 3 in the UGV2

Jeremiah 3 in the UGV3

Jeremiah 3 in the VBL

Jeremiah 3 in the VDCC

Jeremiah 3 in the YALU

Jeremiah 3 in the YAPE

Jeremiah 3 in the YBVTP

Jeremiah 3 in the ZBP