Jeremiah 31 (BOKCV)

1 “Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asema BWANA. 2 Hili ndilo asemalo BWANA:“Watu watakaopona upangawatapata upendeleo jangwani;nitakuja niwape Israeli pumziko.” 3 BWANA alitutokea wakati uliopita, akisema:“Nimekupenda kwa upendo wa milele,nimekuvuta kwa wema. 4 Nitakujenga tena nawe utajengeka upya,ewe Bikira Israeli.Utachukua tena matari yakona kwenda kucheza na wenye furaha. 5 Utapanda tena shamba la mizabibujuu ya vilima vya Samaria,wakulima watapandana kufurahia matunda yake. 6 Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelelejuu ya vilima vya Efraimu wakisema,‘Njooni, twendeni juu Sayuni,kwake BWANA Mungu wetu.’ ” 7 Hili ndilo asemalo BWANA:“Mwimbieni Yakobo kwa furaha,mpigieni kelele aliye mkuu wa mataifa.Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme,‘Ee BWANA, okoa watu wako,mabaki ya Israeli.’ 8 Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazinina kuwakusanya kutoka miisho ya dunia.Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete,mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa.Umati mkubwa wa watu utarudi. 9 Watakuja wakilia;wataomba wakati ninawarudisha.Nitawaongoza kando ya vijito vya majikatika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa,kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli,naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza. 10 “Sikieni neno la BWANA, enyi mataifa,litangazeni katika nchi za pwani ya mbali:‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanyana atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’ 11 Kwa kuwa BWANA atamlipia fidia Yakobona kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao. 12 Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni;watashangilia ukarimu wa BWANA:nafaka, divai mpya na mafuta,wana-kondoo wachangana ndama wa makundi ya ngʼombe nitakaowapa.Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri,wala hawatahuzunika tena. 13 Kisha wanawali watacheza na kufurahi,vijana waume na wazee pia.Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha,nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni. 14 Nitawashibisha makuhani kwa wingi,nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,”asema BWANA. 15 Hili ndilo asemalo BWANA:“Sauti imesikika huko Rama,maombolezo na kilio kikubwa,Raheli akiwalilia watoto wakena anakataa kufarijiwa,kwa sababu watoto wake hawako tena.” 16 Hili ndilo asemalo BWANA:“Izuie sauti yako kulia,na macho yako yasitoe machozi,kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,”asema BWANA.“Watarudi kutoka nchi ya adui. 17 Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,”asema BWANA.“Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe. 18 “Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:‘Ulinirudi kama ndama mkaidi,nami nimekubali kutii.Unirudishe, nami nitarudi,kwa sababu wewe ndiwe BWANA, Mungu wangu. 19 Baada ya kupotea, nilitubu;baada ya kuelewa, nilijipiga kifua.Niliaibika na kuona hayakwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’ 20 Je, Efraimu si mwanangu mpendwa,mtoto ninayependezwa naye?Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake,bado ninamkumbuka.Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku,nina huruma kubwa kwa ajili yake,”asema BWANA. 21 “Weka alama za barabara,weka vibao vya kuelekeza.Zingatia vyema njia kuu,barabara ile unayoipita.Rudi, ee Bikira Israeli,rudi kwenye miji yako. 22 Utatangatanga hata lini,ee binti usiye mwaminifu? BWANA ameumba kitu kipya duniani:mwanamke atamlinda mwanaume.” 23 Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘BWANA akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ 24 Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao. 25 Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.” 26 Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu. 27 BWANA asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 28 Kama vile nilivyowaangalia ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema BWANA. 29 “Katika siku hizo, watu hawatasema tena,“ ‘Baba wamekula zabibu chachu,nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’ 30 Badala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi. 31 “Siku zinakuja,” asema BWANA,“nitakapofanya agano jipyana nyumba ya Israelina nyumba ya Yuda. 32 Halitafanana na aganonililofanya na baba zaowakati nilipowashika mkonokuwaongoza watoke Misri,kwa sababu walivunja agano langu,ijapokuwa nilikuwa mume kwao,”asema BWANA. 33 “Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israelibaada ya siku zile,” asema BWANA.“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,na kuiandika mioyoni mwao.Nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu. 34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake,wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue BWANA Mungu,’kwa sababu wote watanijua mimi,tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”asema BWANA.“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,wala sitazikumbuka dhambi zao tena.” 35 Hili ndilo asemalo BWANA,yeye aliyeweka jualiwake mchana,yeye anayeamuru mwezi na nyotakungʼaa usiku,yeye aichafuaye bahariili mawimbi yake yangurume; BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: 36 “Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,”asema BWANA,“ndipo wazao wa Israeli watakomakuwa taifa mbele yangu daima.” 37 Hili ndilo asemalo BWANA:“Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimikana misingi ya dunia chiniikaweza kuchunguzwa,ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israelikwa sababu ya yote waliyoyatenda,”asema BWANA. 38 “Siku zinakuja,” asema BWANA, “wakati mji huu utajengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni. 39 Kamba ya kupimia itaanzia hapo kuendelea hadi kwenye kilima cha Garebu, na kisha kugeuka kuelekea Goa. 40 Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa BWANA. Kamwe mji huu hautangʼolewa tena wala kubomolewa.”

In Other Versions

Jeremiah 31 in the ANGEFD

Jeremiah 31 in the ANTPNG2D

Jeremiah 31 in the AS21

Jeremiah 31 in the BAGH

Jeremiah 31 in the BBPNG

Jeremiah 31 in the BBT1E

Jeremiah 31 in the BDS

Jeremiah 31 in the BEV

Jeremiah 31 in the BHAD

Jeremiah 31 in the BIB

Jeremiah 31 in the BLPT

Jeremiah 31 in the BNT

Jeremiah 31 in the BNTABOOT

Jeremiah 31 in the BNTLV

Jeremiah 31 in the BOATCB

Jeremiah 31 in the BOATCB2

Jeremiah 31 in the BOBCV

Jeremiah 31 in the BOCNT

Jeremiah 31 in the BOECS

Jeremiah 31 in the BOGWICC

Jeremiah 31 in the BOHCB

Jeremiah 31 in the BOHCV

Jeremiah 31 in the BOHLNT

Jeremiah 31 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 31 in the BOICB

Jeremiah 31 in the BOILNTAP

Jeremiah 31 in the BOITCV

Jeremiah 31 in the BOKCV2

Jeremiah 31 in the BOKHWOG

Jeremiah 31 in the BOKSSV

Jeremiah 31 in the BOLCB

Jeremiah 31 in the BOLCB2

Jeremiah 31 in the BOMCV

Jeremiah 31 in the BONAV

Jeremiah 31 in the BONCB

Jeremiah 31 in the BONLT

Jeremiah 31 in the BONUT2

Jeremiah 31 in the BOPLNT

Jeremiah 31 in the BOSCB

Jeremiah 31 in the BOSNC

Jeremiah 31 in the BOTLNT

Jeremiah 31 in the BOVCB

Jeremiah 31 in the BOYCB

Jeremiah 31 in the BPBB

Jeremiah 31 in the BPH

Jeremiah 31 in the BSB

Jeremiah 31 in the CCB

Jeremiah 31 in the CUV

Jeremiah 31 in the CUVS

Jeremiah 31 in the DBT

Jeremiah 31 in the DGDNT

Jeremiah 31 in the DHNT

Jeremiah 31 in the DNT

Jeremiah 31 in the ELBE

Jeremiah 31 in the EMTV

Jeremiah 31 in the ESV

Jeremiah 31 in the FBV

Jeremiah 31 in the FEB

Jeremiah 31 in the GGMNT

Jeremiah 31 in the GNT

Jeremiah 31 in the HARY

Jeremiah 31 in the HNT

Jeremiah 31 in the IRVA

Jeremiah 31 in the IRVB

Jeremiah 31 in the IRVG

Jeremiah 31 in the IRVH

Jeremiah 31 in the IRVK

Jeremiah 31 in the IRVM

Jeremiah 31 in the IRVM2

Jeremiah 31 in the IRVO

Jeremiah 31 in the IRVP

Jeremiah 31 in the IRVT

Jeremiah 31 in the IRVT2

Jeremiah 31 in the IRVU

Jeremiah 31 in the ISVN

Jeremiah 31 in the JSNT

Jeremiah 31 in the KAPI

Jeremiah 31 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 31 in the KBV

Jeremiah 31 in the KJV

Jeremiah 31 in the KNFD

Jeremiah 31 in the LBA

Jeremiah 31 in the LBLA

Jeremiah 31 in the LNT

Jeremiah 31 in the LSV

Jeremiah 31 in the MAAL

Jeremiah 31 in the MBV

Jeremiah 31 in the MBV2

Jeremiah 31 in the MHNT

Jeremiah 31 in the MKNFD

Jeremiah 31 in the MNG

Jeremiah 31 in the MNT

Jeremiah 31 in the MNT2

Jeremiah 31 in the MRS1T

Jeremiah 31 in the NAA

Jeremiah 31 in the NASB

Jeremiah 31 in the NBLA

Jeremiah 31 in the NBS

Jeremiah 31 in the NBVTP

Jeremiah 31 in the NET2

Jeremiah 31 in the NIV11

Jeremiah 31 in the NNT

Jeremiah 31 in the NNT2

Jeremiah 31 in the NNT3

Jeremiah 31 in the PDDPT

Jeremiah 31 in the PFNT

Jeremiah 31 in the RMNT

Jeremiah 31 in the SBIAS

Jeremiah 31 in the SBIBS

Jeremiah 31 in the SBIBS2

Jeremiah 31 in the SBICS

Jeremiah 31 in the SBIDS

Jeremiah 31 in the SBIGS

Jeremiah 31 in the SBIHS

Jeremiah 31 in the SBIIS

Jeremiah 31 in the SBIIS2

Jeremiah 31 in the SBIIS3

Jeremiah 31 in the SBIKS

Jeremiah 31 in the SBIKS2

Jeremiah 31 in the SBIMS

Jeremiah 31 in the SBIOS

Jeremiah 31 in the SBIPS

Jeremiah 31 in the SBISS

Jeremiah 31 in the SBITS

Jeremiah 31 in the SBITS2

Jeremiah 31 in the SBITS3

Jeremiah 31 in the SBITS4

Jeremiah 31 in the SBIUS

Jeremiah 31 in the SBIVS

Jeremiah 31 in the SBT

Jeremiah 31 in the SBT1E

Jeremiah 31 in the SCHL

Jeremiah 31 in the SNT

Jeremiah 31 in the SUSU

Jeremiah 31 in the SUSU2

Jeremiah 31 in the SYNO

Jeremiah 31 in the TBIAOTANT

Jeremiah 31 in the TBT1E

Jeremiah 31 in the TBT1E2

Jeremiah 31 in the TFTIP

Jeremiah 31 in the TFTU

Jeremiah 31 in the TGNTATF3T

Jeremiah 31 in the THAI

Jeremiah 31 in the TNFD

Jeremiah 31 in the TNT

Jeremiah 31 in the TNTIK

Jeremiah 31 in the TNTIL

Jeremiah 31 in the TNTIN

Jeremiah 31 in the TNTIP

Jeremiah 31 in the TNTIZ

Jeremiah 31 in the TOMA

Jeremiah 31 in the TTENT

Jeremiah 31 in the UBG

Jeremiah 31 in the UGV

Jeremiah 31 in the UGV2

Jeremiah 31 in the UGV3

Jeremiah 31 in the VBL

Jeremiah 31 in the VDCC

Jeremiah 31 in the YALU

Jeremiah 31 in the YAPE

Jeremiah 31 in the YBVTP

Jeremiah 31 in the ZBP