Jeremiah 49 (BOKCV)

1 Kuhusu Waamoni: Hili ndilo asemalo BWANA:“Je, Israeli hana wana?Je, hana warithi?Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake? 2 Lakini siku zinakuja,”asema BWANA,“nitakapopiga kelele ya vitadhidi ya Raba mji wa Waamoni;utakuwa kilima cha magofu,navyo vijiji vinavyouzungukavitateketezwa kwa moto.Kisha Israeli atawafukuzawale waliomfukuza,”asema BWANA. 3 “Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!Vaeni nguo za gunia na kuomboleza,kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni,yeye pamoja na makuhani na maafisa wake. 4 Kwa nini unajivunia mabonde yako,kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana?Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema,‘Ni nani atakayenishambulia?’ 5 Nitaleta hofu kuu juu yakokutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,”asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote.“Kila mmoja wenu ataondolewa,wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi. 6 “Lakini hatimaye,nitarudisha mateka wa Waamoni,”asema BWANA. 7 Kuhusu Edomu: Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“Je, hakuna tena hekima katika Temani?Je, shauri limewapotea wenye busara?Je, hekima yao imechakaa? 8 Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,wewe uishiye Dedani,kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esauwakati nitakapomwadhibu. 9 Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,wasingebakiza zabibu chache?Kama wezi wangekujia usiku,je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji? 10 Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,nitayafunua maficho yake,ili asiweze kujificha.Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,naye hatakuwepo tena. 11 Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.Wajane wako piawanaweza kunitumaini mimi.” 12 Hili ndilo asemalo BWANA: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. 13 Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema BWANA, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.” 14 Nimesikia ujumbe kutoka kwa BWANA:Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,“Jikusanyeni ili kuushambulia!Inukeni kwa ajili ya vita!” 15 “Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,aliyedharauliwa miongoni mwa watu. 16 Vitisho vyako na kiburi cha moyo wakovimekudanganya,wewe unayeishi katika majabali ya miamba,wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,nitakushusha chini kutoka huko,”asema BWANA. 17 “Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;wote wapitao karibuwatashangaa na kuzomeakwa sababu ya majeraha yake yote. 18 Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”asema BWANA,“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo. 19 “Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordanikuja kwenye nchi ya malisho mengi,ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?Ni nani aliye kama mimi,na ni nani awezaye kunipinga?Tena ni mchungaji yupi awezayekusimama kinyume nami?” 20 Kwa hiyo, sikia kile BWANA alichokipanga dhidi ya Edomu,kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. 21 Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu. 22 Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomuitakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 23 Kuhusu Dameski:“Hamathi na Arpadi imetahayarika,kwa kuwa wamesikia habari mbaya.Wamevunjika moyo na wametaabikakama bahari iliyochafuka. 24 Dameski amedhoofika,amegeuka na kukimbia,hofu ya ghafula imemkamata sana;amepatwa na uchungu na maumivu,maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 25 Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa,mji ambao ninaupenda? 26 Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 27 “Nitatia moto kuta za Dameski;utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.” 28 Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia: Hili ndilo asemalo BWANA:“Inuka, ushambulie Kedarina kuwaangamiza watu wa mashariki. 29 Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;vibanda vyao vitatwaliwapamoja na mali zao zote na ngamia zao.Watu watawapigia kelele,‘Hofu kuu iko kila upande!’ 30 “Kimbieni haraka!Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”asema BWANA.“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;amebuni hila dhidi yenu. 31 “Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,linaloishi kwa kujiamini,”asema BWANA,“taifa lisilo na malango wala makomeo;watu wake huishi peke yao. 32 Ngamia wao watakuwa nyara,nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.Wale walio maeneo ya mbalinitawatawanya pande zote,nami nitaleta maafa juu yaokutoka kila upande,”asema BWANA. 33 “Hazori itakuwa makao ya mbweha,mahali pa ukiwa milele.Hakuna yeyote atakayeishi humo;hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” 34 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda: 35 Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo:“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,ulio tegemeo la nguvu zao. 36 Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamutoka pande nne za mbingu,nitawatawanya katika hizo pande nne,wala hapatakuwa na taifaambalo watu wa Elamu waliofukuzwahawatakwenda. 37 Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;nitaleta maafa juu yao,naam, hasira yangu kali,”asema BWANA.“Nitawafuatia kwa upangampaka nitakapowamaliza. 38 Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamuna kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”asema BWANA. 39 “Lakini nitarudisha mateka wa Elamukatika siku zijazo,”asema BWANA.

In Other Versions

Jeremiah 49 in the ANGEFD

Jeremiah 49 in the ANTPNG2D

Jeremiah 49 in the AS21

Jeremiah 49 in the BAGH

Jeremiah 49 in the BBPNG

Jeremiah 49 in the BBT1E

Jeremiah 49 in the BDS

Jeremiah 49 in the BEV

Jeremiah 49 in the BHAD

Jeremiah 49 in the BIB

Jeremiah 49 in the BLPT

Jeremiah 49 in the BNT

Jeremiah 49 in the BNTABOOT

Jeremiah 49 in the BNTLV

Jeremiah 49 in the BOATCB

Jeremiah 49 in the BOATCB2

Jeremiah 49 in the BOBCV

Jeremiah 49 in the BOCNT

Jeremiah 49 in the BOECS

Jeremiah 49 in the BOGWICC

Jeremiah 49 in the BOHCB

Jeremiah 49 in the BOHCV

Jeremiah 49 in the BOHLNT

Jeremiah 49 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 49 in the BOICB

Jeremiah 49 in the BOILNTAP

Jeremiah 49 in the BOITCV

Jeremiah 49 in the BOKCV2

Jeremiah 49 in the BOKHWOG

Jeremiah 49 in the BOKSSV

Jeremiah 49 in the BOLCB

Jeremiah 49 in the BOLCB2

Jeremiah 49 in the BOMCV

Jeremiah 49 in the BONAV

Jeremiah 49 in the BONCB

Jeremiah 49 in the BONLT

Jeremiah 49 in the BONUT2

Jeremiah 49 in the BOPLNT

Jeremiah 49 in the BOSCB

Jeremiah 49 in the BOSNC

Jeremiah 49 in the BOTLNT

Jeremiah 49 in the BOVCB

Jeremiah 49 in the BOYCB

Jeremiah 49 in the BPBB

Jeremiah 49 in the BPH

Jeremiah 49 in the BSB

Jeremiah 49 in the CCB

Jeremiah 49 in the CUV

Jeremiah 49 in the CUVS

Jeremiah 49 in the DBT

Jeremiah 49 in the DGDNT

Jeremiah 49 in the DHNT

Jeremiah 49 in the DNT

Jeremiah 49 in the ELBE

Jeremiah 49 in the EMTV

Jeremiah 49 in the ESV

Jeremiah 49 in the FBV

Jeremiah 49 in the FEB

Jeremiah 49 in the GGMNT

Jeremiah 49 in the GNT

Jeremiah 49 in the HARY

Jeremiah 49 in the HNT

Jeremiah 49 in the IRVA

Jeremiah 49 in the IRVB

Jeremiah 49 in the IRVG

Jeremiah 49 in the IRVH

Jeremiah 49 in the IRVK

Jeremiah 49 in the IRVM

Jeremiah 49 in the IRVM2

Jeremiah 49 in the IRVO

Jeremiah 49 in the IRVP

Jeremiah 49 in the IRVT

Jeremiah 49 in the IRVT2

Jeremiah 49 in the IRVU

Jeremiah 49 in the ISVN

Jeremiah 49 in the JSNT

Jeremiah 49 in the KAPI

Jeremiah 49 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 49 in the KBV

Jeremiah 49 in the KJV

Jeremiah 49 in the KNFD

Jeremiah 49 in the LBA

Jeremiah 49 in the LBLA

Jeremiah 49 in the LNT

Jeremiah 49 in the LSV

Jeremiah 49 in the MAAL

Jeremiah 49 in the MBV

Jeremiah 49 in the MBV2

Jeremiah 49 in the MHNT

Jeremiah 49 in the MKNFD

Jeremiah 49 in the MNG

Jeremiah 49 in the MNT

Jeremiah 49 in the MNT2

Jeremiah 49 in the MRS1T

Jeremiah 49 in the NAA

Jeremiah 49 in the NASB

Jeremiah 49 in the NBLA

Jeremiah 49 in the NBS

Jeremiah 49 in the NBVTP

Jeremiah 49 in the NET2

Jeremiah 49 in the NIV11

Jeremiah 49 in the NNT

Jeremiah 49 in the NNT2

Jeremiah 49 in the NNT3

Jeremiah 49 in the PDDPT

Jeremiah 49 in the PFNT

Jeremiah 49 in the RMNT

Jeremiah 49 in the SBIAS

Jeremiah 49 in the SBIBS

Jeremiah 49 in the SBIBS2

Jeremiah 49 in the SBICS

Jeremiah 49 in the SBIDS

Jeremiah 49 in the SBIGS

Jeremiah 49 in the SBIHS

Jeremiah 49 in the SBIIS

Jeremiah 49 in the SBIIS2

Jeremiah 49 in the SBIIS3

Jeremiah 49 in the SBIKS

Jeremiah 49 in the SBIKS2

Jeremiah 49 in the SBIMS

Jeremiah 49 in the SBIOS

Jeremiah 49 in the SBIPS

Jeremiah 49 in the SBISS

Jeremiah 49 in the SBITS

Jeremiah 49 in the SBITS2

Jeremiah 49 in the SBITS3

Jeremiah 49 in the SBITS4

Jeremiah 49 in the SBIUS

Jeremiah 49 in the SBIVS

Jeremiah 49 in the SBT

Jeremiah 49 in the SBT1E

Jeremiah 49 in the SCHL

Jeremiah 49 in the SNT

Jeremiah 49 in the SUSU

Jeremiah 49 in the SUSU2

Jeremiah 49 in the SYNO

Jeremiah 49 in the TBIAOTANT

Jeremiah 49 in the TBT1E

Jeremiah 49 in the TBT1E2

Jeremiah 49 in the TFTIP

Jeremiah 49 in the TFTU

Jeremiah 49 in the TGNTATF3T

Jeremiah 49 in the THAI

Jeremiah 49 in the TNFD

Jeremiah 49 in the TNT

Jeremiah 49 in the TNTIK

Jeremiah 49 in the TNTIL

Jeremiah 49 in the TNTIN

Jeremiah 49 in the TNTIP

Jeremiah 49 in the TNTIZ

Jeremiah 49 in the TOMA

Jeremiah 49 in the TTENT

Jeremiah 49 in the UBG

Jeremiah 49 in the UGV

Jeremiah 49 in the UGV2

Jeremiah 49 in the UGV3

Jeremiah 49 in the VBL

Jeremiah 49 in the VDCC

Jeremiah 49 in the YALU

Jeremiah 49 in the YAPE

Jeremiah 49 in the YBVTP

Jeremiah 49 in the ZBP