Jeremiah 51 (BOKCV)

1 Hili ndilo asemalo BWANA:“Tazama nitaamsha roho ya mwangamizidhidi ya Babeli na watu wakaao Leb-Kamai. 2 Nitawatuma wageni Babelikumpepeta na kuiharibu nchi yake;watampinga kila upandekatika siku ya maafa yake. 3 Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake,wala usimwache avae silaha zake.Usiwaonee huruma vijana wake;angamiza jeshi lake kabisa. 4 Wataanguka waliouawa katika Babeli,wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake. 5 Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwana Mungu wao, BWANA Mwenye Nguvu Zote,ingawa nchi yao imejaa uovumbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 6 “Kimbieni kutoka Babeli!Okoeni maisha yenu!Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake.Ni wakati wa kisasi cha BWANA,atamlipa kile anachostahili. 7 Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa BWANA;aliufanya ulimwengu wote ulewe.Mataifa walikunywa mvinyo wake;kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu. 8 Babeli ataanguka ghafula na kuvunjika.Mwombolezeni!Tafuteni zeri ya kutuliza maumivu yake,labda anaweza kupona. 9 “ ‘Tungemponya Babeli,lakini hawezi kuponyeka;tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe,kwa kuwa hukumu yake inafika angani,inapanda juu hadi mawinguni.’ 10 “ ‘BWANA amethibitisha haki yetu;njooni, tutangaze katika Sayunikitu ambacho BWANA Mungu wetu amefanya.’ 11 “Noeni mishale,chukueni ngao! BWANA amewaamsha wafalme wa Wamedi,kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. BWANA atalipiza kisasi,kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. 12 Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli!Imarisheni ulinzi,wekeni walinzi,andaeni waviziao! BWANA atatimiza kusudi lake,amri yake juu ya watu wa Babeli. 13 Wewe uishiye kando ya maji mengina uliye na wingi wa hazina,mwisho wako umekuja,wakati wako wa kukatiliwa mbali. 14 BWANA Mwenye Nguvu Zoteameapa kwa nafsi yake mwenyewe:‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige,nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’ 15 “Aliiumba dunia kwa uweza wake;akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yakena akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake. 16 Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma,huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua,naye huuleta upepo kutoka ghala zake. 17 “Kila mtu ni mjinga na hana maarifa;kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.Vinyago vyake ni vya udanganyifu,havina pumzi ndani yavyo. 18 Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha,hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia. 19 Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,pamoja na kabila la urithi wake: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 20 “Wewe ndiwe rungu langu la vita,silaha yangu ya vita:kwa wewe navunjavunja mataifa,kwa wewe naangamiza falme, 21 kwa wewe navunjavunjafarasi na mpanda farasi,kwa wewe navunjavunjagari la vita na mwendeshaji wake, 22 kwa wewe napondapondamwanaume na mwanamke,kwa wewe napondapondamzee na kijana,kwa wewe napondapondakijana wa kiume na mwanamwali, 23 kwa wewe nampondapondamchungaji na kundi,kwa wewe nampondapondamkulima na maksai,kwa wewe nawapondapondawatawala na maafisa. 24 “Mbele ya macho yako nitamlipiza Babeli na wote waishio Ukaldayo kwa ajili ya makosa yote waliyofanya katika Sayuni,” asema BWANA. 25 “Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu,wewe uangamizaye dunia yote,”asema BWANA.“Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako,nikuvingirishe kutoka kwenye kilele cha mwamba,na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto. 26 Hakuna jiwe litakalochukuliwa kutoka kwakokwa ajili ya kufanywa jiwe la pembeni,wala jiwe lolote kwa ajili ya msingi,kwa maana utakuwa ukiwa milele,”asema BWANA. 27 “Twekeni bendera katika nchi!Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa!Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,iteni falme hizi dhidi yake:Ararati, Mini na Ashkenazi.Wekeni jemadari dhidi yake,pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige. 28 Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,wafalme wa Wamedi,watawala wao na maafisa wao wote,pamoja na nchi zote wanazotawala. 29 Nchi inatetemeka na kugaagaa,kwa kuwa makusudi ya BWANA dhidi ya Babeli yanasimama:yaani, kuangamiza nchi ya Babeliili pasiwe na yeyote atakayeishi humo. 30 Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana,wamebaki katika ngome zao.Nguvu zao zimekwisha,wamekuwa kama wanawake.Makazi yake yameteketezwa kwa moto,makomeo ya malango yake yamevunjika. 31 Tarishi mmoja humfuata mwingine,na mjumbe humfuata mjumbe,kumtangazia mfalme wa Babelikwamba mji wake wote umetekwa, 32 Vivuko vya mito vimekamatwa,mabwawa yenye mafunjo yametiwa moto,nao askari wameingiwa na hofu kuu.” 33 Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:“Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuriawakati inapokanyagwa;wakati wa kumvuna utakuja upesi.” 34 “Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula,ametufanya tuchangayikiwe,ametufanya tuwe gudulia tupu.Kama nyoka ametumezana kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri,kisha akatutapika. 35 Jeuri iliyofanyiwa miili yetu na iwe juu ya Babeli,”ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni.“Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,”asema Yerusalemu. 36 Kwa hiyo, hili ndilo BWANA asemalo:“Tazama, nitatetea shauri lakona kulipiza kisasi kwa ajili yako;nitaikausha bahari yakena kuzikausha chemchemi zake. 37 Babeli utakuwa lundo la magofuna makao ya mbweha,kitu cha kutisha na kudharauliwa,mahali asipoishi mtu. 38 Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo,wanakoroma kama wana simba. 39 Lakini wakati wakiwa wameamshwa,nitawaandalia karamuna kuwafanya walewe,ili wapige kelele kwa kicheko,kisha walale milele na wasiamke,”asema BWANA. 40 “Nitawateremsha kama wana-kondoo waendao machinjoni,kama kondoo dume na mbuzi. 41 “Tazama jinsi Sheshaki atakamatwa,majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa.Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi ganikati ya mataifa! 42 Bahari itainuka juu ya Babeli;mawimbi yake yenye kunguruma yatamfunika. 43 Miji yake itakuwa ukiwa,kame na jangwa,nchi ambayo hakuna yeyote anayeishi ndani yake,ambayo hakuna mtu anayepita humo. 44 Nitamwadhibu Beli katika Babeli,na kumfanya atapike kile alichokimeza.Mataifa hayatamiminika tena kwake.Nao ukuta wa Babeli utaanguka. 45 “Tokeni ndani yake, enyi watu wangu!Okoeni maisha yenu!Ikimbieni hasira kali ya BWANA. 46 Msikate tamaa wala msiogope tetesizitakaposikika katika nchi;tetesi moja inasikika mwaka huu,nyingine mwaka unaofuata;tetesi juu ya jeuri katika nchi,na ya mtawala dhidi ya mtawala. 47 Kwa kuwa hakika wakati utawadianitakapoziadhibu sanamu za Babeli;nchi yake yote itatiwa aibu,na watu wake wote waliouawawataangukia ndani yake. 48 Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yakevitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli,kwa kuwa kutoka kaskaziniwaharabu watamshambulia,”asema BWANA. 49 “Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli,kama vile waliouawa duniani kotewalivyoanguka kwa sababu ya Babeli. 50 Wewe uliyepona upanga,ondoka wala usikawie!Mkumbuke BWANA ukiwa katika nchi ya mbali,na utafakari juu ya Yerusalemu.” 51 “Tumetahayari, kwa maana tumetukanwana aibu imefunika nyuso zetu,kwa sababu wageni wameingiamahali patakatifu pa nyumba ya BWANA.” 52 “Lakini siku zinakuja,” asema BWANA,“nitakapoadhibu sanamu zake,na katika nchi yake yotewaliojeruhiwa watalia kwa maumivu makali. 53 Hata kama Babeli ikifika anganina kuziimarisha ngome zake ndefu,nitatuma waharabu dhidi yake,”asema BWANA. 54 “Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli,sauti ya uharibifu mkuukutoka nchi ya Wakaldayo. 55 BWANA ataiangamiza Babeli,atanyamazisha makelele ya kishindo chake.Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu,ngurumo ya sauti zao itavuma. 56 Mharabu atakuja dhidi ya Babeli,mashujaa wake watakamatwa,nazo pinde zao zitavunjwa.Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa kisasi,yeye atalipiza kikamilifu. 57 Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe,watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao;watalala milele na hawataamka,”asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote. 58 Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo:“Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa,na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto;mataifa yanajichosha bure,taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.” 59 Huu ndio ujumbe Yeremia aliompa afisa Seraya mwana wa Neria mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake. 60 Yeremia alikuwa ameandika ndani ya kitabu kuhusu maafa yote yatakayoipata Babeli, yaani yote yaliyokuwa yameandikwa kuhusu Babeli. 61 Yeremia akamwambia Seraya, “Utakapofika Babeli, hakikisha kwamba umesoma maneno haya yote kwa sauti kubwa. 62 Kisha sema, ‘Ee BWANA, umesema utaangamiza mahali hapa ili mtu wala mnyama asiishi ndani yake, napo patakuwa ukiwa milele.’ 63 Utakapomaliza kusoma hiki kitabu, kifungie jiwe kisha ukitupe ndani ya Mto Frati. 64 Kisha sema, ‘Hivi ndivyo Babeli utakavyozama na usiinuke tena, kwa sababu ya maafa nitakayoleta juu yake. Nao watu wake wataanguka.’ ” Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.

In Other Versions

Jeremiah 51 in the ANGEFD

Jeremiah 51 in the ANTPNG2D

Jeremiah 51 in the AS21

Jeremiah 51 in the BAGH

Jeremiah 51 in the BBPNG

Jeremiah 51 in the BBT1E

Jeremiah 51 in the BDS

Jeremiah 51 in the BEV

Jeremiah 51 in the BHAD

Jeremiah 51 in the BIB

Jeremiah 51 in the BLPT

Jeremiah 51 in the BNT

Jeremiah 51 in the BNTABOOT

Jeremiah 51 in the BNTLV

Jeremiah 51 in the BOATCB

Jeremiah 51 in the BOATCB2

Jeremiah 51 in the BOBCV

Jeremiah 51 in the BOCNT

Jeremiah 51 in the BOECS

Jeremiah 51 in the BOGWICC

Jeremiah 51 in the BOHCB

Jeremiah 51 in the BOHCV

Jeremiah 51 in the BOHLNT

Jeremiah 51 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 51 in the BOICB

Jeremiah 51 in the BOILNTAP

Jeremiah 51 in the BOITCV

Jeremiah 51 in the BOKCV2

Jeremiah 51 in the BOKHWOG

Jeremiah 51 in the BOKSSV

Jeremiah 51 in the BOLCB

Jeremiah 51 in the BOLCB2

Jeremiah 51 in the BOMCV

Jeremiah 51 in the BONAV

Jeremiah 51 in the BONCB

Jeremiah 51 in the BONLT

Jeremiah 51 in the BONUT2

Jeremiah 51 in the BOPLNT

Jeremiah 51 in the BOSCB

Jeremiah 51 in the BOSNC

Jeremiah 51 in the BOTLNT

Jeremiah 51 in the BOVCB

Jeremiah 51 in the BOYCB

Jeremiah 51 in the BPBB

Jeremiah 51 in the BPH

Jeremiah 51 in the BSB

Jeremiah 51 in the CCB

Jeremiah 51 in the CUV

Jeremiah 51 in the CUVS

Jeremiah 51 in the DBT

Jeremiah 51 in the DGDNT

Jeremiah 51 in the DHNT

Jeremiah 51 in the DNT

Jeremiah 51 in the ELBE

Jeremiah 51 in the EMTV

Jeremiah 51 in the ESV

Jeremiah 51 in the FBV

Jeremiah 51 in the FEB

Jeremiah 51 in the GGMNT

Jeremiah 51 in the GNT

Jeremiah 51 in the HARY

Jeremiah 51 in the HNT

Jeremiah 51 in the IRVA

Jeremiah 51 in the IRVB

Jeremiah 51 in the IRVG

Jeremiah 51 in the IRVH

Jeremiah 51 in the IRVK

Jeremiah 51 in the IRVM

Jeremiah 51 in the IRVM2

Jeremiah 51 in the IRVO

Jeremiah 51 in the IRVP

Jeremiah 51 in the IRVT

Jeremiah 51 in the IRVT2

Jeremiah 51 in the IRVU

Jeremiah 51 in the ISVN

Jeremiah 51 in the JSNT

Jeremiah 51 in the KAPI

Jeremiah 51 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 51 in the KBV

Jeremiah 51 in the KJV

Jeremiah 51 in the KNFD

Jeremiah 51 in the LBA

Jeremiah 51 in the LBLA

Jeremiah 51 in the LNT

Jeremiah 51 in the LSV

Jeremiah 51 in the MAAL

Jeremiah 51 in the MBV

Jeremiah 51 in the MBV2

Jeremiah 51 in the MHNT

Jeremiah 51 in the MKNFD

Jeremiah 51 in the MNG

Jeremiah 51 in the MNT

Jeremiah 51 in the MNT2

Jeremiah 51 in the MRS1T

Jeremiah 51 in the NAA

Jeremiah 51 in the NASB

Jeremiah 51 in the NBLA

Jeremiah 51 in the NBS

Jeremiah 51 in the NBVTP

Jeremiah 51 in the NET2

Jeremiah 51 in the NIV11

Jeremiah 51 in the NNT

Jeremiah 51 in the NNT2

Jeremiah 51 in the NNT3

Jeremiah 51 in the PDDPT

Jeremiah 51 in the PFNT

Jeremiah 51 in the RMNT

Jeremiah 51 in the SBIAS

Jeremiah 51 in the SBIBS

Jeremiah 51 in the SBIBS2

Jeremiah 51 in the SBICS

Jeremiah 51 in the SBIDS

Jeremiah 51 in the SBIGS

Jeremiah 51 in the SBIHS

Jeremiah 51 in the SBIIS

Jeremiah 51 in the SBIIS2

Jeremiah 51 in the SBIIS3

Jeremiah 51 in the SBIKS

Jeremiah 51 in the SBIKS2

Jeremiah 51 in the SBIMS

Jeremiah 51 in the SBIOS

Jeremiah 51 in the SBIPS

Jeremiah 51 in the SBISS

Jeremiah 51 in the SBITS

Jeremiah 51 in the SBITS2

Jeremiah 51 in the SBITS3

Jeremiah 51 in the SBITS4

Jeremiah 51 in the SBIUS

Jeremiah 51 in the SBIVS

Jeremiah 51 in the SBT

Jeremiah 51 in the SBT1E

Jeremiah 51 in the SCHL

Jeremiah 51 in the SNT

Jeremiah 51 in the SUSU

Jeremiah 51 in the SUSU2

Jeremiah 51 in the SYNO

Jeremiah 51 in the TBIAOTANT

Jeremiah 51 in the TBT1E

Jeremiah 51 in the TBT1E2

Jeremiah 51 in the TFTIP

Jeremiah 51 in the TFTU

Jeremiah 51 in the TGNTATF3T

Jeremiah 51 in the THAI

Jeremiah 51 in the TNFD

Jeremiah 51 in the TNT

Jeremiah 51 in the TNTIK

Jeremiah 51 in the TNTIL

Jeremiah 51 in the TNTIN

Jeremiah 51 in the TNTIP

Jeremiah 51 in the TNTIZ

Jeremiah 51 in the TOMA

Jeremiah 51 in the TTENT

Jeremiah 51 in the UBG

Jeremiah 51 in the UGV

Jeremiah 51 in the UGV2

Jeremiah 51 in the UGV3

Jeremiah 51 in the VBL

Jeremiah 51 in the VDCC

Jeremiah 51 in the YALU

Jeremiah 51 in the YAPE

Jeremiah 51 in the YBVTP

Jeremiah 51 in the ZBP