John 17 (BOKCV)
1 Baada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: “Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. 2 Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo. 6 “Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako. 7 Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, 8 kwa kuwa maneno yale ulionipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. 9 Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. 11 Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 12 Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia. 13 “Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. 14 Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. 17 Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. 18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. 19 Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli. 20 “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao 21 ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiye uliyenituma mimi. 22 Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. 23 Mimi ndani yako na wewe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi. 24 “Baba, shauku yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25 “Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”
In Other Versions
John 17 in the ANGEFD
John 17 in the ANTPNG2D
John 17 in the AS21
John 17 in the BAGH
John 17 in the BBPNG
John 17 in the BBT1E
John 17 in the BDS
John 17 in the BEV
John 17 in the BHAD
John 17 in the BIB
John 17 in the BLPT
John 17 in the BNT
John 17 in the BNTABOOT
John 17 in the BNTLV
John 17 in the BOATCB
John 17 in the BOATCB2
John 17 in the BOBCV
John 17 in the BOCNT
John 17 in the BOECS
John 17 in the BOGWICC
John 17 in the BOHCB
John 17 in the BOHCV
John 17 in the BOHLNT
John 17 in the BOHNTLTAL
John 17 in the BOICB
John 17 in the BOILNTAP
John 17 in the BOITCV
John 17 in the BOKCV2
John 17 in the BOKHWOG
John 17 in the BOKSSV
John 17 in the BOLCB
John 17 in the BOLCB2
John 17 in the BOMCV
John 17 in the BONAV
John 17 in the BONCB
John 17 in the BONLT
John 17 in the BONUT2
John 17 in the BOPLNT
John 17 in the BOSCB
John 17 in the BOSNC
John 17 in the BOTLNT
John 17 in the BOVCB
John 17 in the BOYCB
John 17 in the BPBB
John 17 in the BPH
John 17 in the BSB
John 17 in the CCB
John 17 in the CUV
John 17 in the CUVS
John 17 in the DBT
John 17 in the DGDNT
John 17 in the DHNT
John 17 in the DNT
John 17 in the ELBE
John 17 in the EMTV
John 17 in the ESV
John 17 in the FBV
John 17 in the FEB
John 17 in the GGMNT
John 17 in the GNT
John 17 in the HARY
John 17 in the HNT
John 17 in the IRVA
John 17 in the IRVB
John 17 in the IRVG
John 17 in the IRVH
John 17 in the IRVK
John 17 in the IRVM
John 17 in the IRVM2
John 17 in the IRVO
John 17 in the IRVP
John 17 in the IRVT
John 17 in the IRVT2
John 17 in the IRVU
John 17 in the ISVN
John 17 in the JSNT
John 17 in the KAPI
John 17 in the KBT1ETNIK
John 17 in the KBV
John 17 in the KJV
John 17 in the KNFD
John 17 in the LBA
John 17 in the LBLA
John 17 in the LNT
John 17 in the LSV
John 17 in the MAAL
John 17 in the MBV
John 17 in the MBV2
John 17 in the MHNT
John 17 in the MKNFD
John 17 in the MNG
John 17 in the MNT
John 17 in the MNT2
John 17 in the MRS1T
John 17 in the NAA
John 17 in the NASB
John 17 in the NBLA
John 17 in the NBS
John 17 in the NBVTP
John 17 in the NET2
John 17 in the NIV11
John 17 in the NNT
John 17 in the NNT2
John 17 in the NNT3
John 17 in the PDDPT
John 17 in the PFNT
John 17 in the RMNT
John 17 in the SBIAS
John 17 in the SBIBS
John 17 in the SBIBS2
John 17 in the SBICS
John 17 in the SBIDS
John 17 in the SBIGS
John 17 in the SBIHS
John 17 in the SBIIS
John 17 in the SBIIS2
John 17 in the SBIIS3
John 17 in the SBIKS
John 17 in the SBIKS2
John 17 in the SBIMS
John 17 in the SBIOS
John 17 in the SBIPS
John 17 in the SBISS
John 17 in the SBITS
John 17 in the SBITS2
John 17 in the SBITS3
John 17 in the SBITS4
John 17 in the SBIUS
John 17 in the SBIVS
John 17 in the SBT
John 17 in the SBT1E
John 17 in the SCHL
John 17 in the SNT
John 17 in the SUSU
John 17 in the SUSU2
John 17 in the SYNO
John 17 in the TBIAOTANT
John 17 in the TBT1E
John 17 in the TBT1E2
John 17 in the TFTIP
John 17 in the TFTU
John 17 in the TGNTATF3T
John 17 in the THAI
John 17 in the TNFD
John 17 in the TNT
John 17 in the TNTIK
John 17 in the TNTIL
John 17 in the TNTIN
John 17 in the TNTIP
John 17 in the TNTIZ
John 17 in the TOMA
John 17 in the TTENT
John 17 in the UBG
John 17 in the UGV
John 17 in the UGV2
John 17 in the UGV3
John 17 in the VBL
John 17 in the VDCC
John 17 in the YALU
John 17 in the YAPE
John 17 in the YBVTP
John 17 in the ZBP