Lamentations 3 (BOKCV)
1 Mimi ndiye mtu aliyeona matesokwa fimbo ya ghadhabu yake. 2 Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembeegizani wala si katika nuru; 3 hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangutena na tena, mchana kutwa. 4 Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaana ameivunja mifupa yangu. 5 Amenizingira na kunizungukakwa uchungu na taabu. 6 Amenifanya niishi gizanikama wale waliokufa. 7 Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka,amenifunga kwa minyororo mizito. 8 Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada,anakataa kupokea maombi yangu. 9 Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe,amepotosha njia zangu. 10 Kama dubu aviziaye,kama simba mafichoni, 11 ameniburuta kutoka njia,akanirarua na kuniacha bila msaada. 12 Amevuta upinde wakena kunifanya mimi niwe lengokwa ajili ya mishale yake. 13 Alinichoma moyo wangu kwa mishaleiliyotoka kwenye podo lake. 14 Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa. 15 Amenijaza kwa majani machunguna kunishibisha kwa nyongo. 16 Amevunja meno yangu kwa changarawe,amenikanyagia mavumbini. 17 Amani yangu imeondolewa,nimesahau kufanikiwa ni nini. 18 Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondokana yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa BWANA.” 19 Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,uchungu na nyongo. 20 Ninayakumbuka vyema,nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu. 21 Hata hivyo najikumbusha neno hilina kwa hiyo ninalo tumaini. 22 Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii,kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. 23 Ni mpya kila asubuhi,uaminifu wako ni mkuu. 24 Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu,kwa hiyo nitamngojea.” 25 BWANA ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,kwa yule ambaye humtafuta; 26 ni vyema kungojea kwa utulivukwa ajili ya wokovu wa BWANA. 27 Ni vyema mtu kuchukua nirabado angali kijana. 28 Na akae peke yake awe kimya,kwa maana BWANA ameiweka juu yake. 29 Na azike uso wake mavumbinibado panawezekana kuwa na matumaini. 30 Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,na ajazwe na aibu. 31 Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbalina Bwana milele. 32 Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma,kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. 33 Kwa maana hapendi kuwaletea matesoau huzuni watoto wa wanadamu. 34 Kuwaponda chini ya nyayowafungwa wote katika nchi, 35 Kumnyima mtu haki zakembele za Aliye Juu Sana, 36 kumnyima mtu haki:Je, Bwana asione mambo kama haya? 37 Nani awezaye kusema nalo likatendekakama Bwana hajaamuru? 38 Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sanandiko yatokako maafa na mambo mema? 39 Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamikawakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake? 40 Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu,na tumrudie BWANA Mungu. 41 Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetukwa Mungu mbinguni, na tuseme: 42 “Tumetenda dhambi na kuasinawe hujasamehe. 43 “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia;umetuchinja bila huruma. 44 Unajifunika mwenyewe kwa wingu,ili pasiwe na ombilitakaloweza kupenya. 45 Umetufanya takataka na uchafumiongoni mwa mataifa. 46 “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyaowazi dhidi yetu. 47 Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula,uharibifu na maangamizi.” 48 Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu,kwa sababu watu wangu wameangamizwa. 49 Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,bila kupata nafuu, 50 hadi BWANA atazame chinikutoka mbinguni na kuona. 51 Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsinikwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. 52 Wale waliokuwa adui zangu bila sababuwameniwinda kama ndege. 53 Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimona kunitupia mawe; 54 maji yalifunika juu ya kichwa changu,nami nikafikiri nilikuwa karibukukatiliwa mbali. 55 Nililiitia jina lako, Ee BWANA,kutoka vina vya shimo. 56 Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yakokilio changu nikuombapo msaada.” 57 Ulikuja karibu nilipokuita,nawe ukasema, “Usiogope.” 58 Ee Bwana, ulichukua shauri langu,ukaukomboa uhai wangu. 59 Umeona, Ee BWANA, ubaya niliotendewa.Tetea shauri langu! 60 Umeona kina cha kisasi chao,mashauri yao yote mabaya dhidi yangu. 61 Ee BWANA, umesikia matukano yao,mashauri yao yote mabaya dhidi yangu: 62 kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikiadhidi yangu mchana kutwa. 63 Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama,wananidhihaki katika nyimbo zao. 64 Uwalipe kile wanachostahili, Ee BWANA,kwa yale ambayo mikono yao imetenda. 65 Weka pazia juu ya mioyo yao,laana yako na iwe juu yao! 66 Wafuatilie katika hasira na uwaangamizekutoka chini ya mbingu za BWANA.
In Other Versions
Lamentations 3 in the ANTPNG2D
Lamentations 3 in the BNTABOOT
Lamentations 3 in the BOHNTLTAL
Lamentations 3 in the BOILNTAP
Lamentations 3 in the KBT1ETNIK
Lamentations 3 in the TBIAOTANT