1 John 4 (BOKCV)

1 Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. 2 Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. 3 Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni. 4 Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. 5 Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. 6 Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu. 7 Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 8 Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo. 9 Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. 10 Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. 11 Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 12 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13 Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake. 14 Nasi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu. 15 Kila akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 16 Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu. 18 Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo. 19 Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona? 21 Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.

In Other Versions

1 John 4 in the ANGEFD

1 John 4 in the ANTPNG2D

1 John 4 in the AS21

1 John 4 in the BAGH

1 John 4 in the BBPNG

1 John 4 in the BBT1E

1 John 4 in the BDS

1 John 4 in the BEV

1 John 4 in the BHAD

1 John 4 in the BIB

1 John 4 in the BLPT

1 John 4 in the BNT

1 John 4 in the BNTABOOT

1 John 4 in the BNTLV

1 John 4 in the BOATCB

1 John 4 in the BOATCB2

1 John 4 in the BOBCV

1 John 4 in the BOCNT

1 John 4 in the BOECS

1 John 4 in the BOGWICC

1 John 4 in the BOHCB

1 John 4 in the BOHCV

1 John 4 in the BOHLNT

1 John 4 in the BOHNTLTAL

1 John 4 in the BOICB

1 John 4 in the BOILNTAP

1 John 4 in the BOITCV

1 John 4 in the BOKCV2

1 John 4 in the BOKHWOG

1 John 4 in the BOKSSV

1 John 4 in the BOLCB

1 John 4 in the BOLCB2

1 John 4 in the BOMCV

1 John 4 in the BONAV

1 John 4 in the BONCB

1 John 4 in the BONLT

1 John 4 in the BONUT2

1 John 4 in the BOPLNT

1 John 4 in the BOSCB

1 John 4 in the BOSNC

1 John 4 in the BOTLNT

1 John 4 in the BOVCB

1 John 4 in the BOYCB

1 John 4 in the BPBB

1 John 4 in the BPH

1 John 4 in the BSB

1 John 4 in the CCB

1 John 4 in the CUV

1 John 4 in the CUVS

1 John 4 in the DBT

1 John 4 in the DGDNT

1 John 4 in the DHNT

1 John 4 in the DNT

1 John 4 in the ELBE

1 John 4 in the EMTV

1 John 4 in the ESV

1 John 4 in the FBV

1 John 4 in the FEB

1 John 4 in the GGMNT

1 John 4 in the GNT

1 John 4 in the HARY

1 John 4 in the HNT

1 John 4 in the IRVA

1 John 4 in the IRVB

1 John 4 in the IRVG

1 John 4 in the IRVH

1 John 4 in the IRVK

1 John 4 in the IRVM

1 John 4 in the IRVM2

1 John 4 in the IRVO

1 John 4 in the IRVP

1 John 4 in the IRVT

1 John 4 in the IRVT2

1 John 4 in the IRVU

1 John 4 in the ISVN

1 John 4 in the JSNT

1 John 4 in the KAPI

1 John 4 in the KBT1ETNIK

1 John 4 in the KBV

1 John 4 in the KJV

1 John 4 in the KNFD

1 John 4 in the LBA

1 John 4 in the LBLA

1 John 4 in the LNT

1 John 4 in the LSV

1 John 4 in the MAAL

1 John 4 in the MBV

1 John 4 in the MBV2

1 John 4 in the MHNT

1 John 4 in the MKNFD

1 John 4 in the MNG

1 John 4 in the MNT

1 John 4 in the MNT2

1 John 4 in the MRS1T

1 John 4 in the NAA

1 John 4 in the NASB

1 John 4 in the NBLA

1 John 4 in the NBS

1 John 4 in the NBVTP

1 John 4 in the NET2

1 John 4 in the NIV11

1 John 4 in the NNT

1 John 4 in the NNT2

1 John 4 in the NNT3

1 John 4 in the PDDPT

1 John 4 in the PFNT

1 John 4 in the RMNT

1 John 4 in the SBIAS

1 John 4 in the SBIBS

1 John 4 in the SBIBS2

1 John 4 in the SBICS

1 John 4 in the SBIDS

1 John 4 in the SBIGS

1 John 4 in the SBIHS

1 John 4 in the SBIIS

1 John 4 in the SBIIS2

1 John 4 in the SBIIS3

1 John 4 in the SBIKS

1 John 4 in the SBIKS2

1 John 4 in the SBIMS

1 John 4 in the SBIOS

1 John 4 in the SBIPS

1 John 4 in the SBISS

1 John 4 in the SBITS

1 John 4 in the SBITS2

1 John 4 in the SBITS3

1 John 4 in the SBITS4

1 John 4 in the SBIUS

1 John 4 in the SBIVS

1 John 4 in the SBT

1 John 4 in the SBT1E

1 John 4 in the SCHL

1 John 4 in the SNT

1 John 4 in the SUSU

1 John 4 in the SUSU2

1 John 4 in the SYNO

1 John 4 in the TBIAOTANT

1 John 4 in the TBT1E

1 John 4 in the TBT1E2

1 John 4 in the TFTIP

1 John 4 in the TFTU

1 John 4 in the TGNTATF3T

1 John 4 in the THAI

1 John 4 in the TNFD

1 John 4 in the TNT

1 John 4 in the TNTIK

1 John 4 in the TNTIL

1 John 4 in the TNTIN

1 John 4 in the TNTIP

1 John 4 in the TNTIZ

1 John 4 in the TOMA

1 John 4 in the TTENT

1 John 4 in the UBG

1 John 4 in the UGV

1 John 4 in the UGV2

1 John 4 in the UGV3

1 John 4 in the VBL

1 John 4 in the VDCC

1 John 4 in the YALU

1 John 4 in the YAPE

1 John 4 in the YBVTP

1 John 4 in the ZBP