Isaiah 51 (BOKCV)

1 “Nisikilizeni, ninyi mnaofuatia hakina mnaomtafuta BWANA:Tazameni mwamba ambako mlichongwa,na mahali pa kuvunjia mawe ambako mlichimbwa; 2 mwangalieni Abrahamu, baba yenu,na Sara, ambaye aliwazaa.Wakati nilipomwita alikuwa mmoja tu,nami nikambariki na kumfanya kuwa wengi. 3 Hakika BWANA ataifariji Sayuni,naye atayaangalia kwa huruma magofu yake yote;atayafanya majangwa yake yawe kama Edeni,nazo sehemu zake zisizolimika ziwe kama bustani ya BWANA.Shangwe na furaha zitakuwako ndani yake,shukrani na sauti za kuimba. 4 “Nisikilizeni, watu wangu;nisikieni, taifa langu:Sheria itatoka kwangu;haki yangu itakuwa nuru kwa mataifa. 5 Haki yangu inakaribia mbio,wokovu wangu unakuja,nao mkono wangu utaleta hukumu kwa mataifa.Visiwa vitanitegemeana kungojea mkono wangu kwa matumaini. 6 Inueni macho yenu mbinguni,mkaitazame dunia chini;mbingu zitatoweka kama moshi,dunia itachakaa kama vazi,na wakazi wake kufa kama mainzi.Bali wokovu wangu utadumu milele,haki yangu haitakoma kamwe. 7 “Nisikieni, ninyi mnaojua lililo sawa,ninyi watu ambao mna sheria yangu mioyoni mwenu:Msiogope mashutumu ya wanadamuwala msitiwe hofu na matukano yao. 8 Kwa maana nondo atawala kama vazi,nao funza atawatafuna kama sufu.Lakini haki yangu itadumu milele,wokovu wangu kwa vizazi vyote.” 9 Amka, Amka! Jivike nguvu,ewe mkono wa BWANA,Amka, kama siku zilizopita,kama vile vizazi vya zamani.Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande,uliyemchoma yule joka? 10 Si ni wewe uliyekausha bahari,maji ya kilindi kikuu,uliyefanya barabara katika vilindi vya bahariili waliokombolewa wapate kuvuka? 11 Wale waliolipiwa fidia na BWANA watarudi.Wataingia Sayuni wakiimba;furaha ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao.Furaha na shangwe zitawapata,huzuni na kulia kwa uchungu kutatoweka. 12 “Mimi, naam mimi,ndimi niwafarijie ninyi.Ninyi ni nani hata kuwaogopawanadamu wanaokufa,wanadamu ambao ni majani tu, 13 kwamba mnamsahau BWANA Muumba wenu,aliyezitanda mbinguna kuiweka misingi ya dunia,kwamba mnaishi katika hofu siku zotekwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu,ambaye nia yake ni kuangamiza?Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? 14 Wafungwa waliojikunyata kwa hofuwatawekwa huru karibuni;hawatafia kwenye gereza lao,wala hawatakosa chakula. 15 Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 16 Nimeweka maneno yangu kinywani mwakona kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu:Mimi niliyeweka mbingu mahali pake,niliyeweka misingi ya dunia,niwaambiaye Sayuni,‘Ninyi ni watu wangu.’ ” 17 Amka, amka!Simama, ee Yerusalemu,wewe uliyekunywa kutoka mkono wa BWANAkikombe cha ghadhabu yake,wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake,kikombe kile cha kunyweakiwafanyacho watu kuyumbayumba. 18 Kati ya wana wote aliowazaahakuwepo hata mmoja wa kumwongoza,kati ya wana wote aliowaleahakuwepo hata mmoja wa kumshika mkono. 19 Majanga haya mawili yamekuja juu yako:ni nani awezaye kukufariji?Maangamizi, uharibifu, njaa na upanga:ni nani awezaye kukutuliza? 20 Wana wako wamezimia,wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara,kama swala aliyenaswa kwenye wavu.Wamejazwa na ghadhabu ya BWANAna makaripio ya Mungu wako. 21 Kwa hiyo sikiliza hili, wewe uliyeteswa,uliyelewa, lakini si kwa mvinyo. 22 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi wako,Mungu wako, yeye ambaye huwatetea watu wake:“Tazama, nimeondoa mkononi mwakokikombe kilichokufanya uyumbayumbe;kutoka kikombe hicho,kikombe cha kunywa cha ghadhabu yangu,kamwe hutakunywa tena. 23 Nitakiweka mikononi mwa watesi wako,wale waliokuambia,‘Anguka kifudifudiili tuweze kutembea juu yako.’Ukaufanya mgongo wako kama ardhi,kama njia yao ya kupita.”

In Other Versions

Isaiah 51 in the ANGEFD

Isaiah 51 in the ANTPNG2D

Isaiah 51 in the AS21

Isaiah 51 in the BAGH

Isaiah 51 in the BBPNG

Isaiah 51 in the BBT1E

Isaiah 51 in the BDS

Isaiah 51 in the BEV

Isaiah 51 in the BHAD

Isaiah 51 in the BIB

Isaiah 51 in the BLPT

Isaiah 51 in the BNT

Isaiah 51 in the BNTABOOT

Isaiah 51 in the BNTLV

Isaiah 51 in the BOATCB

Isaiah 51 in the BOATCB2

Isaiah 51 in the BOBCV

Isaiah 51 in the BOCNT

Isaiah 51 in the BOECS

Isaiah 51 in the BOGWICC

Isaiah 51 in the BOHCB

Isaiah 51 in the BOHCV

Isaiah 51 in the BOHLNT

Isaiah 51 in the BOHNTLTAL

Isaiah 51 in the BOICB

Isaiah 51 in the BOILNTAP

Isaiah 51 in the BOITCV

Isaiah 51 in the BOKCV2

Isaiah 51 in the BOKHWOG

Isaiah 51 in the BOKSSV

Isaiah 51 in the BOLCB

Isaiah 51 in the BOLCB2

Isaiah 51 in the BOMCV

Isaiah 51 in the BONAV

Isaiah 51 in the BONCB

Isaiah 51 in the BONLT

Isaiah 51 in the BONUT2

Isaiah 51 in the BOPLNT

Isaiah 51 in the BOSCB

Isaiah 51 in the BOSNC

Isaiah 51 in the BOTLNT

Isaiah 51 in the BOVCB

Isaiah 51 in the BOYCB

Isaiah 51 in the BPBB

Isaiah 51 in the BPH

Isaiah 51 in the BSB

Isaiah 51 in the CCB

Isaiah 51 in the CUV

Isaiah 51 in the CUVS

Isaiah 51 in the DBT

Isaiah 51 in the DGDNT

Isaiah 51 in the DHNT

Isaiah 51 in the DNT

Isaiah 51 in the ELBE

Isaiah 51 in the EMTV

Isaiah 51 in the ESV

Isaiah 51 in the FBV

Isaiah 51 in the FEB

Isaiah 51 in the GGMNT

Isaiah 51 in the GNT

Isaiah 51 in the HARY

Isaiah 51 in the HNT

Isaiah 51 in the IRVA

Isaiah 51 in the IRVB

Isaiah 51 in the IRVG

Isaiah 51 in the IRVH

Isaiah 51 in the IRVK

Isaiah 51 in the IRVM

Isaiah 51 in the IRVM2

Isaiah 51 in the IRVO

Isaiah 51 in the IRVP

Isaiah 51 in the IRVT

Isaiah 51 in the IRVT2

Isaiah 51 in the IRVU

Isaiah 51 in the ISVN

Isaiah 51 in the JSNT

Isaiah 51 in the KAPI

Isaiah 51 in the KBT1ETNIK

Isaiah 51 in the KBV

Isaiah 51 in the KJV

Isaiah 51 in the KNFD

Isaiah 51 in the LBA

Isaiah 51 in the LBLA

Isaiah 51 in the LNT

Isaiah 51 in the LSV

Isaiah 51 in the MAAL

Isaiah 51 in the MBV

Isaiah 51 in the MBV2

Isaiah 51 in the MHNT

Isaiah 51 in the MKNFD

Isaiah 51 in the MNG

Isaiah 51 in the MNT

Isaiah 51 in the MNT2

Isaiah 51 in the MRS1T

Isaiah 51 in the NAA

Isaiah 51 in the NASB

Isaiah 51 in the NBLA

Isaiah 51 in the NBS

Isaiah 51 in the NBVTP

Isaiah 51 in the NET2

Isaiah 51 in the NIV11

Isaiah 51 in the NNT

Isaiah 51 in the NNT2

Isaiah 51 in the NNT3

Isaiah 51 in the PDDPT

Isaiah 51 in the PFNT

Isaiah 51 in the RMNT

Isaiah 51 in the SBIAS

Isaiah 51 in the SBIBS

Isaiah 51 in the SBIBS2

Isaiah 51 in the SBICS

Isaiah 51 in the SBIDS

Isaiah 51 in the SBIGS

Isaiah 51 in the SBIHS

Isaiah 51 in the SBIIS

Isaiah 51 in the SBIIS2

Isaiah 51 in the SBIIS3

Isaiah 51 in the SBIKS

Isaiah 51 in the SBIKS2

Isaiah 51 in the SBIMS

Isaiah 51 in the SBIOS

Isaiah 51 in the SBIPS

Isaiah 51 in the SBISS

Isaiah 51 in the SBITS

Isaiah 51 in the SBITS2

Isaiah 51 in the SBITS3

Isaiah 51 in the SBITS4

Isaiah 51 in the SBIUS

Isaiah 51 in the SBIVS

Isaiah 51 in the SBT

Isaiah 51 in the SBT1E

Isaiah 51 in the SCHL

Isaiah 51 in the SNT

Isaiah 51 in the SUSU

Isaiah 51 in the SUSU2

Isaiah 51 in the SYNO

Isaiah 51 in the TBIAOTANT

Isaiah 51 in the TBT1E

Isaiah 51 in the TBT1E2

Isaiah 51 in the TFTIP

Isaiah 51 in the TFTU

Isaiah 51 in the TGNTATF3T

Isaiah 51 in the THAI

Isaiah 51 in the TNFD

Isaiah 51 in the TNT

Isaiah 51 in the TNTIK

Isaiah 51 in the TNTIL

Isaiah 51 in the TNTIN

Isaiah 51 in the TNTIP

Isaiah 51 in the TNTIZ

Isaiah 51 in the TOMA

Isaiah 51 in the TTENT

Isaiah 51 in the UBG

Isaiah 51 in the UGV

Isaiah 51 in the UGV2

Isaiah 51 in the UGV3

Isaiah 51 in the VBL

Isaiah 51 in the VDCC

Isaiah 51 in the YALU

Isaiah 51 in the YAPE

Isaiah 51 in the YBVTP

Isaiah 51 in the ZBP