Job 15 (BOKCV)
1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu: 2 “Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu,au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki? 3 Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa,kwa hotuba zisizo na maana? 4 Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Munguna kuzuia ibada mbele za Mungu. 5 Dhambi yako inasukuma kinywa chako,nawe umechagua ulimi wa hila. 6 Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu;midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako. 7 “Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?Ulizaliwa kabla ya vilima? 8 Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu?Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe? 9 Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi?Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi? 10 Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu,watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako. 11 Je, faraja za Mungu hazikutoshi,au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu? 12 Kwa nini moyo wako unakudanganya,na kwa nini macho yako yanangʼaa, 13 ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu,na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako? 14 “Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi,au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu? 15 Kama Mungu hawaamini watakatifu wake,kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake, 16 sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu,ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji! 17 “Nisikilize mimi nami nitakueleza,acha nikuambie yale niliyoyaona, 18 ambayo watu wenye hekima wameyanena,bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao 19 (wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi,hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao): 20 Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso,miaka yote aliwekewa mkorofi. 21 Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake;katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia. 22 Hukata tamaa kuokoka gizani;amewekwa kwa ajili ya upanga. 23 Hutangatanga, akitafuta chakula;anajua kwamba siku ya giza iko karibu. 24 Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu;humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita, 25 kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yakena kujigamba dhidi ya Mwenyezi, 26 kwa kiburi akishambulia dhidi ya Munguakiwa na ngao nene, iliyo imara. 27 “Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unenena kiuno chake kimevimba kwa kunenepa, 28 ataishi katika miji ya magofu,na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote,nyumba zinazokuwa vifusi. 29 Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu,wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi. 30 Hatatoka gizani;mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali. 31 Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,kwa kuwa hatapata malipo yoyote. 32 Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake,nayo matawi yake hayatastawi. 33 Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva,kama mzeituni unaodondosha maua yake. 34 Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa,nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa. 35 Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu;matumbo yao huumba udanganyifu.”
In Other Versions
Job 15 in the ANGEFD
Job 15 in the ANTPNG2D
Job 15 in the AS21
Job 15 in the BAGH
Job 15 in the BBPNG
Job 15 in the BBT1E
Job 15 in the BDS
Job 15 in the BEV
Job 15 in the BHAD
Job 15 in the BIB
Job 15 in the BLPT
Job 15 in the BNT
Job 15 in the BNTABOOT
Job 15 in the BNTLV
Job 15 in the BOATCB
Job 15 in the BOATCB2
Job 15 in the BOBCV
Job 15 in the BOCNT
Job 15 in the BOECS
Job 15 in the BOGWICC
Job 15 in the BOHCB
Job 15 in the BOHCV
Job 15 in the BOHLNT
Job 15 in the BOHNTLTAL
Job 15 in the BOICB
Job 15 in the BOILNTAP
Job 15 in the BOITCV
Job 15 in the BOKCV2
Job 15 in the BOKHWOG
Job 15 in the BOKSSV
Job 15 in the BOLCB
Job 15 in the BOLCB2
Job 15 in the BOMCV
Job 15 in the BONAV
Job 15 in the BONCB
Job 15 in the BONLT
Job 15 in the BONUT2
Job 15 in the BOPLNT
Job 15 in the BOSCB
Job 15 in the BOSNC
Job 15 in the BOTLNT
Job 15 in the BOVCB
Job 15 in the BOYCB
Job 15 in the BPBB
Job 15 in the BPH
Job 15 in the BSB
Job 15 in the CCB
Job 15 in the CUV
Job 15 in the CUVS
Job 15 in the DBT
Job 15 in the DGDNT
Job 15 in the DHNT
Job 15 in the DNT
Job 15 in the ELBE
Job 15 in the EMTV
Job 15 in the ESV
Job 15 in the FBV
Job 15 in the FEB
Job 15 in the GGMNT
Job 15 in the GNT
Job 15 in the HARY
Job 15 in the HNT
Job 15 in the IRVA
Job 15 in the IRVB
Job 15 in the IRVG
Job 15 in the IRVH
Job 15 in the IRVK
Job 15 in the IRVM
Job 15 in the IRVM2
Job 15 in the IRVO
Job 15 in the IRVP
Job 15 in the IRVT
Job 15 in the IRVT2
Job 15 in the IRVU
Job 15 in the ISVN
Job 15 in the JSNT
Job 15 in the KAPI
Job 15 in the KBT1ETNIK
Job 15 in the KBV
Job 15 in the KJV
Job 15 in the KNFD
Job 15 in the LBA
Job 15 in the LBLA
Job 15 in the LNT
Job 15 in the LSV
Job 15 in the MAAL
Job 15 in the MBV
Job 15 in the MBV2
Job 15 in the MHNT
Job 15 in the MKNFD
Job 15 in the MNG
Job 15 in the MNT
Job 15 in the MNT2
Job 15 in the MRS1T
Job 15 in the NAA
Job 15 in the NASB
Job 15 in the NBLA
Job 15 in the NBS
Job 15 in the NBVTP
Job 15 in the NET2
Job 15 in the NIV11
Job 15 in the NNT
Job 15 in the NNT2
Job 15 in the NNT3
Job 15 in the PDDPT
Job 15 in the PFNT
Job 15 in the RMNT
Job 15 in the SBIAS
Job 15 in the SBIBS
Job 15 in the SBIBS2
Job 15 in the SBICS
Job 15 in the SBIDS
Job 15 in the SBIGS
Job 15 in the SBIHS
Job 15 in the SBIIS
Job 15 in the SBIIS2
Job 15 in the SBIIS3
Job 15 in the SBIKS
Job 15 in the SBIKS2
Job 15 in the SBIMS
Job 15 in the SBIOS
Job 15 in the SBIPS
Job 15 in the SBISS
Job 15 in the SBITS
Job 15 in the SBITS2
Job 15 in the SBITS3
Job 15 in the SBITS4
Job 15 in the SBIUS
Job 15 in the SBIVS
Job 15 in the SBT
Job 15 in the SBT1E
Job 15 in the SCHL
Job 15 in the SNT
Job 15 in the SUSU
Job 15 in the SUSU2
Job 15 in the SYNO
Job 15 in the TBIAOTANT
Job 15 in the TBT1E
Job 15 in the TBT1E2
Job 15 in the TFTIP
Job 15 in the TFTU
Job 15 in the TGNTATF3T
Job 15 in the THAI
Job 15 in the TNFD
Job 15 in the TNT
Job 15 in the TNTIK
Job 15 in the TNTIL
Job 15 in the TNTIN
Job 15 in the TNTIP
Job 15 in the TNTIZ
Job 15 in the TOMA
Job 15 in the TTENT
Job 15 in the UBG
Job 15 in the UGV
Job 15 in the UGV2
Job 15 in the UGV3
Job 15 in the VBL
Job 15 in the VDCC
Job 15 in the YALU
Job 15 in the YAPE
Job 15 in the YBVTP
Job 15 in the ZBP