1 Peter 1 (BOKCV)
1 Petro, mtume wa Yesu Kristo:Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. 2 Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utiifu kwa Yesu Kristo na kunyunyiziwa damu yake:Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi. 3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake kuu ametuzaa sisi mara ya pili katika tumaini lenye uzima kupitia kwa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu, 4 ili tuupate urithi usioharibika, usio na uchafu, ule usionyauka: uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu, 5 ninyi ambao mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani, hadi uje ule wokovu ulio tayari kufunuliwa nyakati za mwisho. 6 Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi. 7 Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atadhihirishwa. 8 Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. 9 Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu. 10 Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, 11 wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata. 12 Walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali waliwahudumia ninyi, waliponena kuhusu mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya. 13 Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Yesu Kristo atakapodhihirishwa. 14 Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 16 Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” 17 Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni. 18 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 19 bali kwa damu ya thamani ya Kristo, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeye alichaguliwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu. 22 Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. 23 Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. 24 Maana,“Wanadamu wote ni kama majani,nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni;majani hunyauka na maua huanguka, 25 lakini neno la Bwana ladumu milele.”Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
In Other Versions
1 Peter 1 in the ANGEFD
1 Peter 1 in the ANTPNG2D
1 Peter 1 in the AS21
1 Peter 1 in the BAGH
1 Peter 1 in the BBPNG
1 Peter 1 in the BBT1E
1 Peter 1 in the BDS
1 Peter 1 in the BEV
1 Peter 1 in the BHAD
1 Peter 1 in the BIB
1 Peter 1 in the BLPT
1 Peter 1 in the BNT
1 Peter 1 in the BNTABOOT
1 Peter 1 in the BNTLV
1 Peter 1 in the BOATCB
1 Peter 1 in the BOATCB2
1 Peter 1 in the BOBCV
1 Peter 1 in the BOCNT
1 Peter 1 in the BOECS
1 Peter 1 in the BOGWICC
1 Peter 1 in the BOHCB
1 Peter 1 in the BOHCV
1 Peter 1 in the BOHLNT
1 Peter 1 in the BOHNTLTAL
1 Peter 1 in the BOICB
1 Peter 1 in the BOILNTAP
1 Peter 1 in the BOITCV
1 Peter 1 in the BOKCV2
1 Peter 1 in the BOKHWOG
1 Peter 1 in the BOKSSV
1 Peter 1 in the BOLCB
1 Peter 1 in the BOLCB2
1 Peter 1 in the BOMCV
1 Peter 1 in the BONAV
1 Peter 1 in the BONCB
1 Peter 1 in the BONLT
1 Peter 1 in the BONUT2
1 Peter 1 in the BOPLNT
1 Peter 1 in the BOSCB
1 Peter 1 in the BOSNC
1 Peter 1 in the BOTLNT
1 Peter 1 in the BOVCB
1 Peter 1 in the BOYCB
1 Peter 1 in the BPBB
1 Peter 1 in the BPH
1 Peter 1 in the BSB
1 Peter 1 in the CCB
1 Peter 1 in the CUV
1 Peter 1 in the CUVS
1 Peter 1 in the DBT
1 Peter 1 in the DGDNT
1 Peter 1 in the DHNT
1 Peter 1 in the DNT
1 Peter 1 in the ELBE
1 Peter 1 in the EMTV
1 Peter 1 in the ESV
1 Peter 1 in the FBV
1 Peter 1 in the FEB
1 Peter 1 in the GGMNT
1 Peter 1 in the GNT
1 Peter 1 in the HARY
1 Peter 1 in the HNT
1 Peter 1 in the IRVA
1 Peter 1 in the IRVB
1 Peter 1 in the IRVG
1 Peter 1 in the IRVH
1 Peter 1 in the IRVK
1 Peter 1 in the IRVM
1 Peter 1 in the IRVM2
1 Peter 1 in the IRVO
1 Peter 1 in the IRVP
1 Peter 1 in the IRVT
1 Peter 1 in the IRVT2
1 Peter 1 in the IRVU
1 Peter 1 in the ISVN
1 Peter 1 in the JSNT
1 Peter 1 in the KAPI
1 Peter 1 in the KBT1ETNIK
1 Peter 1 in the KBV
1 Peter 1 in the KJV
1 Peter 1 in the KNFD
1 Peter 1 in the LBA
1 Peter 1 in the LBLA
1 Peter 1 in the LNT
1 Peter 1 in the LSV
1 Peter 1 in the MAAL
1 Peter 1 in the MBV
1 Peter 1 in the MBV2
1 Peter 1 in the MHNT
1 Peter 1 in the MKNFD
1 Peter 1 in the MNG
1 Peter 1 in the MNT
1 Peter 1 in the MNT2
1 Peter 1 in the MRS1T
1 Peter 1 in the NAA
1 Peter 1 in the NASB
1 Peter 1 in the NBLA
1 Peter 1 in the NBS
1 Peter 1 in the NBVTP
1 Peter 1 in the NET2
1 Peter 1 in the NIV11
1 Peter 1 in the NNT
1 Peter 1 in the NNT2
1 Peter 1 in the NNT3
1 Peter 1 in the PDDPT
1 Peter 1 in the PFNT
1 Peter 1 in the RMNT
1 Peter 1 in the SBIAS
1 Peter 1 in the SBIBS
1 Peter 1 in the SBIBS2
1 Peter 1 in the SBICS
1 Peter 1 in the SBIDS
1 Peter 1 in the SBIGS
1 Peter 1 in the SBIHS
1 Peter 1 in the SBIIS
1 Peter 1 in the SBIIS2
1 Peter 1 in the SBIIS3
1 Peter 1 in the SBIKS
1 Peter 1 in the SBIKS2
1 Peter 1 in the SBIMS
1 Peter 1 in the SBIOS
1 Peter 1 in the SBIPS
1 Peter 1 in the SBISS
1 Peter 1 in the SBITS
1 Peter 1 in the SBITS2
1 Peter 1 in the SBITS3
1 Peter 1 in the SBITS4
1 Peter 1 in the SBIUS
1 Peter 1 in the SBIVS
1 Peter 1 in the SBT
1 Peter 1 in the SBT1E
1 Peter 1 in the SCHL
1 Peter 1 in the SNT
1 Peter 1 in the SUSU
1 Peter 1 in the SUSU2
1 Peter 1 in the SYNO
1 Peter 1 in the TBIAOTANT
1 Peter 1 in the TBT1E
1 Peter 1 in the TBT1E2
1 Peter 1 in the TFTIP
1 Peter 1 in the TFTU
1 Peter 1 in the TGNTATF3T
1 Peter 1 in the THAI
1 Peter 1 in the TNFD
1 Peter 1 in the TNT
1 Peter 1 in the TNTIK
1 Peter 1 in the TNTIL
1 Peter 1 in the TNTIN
1 Peter 1 in the TNTIP
1 Peter 1 in the TNTIZ
1 Peter 1 in the TOMA
1 Peter 1 in the TTENT
1 Peter 1 in the UBG
1 Peter 1 in the UGV
1 Peter 1 in the UGV2
1 Peter 1 in the UGV3
1 Peter 1 in the VBL
1 Peter 1 in the VDCC
1 Peter 1 in the YALU
1 Peter 1 in the YAPE
1 Peter 1 in the YBVTP
1 Peter 1 in the ZBP