Isaiah 65 (BOKCV)

1 “Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’ 2 Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangukwa watu wakaidi,wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,wafuatao mawazo yao wenyewe: 3 taifa ambalo daima hunikasirishamachoni pangu,wakitoa dhabihu katika bustanina kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali; 4 watu waketio katikati ya makaburina kukesha mahali pa siri,walao nyama za nguruwe,nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi, 5 wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,ni moto uwakao mchana kutwa. 6 “Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;nitalipiza mapajani mwao: 7 dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”asema BWANA.“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milimana kunichokoza mimi juu ya vilima,nitawapimia mapajani mwaomalipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.” 8 Hili ndilo asemalo BWANA:“Kama vile divai mpya ingali bado inapatikanakatika kishada cha zabibu,nao watu husema, ‘Usikiharibu,kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;sitawaangamiza wote. 9 Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,nao watu wangu wateule watairithi,nako huko wataishi watumishi wangu. 10 Sharoni itakuwa malishokwa ajili ya makundi ya kondoo,na Bonde la Akori mahali pa kupumzikiakwa makundi ya ngʼombe,kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. 11 “Bali kwenu ninyi mnaomwacha BWANAna kuusahau mlima wangu mtakatifu,ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywakwa ajili ya Ajali, 12 nitawaagiza mfe kwa upanga,nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa;kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika,nilisema lakini hamkusikiliza.Mlitenda maovu machoni pangu,nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.” 13 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi:“Watumishi wangu watakula,lakini ninyi mtaona njaa;watumishi wangu watakunywalakini ninyi mtaona kiu;watumishi wangu watafurahi,lakini ninyi mtaona haya. 14 Watumishi wangu wataimbakwa furaha ya mioyo yao,lakini ninyi mtaliakutokana na uchungu wa moyoni,na kupiga yowe kwa sababuya uchungu wa roho zenu. 15 Mtaliacha jina lenukuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa; BWANA Mwenyezi atawaua ninyi,lakini watumishi wake atawapa jina jingine. 16 Yeye aombaye baraka katika nchiatafanya hivyo kwa Mungu wa kweli;yeye aapaye katika nchiataapa kwa Mungu wa kweli.Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulikana kufichwa kutoka machoni pangu. 17 “Tazama, nitaumbambingu mpya na dunia mpya.Mambo ya zamani hayatakumbukwa,wala hayatakuja akilini. 18 Lakini furahini na kushangilia daimakatika hivi nitakavyoumba,kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,nao watu wake wawe furaha. 19 Nami nitaifurahia Yerusalemuna kuwafurahia watu wangu;sauti ya maombolezo na ya kiliohaitasikika humo tena. 20 “Kamwe hatakuwepo tena ndani yakemtoto mchanga atakayeishi siku chache tu,au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake.Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia mojaatahesabiwa kwamba ni kijana tu,yeye ambaye hatafika miaka mia moja,atahesabiwa kuwa amelaaniwa. 21 Watajenga nyumba na kuishi ndani yake;watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. 22 Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,au kupanda mazao na wengine wale.Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,wateule wangu watafurahia kwa siku nyingikazi za mikono yao. 23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure,wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga,kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na BWANA,wao na wazao wao pamoja nao. 24 Kabla hawajaita, nitajibu,nao wakiwa katika kunena, nitasikia. 25 Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja,naye simba atakula nyasi kama maksai,lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.Hawatadhuru wala kuharibukatika mlima wangu mtakatifu wote,”asema BWANA.

In Other Versions

Isaiah 65 in the ANGEFD

Isaiah 65 in the ANTPNG2D

Isaiah 65 in the AS21

Isaiah 65 in the BAGH

Isaiah 65 in the BBPNG

Isaiah 65 in the BBT1E

Isaiah 65 in the BDS

Isaiah 65 in the BEV

Isaiah 65 in the BHAD

Isaiah 65 in the BIB

Isaiah 65 in the BLPT

Isaiah 65 in the BNT

Isaiah 65 in the BNTABOOT

Isaiah 65 in the BNTLV

Isaiah 65 in the BOATCB

Isaiah 65 in the BOATCB2

Isaiah 65 in the BOBCV

Isaiah 65 in the BOCNT

Isaiah 65 in the BOECS

Isaiah 65 in the BOGWICC

Isaiah 65 in the BOHCB

Isaiah 65 in the BOHCV

Isaiah 65 in the BOHLNT

Isaiah 65 in the BOHNTLTAL

Isaiah 65 in the BOICB

Isaiah 65 in the BOILNTAP

Isaiah 65 in the BOITCV

Isaiah 65 in the BOKCV2

Isaiah 65 in the BOKHWOG

Isaiah 65 in the BOKSSV

Isaiah 65 in the BOLCB

Isaiah 65 in the BOLCB2

Isaiah 65 in the BOMCV

Isaiah 65 in the BONAV

Isaiah 65 in the BONCB

Isaiah 65 in the BONLT

Isaiah 65 in the BONUT2

Isaiah 65 in the BOPLNT

Isaiah 65 in the BOSCB

Isaiah 65 in the BOSNC

Isaiah 65 in the BOTLNT

Isaiah 65 in the BOVCB

Isaiah 65 in the BOYCB

Isaiah 65 in the BPBB

Isaiah 65 in the BPH

Isaiah 65 in the BSB

Isaiah 65 in the CCB

Isaiah 65 in the CUV

Isaiah 65 in the CUVS

Isaiah 65 in the DBT

Isaiah 65 in the DGDNT

Isaiah 65 in the DHNT

Isaiah 65 in the DNT

Isaiah 65 in the ELBE

Isaiah 65 in the EMTV

Isaiah 65 in the ESV

Isaiah 65 in the FBV

Isaiah 65 in the FEB

Isaiah 65 in the GGMNT

Isaiah 65 in the GNT

Isaiah 65 in the HARY

Isaiah 65 in the HNT

Isaiah 65 in the IRVA

Isaiah 65 in the IRVB

Isaiah 65 in the IRVG

Isaiah 65 in the IRVH

Isaiah 65 in the IRVK

Isaiah 65 in the IRVM

Isaiah 65 in the IRVM2

Isaiah 65 in the IRVO

Isaiah 65 in the IRVP

Isaiah 65 in the IRVT

Isaiah 65 in the IRVT2

Isaiah 65 in the IRVU

Isaiah 65 in the ISVN

Isaiah 65 in the JSNT

Isaiah 65 in the KAPI

Isaiah 65 in the KBT1ETNIK

Isaiah 65 in the KBV

Isaiah 65 in the KJV

Isaiah 65 in the KNFD

Isaiah 65 in the LBA

Isaiah 65 in the LBLA

Isaiah 65 in the LNT

Isaiah 65 in the LSV

Isaiah 65 in the MAAL

Isaiah 65 in the MBV

Isaiah 65 in the MBV2

Isaiah 65 in the MHNT

Isaiah 65 in the MKNFD

Isaiah 65 in the MNG

Isaiah 65 in the MNT

Isaiah 65 in the MNT2

Isaiah 65 in the MRS1T

Isaiah 65 in the NAA

Isaiah 65 in the NASB

Isaiah 65 in the NBLA

Isaiah 65 in the NBS

Isaiah 65 in the NBVTP

Isaiah 65 in the NET2

Isaiah 65 in the NIV11

Isaiah 65 in the NNT

Isaiah 65 in the NNT2

Isaiah 65 in the NNT3

Isaiah 65 in the PDDPT

Isaiah 65 in the PFNT

Isaiah 65 in the RMNT

Isaiah 65 in the SBIAS

Isaiah 65 in the SBIBS

Isaiah 65 in the SBIBS2

Isaiah 65 in the SBICS

Isaiah 65 in the SBIDS

Isaiah 65 in the SBIGS

Isaiah 65 in the SBIHS

Isaiah 65 in the SBIIS

Isaiah 65 in the SBIIS2

Isaiah 65 in the SBIIS3

Isaiah 65 in the SBIKS

Isaiah 65 in the SBIKS2

Isaiah 65 in the SBIMS

Isaiah 65 in the SBIOS

Isaiah 65 in the SBIPS

Isaiah 65 in the SBISS

Isaiah 65 in the SBITS

Isaiah 65 in the SBITS2

Isaiah 65 in the SBITS3

Isaiah 65 in the SBITS4

Isaiah 65 in the SBIUS

Isaiah 65 in the SBIVS

Isaiah 65 in the SBT

Isaiah 65 in the SBT1E

Isaiah 65 in the SCHL

Isaiah 65 in the SNT

Isaiah 65 in the SUSU

Isaiah 65 in the SUSU2

Isaiah 65 in the SYNO

Isaiah 65 in the TBIAOTANT

Isaiah 65 in the TBT1E

Isaiah 65 in the TBT1E2

Isaiah 65 in the TFTIP

Isaiah 65 in the TFTU

Isaiah 65 in the TGNTATF3T

Isaiah 65 in the THAI

Isaiah 65 in the TNFD

Isaiah 65 in the TNT

Isaiah 65 in the TNTIK

Isaiah 65 in the TNTIL

Isaiah 65 in the TNTIN

Isaiah 65 in the TNTIP

Isaiah 65 in the TNTIZ

Isaiah 65 in the TOMA

Isaiah 65 in the TTENT

Isaiah 65 in the UBG

Isaiah 65 in the UGV

Isaiah 65 in the UGV2

Isaiah 65 in the UGV3

Isaiah 65 in the VBL

Isaiah 65 in the VDCC

Isaiah 65 in the YALU

Isaiah 65 in the YAPE

Isaiah 65 in the YBVTP

Isaiah 65 in the ZBP