Jeremiah 30 (BOKCV)
1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa BWANA: 2 “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe. 3 Siku zinakuja,’ asema BWANA, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema BWANA.” 4 Haya ndiyo maneno BWANA aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda: 5 “Hili ndilo asemalo BWANA:“ ‘Vilio vya woga vinasikika:hofu kuu, wala si amani. 6 Ulizeni na mkaone:Je, mwanaume aweza kuzaa watoto?Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvuameweka mikono yake tumbonikama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa,kila uso ukigeuka rangi kabisa? 7 Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha!Hakutakuwa na nyingine mfano wake.Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo,lakini ataokolewa kutoka hiyo. 8 “ ‘Katika siku ile,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote,‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwaona kuvipasua vifungo vyao;wageni hawatawafanya tena watumwa. 9 Badala yake, watamtumikia BWANA, Mungu waona Daudi mfalme wao,nitakayemwinua kwa ajili yao. 10 “ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,usifadhaike, ee Israeli,’asema BWANA.‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali,wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.Yakobo atakuwa tena na amani na usalama,wala hakuna atakayemtia hofu. 11 Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’asema BWANA.‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yoteambamo miongoni mwao nimewatawanya,sitawaangamiza ninyi kabisa.Nitawaadhibu, lakini kwa haki.Sitawaacha kabisa bila adhabu.’ 12 “Hili ndilo asemalo BWANA:“ ‘Kidonda chako hakina dawa,jeraha lako haliponyeki. 13 Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako,hakuna dawa ya kidonda chako,wewe hutapona. 14 Wale walioungana nawe wote wamekusahau,hawajali chochote kukuhusu wewe.Nimekupiga kama vile adui angelifanya,na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya,kwa sababu hatia yako ni kubwa mnona dhambi zako ni nyingi sana. 15 Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,yale maumivu yako yasiyoponyeka?Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyinginimekufanyia mambo haya. 16 “ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa;adui zako wote watakwenda uhamishoni.Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara;wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka. 17 Lakini nitakurudishia afya yakona kuyaponya majeraha yako,’asema BWANA,‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa,Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’ 18 “Hili ndilo asemalo BWANA:“ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo,na kuhurumia maskani yake.Mji utajengwa tena juu ya magofu yake,nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi. 19 Nyimbo za kushukuru zitatoka kwaona sauti ya furaha.Nitaiongeza idadi yaowala hawatapungua,nitawapa heshimana hawatadharauliwa. 20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwasiku za zamani,nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu;nitawaadhibu wale wote wawaoneao. 21 Mmoja wao atakuwa kiongozi wao;mtawala wao atainuka miongoni mwao.Nitamleta karibu nami,naye atanikaribia mimi,kwa maana ni nani yule atakayejitoleakuwa karibu nami?’asema BWANA. 22 ‘Kwa hiyo ninyi mtakuwa watu wangu,nami nitakuwa Mungu wenu.’ ” 23 Tazama, tufani ya BWANAitalipuka kwa ghadhabu,upepo wa kisulisuli uendao kasiutashuka juu ya vichwa vya waovu. 24 Hasira kali ya BWANA haitarudi nyumampaka atakapotimiza makusudi yote ya moyo wake.Siku zijazomtayaelewa haya.
In Other Versions
Jeremiah 30 in the ANGEFD
Jeremiah 30 in the ANTPNG2D
Jeremiah 30 in the AS21
Jeremiah 30 in the BAGH
Jeremiah 30 in the BBPNG
Jeremiah 30 in the BBT1E
Jeremiah 30 in the BDS
Jeremiah 30 in the BEV
Jeremiah 30 in the BHAD
Jeremiah 30 in the BIB
Jeremiah 30 in the BLPT
Jeremiah 30 in the BNT
Jeremiah 30 in the BNTABOOT
Jeremiah 30 in the BNTLV
Jeremiah 30 in the BOATCB
Jeremiah 30 in the BOATCB2
Jeremiah 30 in the BOBCV
Jeremiah 30 in the BOCNT
Jeremiah 30 in the BOECS
Jeremiah 30 in the BOGWICC
Jeremiah 30 in the BOHCB
Jeremiah 30 in the BOHCV
Jeremiah 30 in the BOHLNT
Jeremiah 30 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 30 in the BOICB
Jeremiah 30 in the BOILNTAP
Jeremiah 30 in the BOITCV
Jeremiah 30 in the BOKCV2
Jeremiah 30 in the BOKHWOG
Jeremiah 30 in the BOKSSV
Jeremiah 30 in the BOLCB
Jeremiah 30 in the BOLCB2
Jeremiah 30 in the BOMCV
Jeremiah 30 in the BONAV
Jeremiah 30 in the BONCB
Jeremiah 30 in the BONLT
Jeremiah 30 in the BONUT2
Jeremiah 30 in the BOPLNT
Jeremiah 30 in the BOSCB
Jeremiah 30 in the BOSNC
Jeremiah 30 in the BOTLNT
Jeremiah 30 in the BOVCB
Jeremiah 30 in the BOYCB
Jeremiah 30 in the BPBB
Jeremiah 30 in the BPH
Jeremiah 30 in the BSB
Jeremiah 30 in the CCB
Jeremiah 30 in the CUV
Jeremiah 30 in the CUVS
Jeremiah 30 in the DBT
Jeremiah 30 in the DGDNT
Jeremiah 30 in the DHNT
Jeremiah 30 in the DNT
Jeremiah 30 in the ELBE
Jeremiah 30 in the EMTV
Jeremiah 30 in the ESV
Jeremiah 30 in the FBV
Jeremiah 30 in the FEB
Jeremiah 30 in the GGMNT
Jeremiah 30 in the GNT
Jeremiah 30 in the HARY
Jeremiah 30 in the HNT
Jeremiah 30 in the IRVA
Jeremiah 30 in the IRVB
Jeremiah 30 in the IRVG
Jeremiah 30 in the IRVH
Jeremiah 30 in the IRVK
Jeremiah 30 in the IRVM
Jeremiah 30 in the IRVM2
Jeremiah 30 in the IRVO
Jeremiah 30 in the IRVP
Jeremiah 30 in the IRVT
Jeremiah 30 in the IRVT2
Jeremiah 30 in the IRVU
Jeremiah 30 in the ISVN
Jeremiah 30 in the JSNT
Jeremiah 30 in the KAPI
Jeremiah 30 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 30 in the KBV
Jeremiah 30 in the KJV
Jeremiah 30 in the KNFD
Jeremiah 30 in the LBA
Jeremiah 30 in the LBLA
Jeremiah 30 in the LNT
Jeremiah 30 in the LSV
Jeremiah 30 in the MAAL
Jeremiah 30 in the MBV
Jeremiah 30 in the MBV2
Jeremiah 30 in the MHNT
Jeremiah 30 in the MKNFD
Jeremiah 30 in the MNG
Jeremiah 30 in the MNT
Jeremiah 30 in the MNT2
Jeremiah 30 in the MRS1T
Jeremiah 30 in the NAA
Jeremiah 30 in the NASB
Jeremiah 30 in the NBLA
Jeremiah 30 in the NBS
Jeremiah 30 in the NBVTP
Jeremiah 30 in the NET2
Jeremiah 30 in the NIV11
Jeremiah 30 in the NNT
Jeremiah 30 in the NNT2
Jeremiah 30 in the NNT3
Jeremiah 30 in the PDDPT
Jeremiah 30 in the PFNT
Jeremiah 30 in the RMNT
Jeremiah 30 in the SBIAS
Jeremiah 30 in the SBIBS
Jeremiah 30 in the SBIBS2
Jeremiah 30 in the SBICS
Jeremiah 30 in the SBIDS
Jeremiah 30 in the SBIGS
Jeremiah 30 in the SBIHS
Jeremiah 30 in the SBIIS
Jeremiah 30 in the SBIIS2
Jeremiah 30 in the SBIIS3
Jeremiah 30 in the SBIKS
Jeremiah 30 in the SBIKS2
Jeremiah 30 in the SBIMS
Jeremiah 30 in the SBIOS
Jeremiah 30 in the SBIPS
Jeremiah 30 in the SBISS
Jeremiah 30 in the SBITS
Jeremiah 30 in the SBITS2
Jeremiah 30 in the SBITS3
Jeremiah 30 in the SBITS4
Jeremiah 30 in the SBIUS
Jeremiah 30 in the SBIVS
Jeremiah 30 in the SBT
Jeremiah 30 in the SBT1E
Jeremiah 30 in the SCHL
Jeremiah 30 in the SNT
Jeremiah 30 in the SUSU
Jeremiah 30 in the SUSU2
Jeremiah 30 in the SYNO
Jeremiah 30 in the TBIAOTANT
Jeremiah 30 in the TBT1E
Jeremiah 30 in the TBT1E2
Jeremiah 30 in the TFTIP
Jeremiah 30 in the TFTU
Jeremiah 30 in the TGNTATF3T
Jeremiah 30 in the THAI
Jeremiah 30 in the TNFD
Jeremiah 30 in the TNT
Jeremiah 30 in the TNTIK
Jeremiah 30 in the TNTIL
Jeremiah 30 in the TNTIN
Jeremiah 30 in the TNTIP
Jeremiah 30 in the TNTIZ
Jeremiah 30 in the TOMA
Jeremiah 30 in the TTENT
Jeremiah 30 in the UBG
Jeremiah 30 in the UGV
Jeremiah 30 in the UGV2
Jeremiah 30 in the UGV3
Jeremiah 30 in the VBL
Jeremiah 30 in the VDCC
Jeremiah 30 in the YALU
Jeremiah 30 in the YAPE
Jeremiah 30 in the YBVTP
Jeremiah 30 in the ZBP