Job 6 (BOKCV)
1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa,nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani! 3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote,kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka. 4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu,roho yangu inakunywa sumu yake;vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu. 5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani,au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula? 6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi,au upo utamu katika ute mweupe wa yai? 7 Ninakataa kuvigusa;vyakula vya aina hii hunichukiza. 8 “Laiti ningepata haja yangu,kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia, 9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda,kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali! 10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja,furaha yangu katika maumivu makali:kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu. 11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini?Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu? 12 Je, mimi nina nguvu za jiwe?Je, mwili wangu ni shaba? 13 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe,wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami? 14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi. 15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,ni kama vijito vya msimu,ni kama vijito ambavyo hufurika 16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka, 17 lakini hukauka majira ya ukame,na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake. 18 Misafara hugeuka kutoka njia zake;hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia. 19 Misafara ya Tema inatafuta maji,wafanyabiashara wa Sheba wanaosafirihutazama kwa matarajio. 20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini;wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia. 21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote;mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa. 22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu,au mnilipie fidia kutoka mali zenu, 23 au niokoeni mikononi mwa adui,au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’? 24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya;nionyesheni nilikokosea. 25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli!Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini? 26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema,na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo? 27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima,na kubadilishana rafiki yenu na mali. 28 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi.Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu? 29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu;angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu. 30 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu?Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?
In Other Versions
Job 6 in the ANGEFD
Job 6 in the ANTPNG2D
Job 6 in the AS21
Job 6 in the BAGH
Job 6 in the BBPNG
Job 6 in the BBT1E
Job 6 in the BDS
Job 6 in the BEV
Job 6 in the BHAD
Job 6 in the BIB
Job 6 in the BLPT
Job 6 in the BNT
Job 6 in the BNTABOOT
Job 6 in the BNTLV
Job 6 in the BOATCB
Job 6 in the BOATCB2
Job 6 in the BOBCV
Job 6 in the BOCNT
Job 6 in the BOECS
Job 6 in the BOGWICC
Job 6 in the BOHCB
Job 6 in the BOHCV
Job 6 in the BOHLNT
Job 6 in the BOHNTLTAL
Job 6 in the BOICB
Job 6 in the BOILNTAP
Job 6 in the BOITCV
Job 6 in the BOKCV2
Job 6 in the BOKHWOG
Job 6 in the BOKSSV
Job 6 in the BOLCB
Job 6 in the BOLCB2
Job 6 in the BOMCV
Job 6 in the BONAV
Job 6 in the BONCB
Job 6 in the BONLT
Job 6 in the BONUT2
Job 6 in the BOPLNT
Job 6 in the BOSCB
Job 6 in the BOSNC
Job 6 in the BOTLNT
Job 6 in the BOVCB
Job 6 in the BOYCB
Job 6 in the BPBB
Job 6 in the BPH
Job 6 in the BSB
Job 6 in the CCB
Job 6 in the CUV
Job 6 in the CUVS
Job 6 in the DBT
Job 6 in the DGDNT
Job 6 in the DHNT
Job 6 in the DNT
Job 6 in the ELBE
Job 6 in the EMTV
Job 6 in the ESV
Job 6 in the FBV
Job 6 in the FEB
Job 6 in the GGMNT
Job 6 in the GNT
Job 6 in the HARY
Job 6 in the HNT
Job 6 in the IRVA
Job 6 in the IRVB
Job 6 in the IRVG
Job 6 in the IRVH
Job 6 in the IRVK
Job 6 in the IRVM
Job 6 in the IRVM2
Job 6 in the IRVO
Job 6 in the IRVP
Job 6 in the IRVT
Job 6 in the IRVT2
Job 6 in the IRVU
Job 6 in the ISVN
Job 6 in the JSNT
Job 6 in the KAPI
Job 6 in the KBT1ETNIK
Job 6 in the KBV
Job 6 in the KJV
Job 6 in the KNFD
Job 6 in the LBA
Job 6 in the LBLA
Job 6 in the LNT
Job 6 in the LSV
Job 6 in the MAAL
Job 6 in the MBV
Job 6 in the MBV2
Job 6 in the MHNT
Job 6 in the MKNFD
Job 6 in the MNG
Job 6 in the MNT
Job 6 in the MNT2
Job 6 in the MRS1T
Job 6 in the NAA
Job 6 in the NASB
Job 6 in the NBLA
Job 6 in the NBS
Job 6 in the NBVTP
Job 6 in the NET2
Job 6 in the NIV11
Job 6 in the NNT
Job 6 in the NNT2
Job 6 in the NNT3
Job 6 in the PDDPT
Job 6 in the PFNT
Job 6 in the RMNT
Job 6 in the SBIAS
Job 6 in the SBIBS
Job 6 in the SBIBS2
Job 6 in the SBICS
Job 6 in the SBIDS
Job 6 in the SBIGS
Job 6 in the SBIHS
Job 6 in the SBIIS
Job 6 in the SBIIS2
Job 6 in the SBIIS3
Job 6 in the SBIKS
Job 6 in the SBIKS2
Job 6 in the SBIMS
Job 6 in the SBIOS
Job 6 in the SBIPS
Job 6 in the SBISS
Job 6 in the SBITS
Job 6 in the SBITS2
Job 6 in the SBITS3
Job 6 in the SBITS4
Job 6 in the SBIUS
Job 6 in the SBIVS
Job 6 in the SBT
Job 6 in the SBT1E
Job 6 in the SCHL
Job 6 in the SNT
Job 6 in the SUSU
Job 6 in the SUSU2
Job 6 in the SYNO
Job 6 in the TBIAOTANT
Job 6 in the TBT1E
Job 6 in the TBT1E2
Job 6 in the TFTIP
Job 6 in the TFTU
Job 6 in the TGNTATF3T
Job 6 in the THAI
Job 6 in the TNFD
Job 6 in the TNT
Job 6 in the TNTIK
Job 6 in the TNTIL
Job 6 in the TNTIN
Job 6 in the TNTIP
Job 6 in the TNTIZ
Job 6 in the TOMA
Job 6 in the TTENT
Job 6 in the UBG
Job 6 in the UGV
Job 6 in the UGV2
Job 6 in the UGV3
Job 6 in the VBL
Job 6 in the VDCC
Job 6 in the YALU
Job 6 in the YAPE
Job 6 in the YBVTP
Job 6 in the ZBP