Isaiah 66 (BOKCV)

1 Hili ndilo asemalo BWANA,“Mbingu ni kiti changu cha enzi,nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi? 2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,hivyo vikapata kuwepo?”asema BWANA. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini:yeye ambaye ni mnyenyekevuna mwenye roho yenye toba,atetemekaye asikiapo neno langu. 3 Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahalini kama yeye auaye mtu,na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,ni kama yule aabuduye sanamu.Wamejichagulia njia zao wenyewe,nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 4 Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.Walifanya maovu machoni panguna kuchagua lile linalonichukiza.” 5 Sikieni neno la BWANA,ninyi mtetemekao kwa neno lake:“Ndugu zenu wanaowachukia ninyina kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,‘BWANA na atukuzwe,ili tupate kuona furaha yenu!’Hata sasa wataaibika. 6 Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!Ni sauti ya BWANA ikiwalipa adui zakeyote wanayostahili. 7 “Kabla hajasikia utungu, alizaa;kabla hajapata maumivu,alizaa mtoto mwanaume. 8 Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?Ni nani amepata kuona mambo kama haya?Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,au taifa laweza kutokea mara?Mara Sayuni alipoona utungu,alizaa watoto wake. 9 Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwana nisizalishe?” asema BWANA.“Je, nifunge tumbo la uzaziwakati mimi ndiye nizalishaye?”asema Mungu wako. 10 “Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,ninyi nyote mnaompenda,shangilieni kwa nguvu pamoja naye,ninyi nyote mnaoomboleza juu yake. 11 Kwa kuwa mtanyonya na kutoshekakatika faraja ya matiti yake;mtakunywa sana,na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.” 12 Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA:“Nitamwongezea amani kama mto,nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwakena kubembelezwa magotini pake. 13 Kama mama anavyomfariji mtoto wake,ndivyo nitakavyokufariji wewe,nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.” 14 Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,nanyi mtastawi kama majani;mkono wa BWANA utajulikana kwa watumishi wake,bali ghadhabu yake kaliitaonyeshwa kwa adui zake. 15 Tazama, BWANA anakuja na moto,magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,na karipio lake pamoja na miali ya moto. 16 Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake BWANA atatekeleza hukumu juu ya watu wote,nao wengi watakuwa ni walewaliouawa na BWANA. 17 “Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema BWANA. 18 “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu. 19 “Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema BWANA. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la BWANA, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada. 21 Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asema BWANA. 22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema BWANA, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu. 23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema BWANA. 24 “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

In Other Versions

Isaiah 66 in the ANGEFD

Isaiah 66 in the ANTPNG2D

Isaiah 66 in the AS21

Isaiah 66 in the BAGH

Isaiah 66 in the BBPNG

Isaiah 66 in the BBT1E

Isaiah 66 in the BDS

Isaiah 66 in the BEV

Isaiah 66 in the BHAD

Isaiah 66 in the BIB

Isaiah 66 in the BLPT

Isaiah 66 in the BNT

Isaiah 66 in the BNTABOOT

Isaiah 66 in the BNTLV

Isaiah 66 in the BOATCB

Isaiah 66 in the BOATCB2

Isaiah 66 in the BOBCV

Isaiah 66 in the BOCNT

Isaiah 66 in the BOECS

Isaiah 66 in the BOGWICC

Isaiah 66 in the BOHCB

Isaiah 66 in the BOHCV

Isaiah 66 in the BOHLNT

Isaiah 66 in the BOHNTLTAL

Isaiah 66 in the BOICB

Isaiah 66 in the BOILNTAP

Isaiah 66 in the BOITCV

Isaiah 66 in the BOKCV2

Isaiah 66 in the BOKHWOG

Isaiah 66 in the BOKSSV

Isaiah 66 in the BOLCB

Isaiah 66 in the BOLCB2

Isaiah 66 in the BOMCV

Isaiah 66 in the BONAV

Isaiah 66 in the BONCB

Isaiah 66 in the BONLT

Isaiah 66 in the BONUT2

Isaiah 66 in the BOPLNT

Isaiah 66 in the BOSCB

Isaiah 66 in the BOSNC

Isaiah 66 in the BOTLNT

Isaiah 66 in the BOVCB

Isaiah 66 in the BOYCB

Isaiah 66 in the BPBB

Isaiah 66 in the BPH

Isaiah 66 in the BSB

Isaiah 66 in the CCB

Isaiah 66 in the CUV

Isaiah 66 in the CUVS

Isaiah 66 in the DBT

Isaiah 66 in the DGDNT

Isaiah 66 in the DHNT

Isaiah 66 in the DNT

Isaiah 66 in the ELBE

Isaiah 66 in the EMTV

Isaiah 66 in the ESV

Isaiah 66 in the FBV

Isaiah 66 in the FEB

Isaiah 66 in the GGMNT

Isaiah 66 in the GNT

Isaiah 66 in the HARY

Isaiah 66 in the HNT

Isaiah 66 in the IRVA

Isaiah 66 in the IRVB

Isaiah 66 in the IRVG

Isaiah 66 in the IRVH

Isaiah 66 in the IRVK

Isaiah 66 in the IRVM

Isaiah 66 in the IRVM2

Isaiah 66 in the IRVO

Isaiah 66 in the IRVP

Isaiah 66 in the IRVT

Isaiah 66 in the IRVT2

Isaiah 66 in the IRVU

Isaiah 66 in the ISVN

Isaiah 66 in the JSNT

Isaiah 66 in the KAPI

Isaiah 66 in the KBT1ETNIK

Isaiah 66 in the KBV

Isaiah 66 in the KJV

Isaiah 66 in the KNFD

Isaiah 66 in the LBA

Isaiah 66 in the LBLA

Isaiah 66 in the LNT

Isaiah 66 in the LSV

Isaiah 66 in the MAAL

Isaiah 66 in the MBV

Isaiah 66 in the MBV2

Isaiah 66 in the MHNT

Isaiah 66 in the MKNFD

Isaiah 66 in the MNG

Isaiah 66 in the MNT

Isaiah 66 in the MNT2

Isaiah 66 in the MRS1T

Isaiah 66 in the NAA

Isaiah 66 in the NASB

Isaiah 66 in the NBLA

Isaiah 66 in the NBS

Isaiah 66 in the NBVTP

Isaiah 66 in the NET2

Isaiah 66 in the NIV11

Isaiah 66 in the NNT

Isaiah 66 in the NNT2

Isaiah 66 in the NNT3

Isaiah 66 in the PDDPT

Isaiah 66 in the PFNT

Isaiah 66 in the RMNT

Isaiah 66 in the SBIAS

Isaiah 66 in the SBIBS

Isaiah 66 in the SBIBS2

Isaiah 66 in the SBICS

Isaiah 66 in the SBIDS

Isaiah 66 in the SBIGS

Isaiah 66 in the SBIHS

Isaiah 66 in the SBIIS

Isaiah 66 in the SBIIS2

Isaiah 66 in the SBIIS3

Isaiah 66 in the SBIKS

Isaiah 66 in the SBIKS2

Isaiah 66 in the SBIMS

Isaiah 66 in the SBIOS

Isaiah 66 in the SBIPS

Isaiah 66 in the SBISS

Isaiah 66 in the SBITS

Isaiah 66 in the SBITS2

Isaiah 66 in the SBITS3

Isaiah 66 in the SBITS4

Isaiah 66 in the SBIUS

Isaiah 66 in the SBIVS

Isaiah 66 in the SBT

Isaiah 66 in the SBT1E

Isaiah 66 in the SCHL

Isaiah 66 in the SNT

Isaiah 66 in the SUSU

Isaiah 66 in the SUSU2

Isaiah 66 in the SYNO

Isaiah 66 in the TBIAOTANT

Isaiah 66 in the TBT1E

Isaiah 66 in the TBT1E2

Isaiah 66 in the TFTIP

Isaiah 66 in the TFTU

Isaiah 66 in the TGNTATF3T

Isaiah 66 in the THAI

Isaiah 66 in the TNFD

Isaiah 66 in the TNT

Isaiah 66 in the TNTIK

Isaiah 66 in the TNTIL

Isaiah 66 in the TNTIN

Isaiah 66 in the TNTIP

Isaiah 66 in the TNTIZ

Isaiah 66 in the TOMA

Isaiah 66 in the TTENT

Isaiah 66 in the UBG

Isaiah 66 in the UGV

Isaiah 66 in the UGV2

Isaiah 66 in the UGV3

Isaiah 66 in the VBL

Isaiah 66 in the VDCC

Isaiah 66 in the YALU

Isaiah 66 in the YAPE

Isaiah 66 in the YBVTP

Isaiah 66 in the ZBP