Job 33 (BOKCV)

1 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu;zingatia kila kitu nitakachosema. 2 Karibu nitafungua kinywa changu;maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. 3 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu;midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. 4 Roho wa Mungu ameniumba;pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. 5 Unijibu basi, kama unaweza;jiandae kunikabili mimi. 6 Mimi ni kama wewe mbele za Mungu;mimi pia nimetolewa kwenye udongo. 7 Huna sababu ya kuniogopa,wala mkono wangu haupaswi kukulemea. 8 “Lakini umesema nikiwa ninakusikia,nami nilisikia maneno yenyewe: 9 ‘Mimi ni safi na sina dhambi;mimi ni safi na sina hatia. 10 Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu,naye ananiona kama adui yake. 11 Ananifunga miguu kwa pingu,tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’ 12 “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. 13 Kwa nini unamlalamikiakwamba yeye hamjibu mwanadamu? 14 Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja,au wakati mwingine kwa njia nyingine,ingawa mwanadamu anaweza asielewe. 15 Mungu husema na mwanadamu katika ndoto,katika maono ya usiku,wakati usingizi mzito uwaangukiapowanadamu wasinziapo vitandani mwao, 16 anaweza akasemea masikioni mwao,na kuwatia hofu kwa maonyo, 17 ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabayana kumwepusha na kiburi, 18 kuiokoa nafsi yake na shimo,uhai wake usiangamizwe kwa upanga. 19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake, 20 kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakulanayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri. 21 Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda,nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika,sasa inatokeza nje. 22 Nafsi yake inakaribia kaburi,nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo. 23 “Kama bado kuna malaika upande wakekama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu,wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake, 24 kumwonea huruma na kusema,‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni;nimepata ukombozi kwa ajili yake’: 25 ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto;hurudishwa upya kama siku za ujana wake. 26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha;Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu. 27 Ndipo huja mbele za watu na kusema,‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki,lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. 28 Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni,nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’ 29 “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu;mara mbili hata mara tatu, 30 ili aigeuze nafsi yake toka shimoni,ili nuru ya uzima imwangazie. 31 “Ayubu, zingatia, nisikilize mimi;nyamaza, nami nitanena. 32 Kama unalo lolote la kusema, unijibu;sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia. 33 Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi;nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”

In Other Versions

Job 33 in the ANGEFD

Job 33 in the ANTPNG2D

Job 33 in the AS21

Job 33 in the BAGH

Job 33 in the BBPNG

Job 33 in the BBT1E

Job 33 in the BDS

Job 33 in the BEV

Job 33 in the BHAD

Job 33 in the BIB

Job 33 in the BLPT

Job 33 in the BNT

Job 33 in the BNTABOOT

Job 33 in the BNTLV

Job 33 in the BOATCB

Job 33 in the BOATCB2

Job 33 in the BOBCV

Job 33 in the BOCNT

Job 33 in the BOECS

Job 33 in the BOGWICC

Job 33 in the BOHCB

Job 33 in the BOHCV

Job 33 in the BOHLNT

Job 33 in the BOHNTLTAL

Job 33 in the BOICB

Job 33 in the BOILNTAP

Job 33 in the BOITCV

Job 33 in the BOKCV2

Job 33 in the BOKHWOG

Job 33 in the BOKSSV

Job 33 in the BOLCB

Job 33 in the BOLCB2

Job 33 in the BOMCV

Job 33 in the BONAV

Job 33 in the BONCB

Job 33 in the BONLT

Job 33 in the BONUT2

Job 33 in the BOPLNT

Job 33 in the BOSCB

Job 33 in the BOSNC

Job 33 in the BOTLNT

Job 33 in the BOVCB

Job 33 in the BOYCB

Job 33 in the BPBB

Job 33 in the BPH

Job 33 in the BSB

Job 33 in the CCB

Job 33 in the CUV

Job 33 in the CUVS

Job 33 in the DBT

Job 33 in the DGDNT

Job 33 in the DHNT

Job 33 in the DNT

Job 33 in the ELBE

Job 33 in the EMTV

Job 33 in the ESV

Job 33 in the FBV

Job 33 in the FEB

Job 33 in the GGMNT

Job 33 in the GNT

Job 33 in the HARY

Job 33 in the HNT

Job 33 in the IRVA

Job 33 in the IRVB

Job 33 in the IRVG

Job 33 in the IRVH

Job 33 in the IRVK

Job 33 in the IRVM

Job 33 in the IRVM2

Job 33 in the IRVO

Job 33 in the IRVP

Job 33 in the IRVT

Job 33 in the IRVT2

Job 33 in the IRVU

Job 33 in the ISVN

Job 33 in the JSNT

Job 33 in the KAPI

Job 33 in the KBT1ETNIK

Job 33 in the KBV

Job 33 in the KJV

Job 33 in the KNFD

Job 33 in the LBA

Job 33 in the LBLA

Job 33 in the LNT

Job 33 in the LSV

Job 33 in the MAAL

Job 33 in the MBV

Job 33 in the MBV2

Job 33 in the MHNT

Job 33 in the MKNFD

Job 33 in the MNG

Job 33 in the MNT

Job 33 in the MNT2

Job 33 in the MRS1T

Job 33 in the NAA

Job 33 in the NASB

Job 33 in the NBLA

Job 33 in the NBS

Job 33 in the NBVTP

Job 33 in the NET2

Job 33 in the NIV11

Job 33 in the NNT

Job 33 in the NNT2

Job 33 in the NNT3

Job 33 in the PDDPT

Job 33 in the PFNT

Job 33 in the RMNT

Job 33 in the SBIAS

Job 33 in the SBIBS

Job 33 in the SBIBS2

Job 33 in the SBICS

Job 33 in the SBIDS

Job 33 in the SBIGS

Job 33 in the SBIHS

Job 33 in the SBIIS

Job 33 in the SBIIS2

Job 33 in the SBIIS3

Job 33 in the SBIKS

Job 33 in the SBIKS2

Job 33 in the SBIMS

Job 33 in the SBIOS

Job 33 in the SBIPS

Job 33 in the SBISS

Job 33 in the SBITS

Job 33 in the SBITS2

Job 33 in the SBITS3

Job 33 in the SBITS4

Job 33 in the SBIUS

Job 33 in the SBIVS

Job 33 in the SBT

Job 33 in the SBT1E

Job 33 in the SCHL

Job 33 in the SNT

Job 33 in the SUSU

Job 33 in the SUSU2

Job 33 in the SYNO

Job 33 in the TBIAOTANT

Job 33 in the TBT1E

Job 33 in the TBT1E2

Job 33 in the TFTIP

Job 33 in the TFTU

Job 33 in the TGNTATF3T

Job 33 in the THAI

Job 33 in the TNFD

Job 33 in the TNT

Job 33 in the TNTIK

Job 33 in the TNTIL

Job 33 in the TNTIN

Job 33 in the TNTIP

Job 33 in the TNTIZ

Job 33 in the TOMA

Job 33 in the TTENT

Job 33 in the UBG

Job 33 in the UGV

Job 33 in the UGV2

Job 33 in the UGV3

Job 33 in the VBL

Job 33 in the VDCC

Job 33 in the YALU

Job 33 in the YAPE

Job 33 in the YBVTP

Job 33 in the ZBP