Lamentations 1 (BOKCV)
1 Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa,mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu!Jinsi ambavyo umekuwa kama mama mjane,ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa!Yule ambaye alikuwa malkia miongoni mwa majimbosasa amekuwa mtumwa. 2 Kwa uchungu, hulia sana usiku,machozi yapo kwenye mashavu yake.Miongoni mwa wapenzi wake wotehakuna yeyote wa kumfariji.Rafiki zake wote wamemsaliti,wamekuwa adui zake. 3 Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili,Yuda amekwenda uhamishoni.Anakaa miongoni mwa mataifa,hapati mahali pa kupumzika.Wote ambao wanamsaka wamemkamatakatikati ya dhiki yake. 4 Barabara zielekeazo Sayuni zaomboleza,kwa kuwa hakuna yeyote anayekujakwenye sikukuu zake zilizoamriwa.Malango yake yote yamekuwa ukiwa,makuhani wake wanalia kwa uchungu,wanawali wake wanahuzunika,naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu. 5 Adui zake wamekuwa mabwana zake,watesi wake wana raha. BWANA amemletea huzunikwa sababu ya dhambi zake nyingi.Watoto wake wamekwenda uhamishoni,mateka mbele ya adui. 6 Fahari yote imeondokakutoka kwa Binti Sayuni.Wakuu wake wako kama ayalaambaye hapati malisho,katika udhaifu wamekimbiambele ya anayewasaka. 7 Katika siku za mateso yake na kutangatanga,Yerusalemu hukumbuka hazina zoteambazo zilikuwa zake siku za kale.Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui,hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia.Watesi wake walimtazamana kumcheka katika maangamizi yake. 8 Yerusalemu ametenda dhambi sanakwa hiyo amekuwa najisi.Wote waliomheshimu wanamdharau,kwa maana wameuona uchi wake.Yeye mwenyewe anapiga kitena kugeukia mbali. 9 Uchafu wake umegandamana na nguo zake;hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye.Anguko lake lilikuwa la kushangaza,hapakuwepo na yeyote wa kumfariji.“Tazama, Ee BWANA, teso langu,kwa maana adui ameshinda.” 10 Adui ametia mikonojuu ya hazina zake zote,aliona mataifa ya kipaganiwakiingia mahali patakatifu pake,wale uliowakataza kuingiakwenye kusanyiko lako. 11 Watu wake wote wanalia kwa uchunguwatafutapo chakula;wanabadilisha hazina zao kwa chakulaili waweze kuendelea kuishi.“Tazama, Ee BWANA, ufikiri,kwa maana nimedharauliwa.” 12 “Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando?Angalieni kote mwone.Je, kuna maumivu kama maumivu yanguyale yaliyotiwa juu yangu,yale BWANA aliyoyaleta juu yangukatika siku ya hasira yake kali? 13 “Kutoka juu alipeleka moto,akaushusha katika mifupa yangu.Aliitandia wavu miguu yanguna akanirudisha nyuma.Akanifanya mkiwa,na mdhaifu mchana kutwa. 14 “Dhambi zangu zimefungwa kwenye nira,kwa mikono yake zilifumwa pamoja.Zimefika shingoni mwanguna Bwana ameziondoa nguvu zangu.Amenitia mikononi mwa waleambao siwezi kushindana nao. 15 “Bwana amewakataa wapiganaji wa vitawote walio kati yangu,ameagiza jeshi dhidi yangukuwaponda vijana wangu wa kiume.Katika shinikizo lake la divai Bwana amemkanyagaBikira Binti Yuda. 16 “Hii ndiyo sababu ninaliana macho yangu yanafurika machozi.Hakuna yeyote aliye karibu kunifariji,hakuna yeyote wa kuhuisha roho yangu.Watoto wangu ni wakiwakwa sababu adui ameshinda.” 17 Sayuni ananyoosha mikono yake,lakini hakuna yeyote wa kumfariji. BWANA ametoa amri kwa ajili ya Yakobokwamba majirani zake wawe adui zake;Yerusalemu umekuwakitu najisi miongoni mwao. 18 “BWANA ni mwenye haki,hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake.Sikilizeni, enyi mataifa yote,tazameni maumivu yangu.Wavulana wangu na wasichana wanguwamekwenda uhamishoni. 19 “Niliita washirika wangulakini walinisaliti.Makuhani wangu na wazee wanguwaliangamia mjiniwalipokuwa wakitafuta chakulaili waweze kuishi. 20 “Angalia, Ee BWANA, jinsi nilivyo katika dhiki!Nina maumivu makali ndani yangu,nami ninahangaika moyoni mwangu,kwa kuwa nimekuwa mwasi sana.Huko nje, upanga unaua watu,ndani, kipo kifo tu. 21 “Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu,lakini hakuna yeyote wa kunifariji.Adui zangu wote wamesikia juu ya dhiki yangu,wanafurahia lile ulilolitenda.Naomba uilete siku uliyoitangazaili wawe kama mimi. 22 “Uovu wao wote na uje mbele zako;uwashughulikie waokama vile ulivyonishughulikia mimikwa sababu ya dhambi zangu zote.Kulia kwangu kwa uchungu ni kwingina moyo wangu umedhoofika.”
In Other Versions
Lamentations 1 in the ANTPNG2D
Lamentations 1 in the BNTABOOT
Lamentations 1 in the BOHNTLTAL
Lamentations 1 in the BOILNTAP
Lamentations 1 in the KBT1ETNIK
Lamentations 1 in the TBIAOTANT