Psalms 107 (BOKCV)
1 Mshukuruni BWANA, kwa kuwa yeye ni mwema,upendo wake wadumu milele. 2 Waliokombolewa wa BWANA na waseme hivi,wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, 3 wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali,kutoka mashariki na magharibi,kutoka kaskazini na kusini. 4 Baadhi yao walitangatanga jangwani,hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. 5 Walikuwa na njaa na kiu,nafsi zao zikadhoofika. 6 Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao,naye akawaokoa kutoka taabu yao. 7 Akawaongoza kwa njia iliyo sawahadi mji ambao wangeweza kuishi. 8 Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma,na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 9 kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema. 10 Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu,wafungwa wakiteseka katika minyororo, 11 kwa sababu walikuwa wameasidhidi ya maneno ya Munguna kudharau shaurila Aliye Juu Sana. 12 Aliwatumikisha kwa kazi ngumu;walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia. 13 Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao,naye akawaokoa kutoka taabu yao. 14 Akawatoa katika giza na huzuni kuuna akavunja minyororo yao. 15 Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma,na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 16 kwa kuwa yeye huvunja malango ya shabana kukata mapingo ya chuma. 17 Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao,wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. 18 Wakachukia kabisa vyakula vyote,wakakaribia malango ya mauti. 19 Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao,naye akawaokoa kutoka taabu yao. 20 Akalituma neno lake na kuwaponya,akawaokoa kutoka maangamizo yao. 21 Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma,na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 22 Na watoe dhabihu za kushukuru,na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha. 23 Wengine walisafiri baharini kwa meli,walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu. 24 Waliziona kazi za BWANA,matendo yake ya ajabu kilindini. 25 Kwa maana alisema na kuamsha tufaniiliyoinua mawimbi juu. 26 Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. 27 Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi,ujanja wao ukafikia ukomo. 28 Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao,naye akawatoa kwenye taabu yao. 29 Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono,mawimbi ya bahari yakatulia. 30 Walifurahi ilipokuwa shwari,naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. 31 Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma,na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 32 Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu,na wamsifu katika baraza la wazee. 33 Yeye aligeuza mito kuwa jangwa,chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu, 34 nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa,kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo. 35 Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji,nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo; 36 aliwaleta wenye njaa wakaishi humo,nao wakajenga mji wangeweza kuishi. 37 Walilima mashamba na kupanda mizabibu,nayo ikazaa matunda mengi, 38 Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana,wala hakuruhusu mifugo yao kupungua. 39 Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwakwa kuonewa, maafa na huzuni. 40 Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu,aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia. 41 Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao,na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo. 42 Wanyofu wataona na kufurahi,lakini waovu wote watafunga vinywa vyao. 43 Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,na atafakari upendo mkuu wa BWANA.
In Other Versions
Psalms 107 in the ANGEFD
Psalms 107 in the ANTPNG2D
Psalms 107 in the AS21
Psalms 107 in the BAGH
Psalms 107 in the BBPNG
Psalms 107 in the BBT1E
Psalms 107 in the BDS
Psalms 107 in the BEV
Psalms 107 in the BHAD
Psalms 107 in the BIB
Psalms 107 in the BLPT
Psalms 107 in the BNT
Psalms 107 in the BNTABOOT
Psalms 107 in the BNTLV
Psalms 107 in the BOATCB
Psalms 107 in the BOATCB2
Psalms 107 in the BOBCV
Psalms 107 in the BOCNT
Psalms 107 in the BOECS
Psalms 107 in the BOGWICC
Psalms 107 in the BOHCB
Psalms 107 in the BOHCV
Psalms 107 in the BOHLNT
Psalms 107 in the BOHNTLTAL
Psalms 107 in the BOICB
Psalms 107 in the BOILNTAP
Psalms 107 in the BOITCV
Psalms 107 in the BOKCV2
Psalms 107 in the BOKHWOG
Psalms 107 in the BOKSSV
Psalms 107 in the BOLCB
Psalms 107 in the BOLCB2
Psalms 107 in the BOMCV
Psalms 107 in the BONAV
Psalms 107 in the BONCB
Psalms 107 in the BONLT
Psalms 107 in the BONUT2
Psalms 107 in the BOPLNT
Psalms 107 in the BOSCB
Psalms 107 in the BOSNC
Psalms 107 in the BOTLNT
Psalms 107 in the BOVCB
Psalms 107 in the BOYCB
Psalms 107 in the BPBB
Psalms 107 in the BPH
Psalms 107 in the BSB
Psalms 107 in the CCB
Psalms 107 in the CUV
Psalms 107 in the CUVS
Psalms 107 in the DBT
Psalms 107 in the DGDNT
Psalms 107 in the DHNT
Psalms 107 in the DNT
Psalms 107 in the ELBE
Psalms 107 in the EMTV
Psalms 107 in the ESV
Psalms 107 in the FBV
Psalms 107 in the FEB
Psalms 107 in the GGMNT
Psalms 107 in the GNT
Psalms 107 in the HARY
Psalms 107 in the HNT
Psalms 107 in the IRVA
Psalms 107 in the IRVB
Psalms 107 in the IRVG
Psalms 107 in the IRVH
Psalms 107 in the IRVK
Psalms 107 in the IRVM
Psalms 107 in the IRVM2
Psalms 107 in the IRVO
Psalms 107 in the IRVP
Psalms 107 in the IRVT
Psalms 107 in the IRVT2
Psalms 107 in the IRVU
Psalms 107 in the ISVN
Psalms 107 in the JSNT
Psalms 107 in the KAPI
Psalms 107 in the KBT1ETNIK
Psalms 107 in the KBV
Psalms 107 in the KJV
Psalms 107 in the KNFD
Psalms 107 in the LBA
Psalms 107 in the LBLA
Psalms 107 in the LNT
Psalms 107 in the LSV
Psalms 107 in the MAAL
Psalms 107 in the MBV
Psalms 107 in the MBV2
Psalms 107 in the MHNT
Psalms 107 in the MKNFD
Psalms 107 in the MNG
Psalms 107 in the MNT
Psalms 107 in the MNT2
Psalms 107 in the MRS1T
Psalms 107 in the NAA
Psalms 107 in the NASB
Psalms 107 in the NBLA
Psalms 107 in the NBS
Psalms 107 in the NBVTP
Psalms 107 in the NET2
Psalms 107 in the NIV11
Psalms 107 in the NNT
Psalms 107 in the NNT2
Psalms 107 in the NNT3
Psalms 107 in the PDDPT
Psalms 107 in the PFNT
Psalms 107 in the RMNT
Psalms 107 in the SBIAS
Psalms 107 in the SBIBS
Psalms 107 in the SBIBS2
Psalms 107 in the SBICS
Psalms 107 in the SBIDS
Psalms 107 in the SBIGS
Psalms 107 in the SBIHS
Psalms 107 in the SBIIS
Psalms 107 in the SBIIS2
Psalms 107 in the SBIIS3
Psalms 107 in the SBIKS
Psalms 107 in the SBIKS2
Psalms 107 in the SBIMS
Psalms 107 in the SBIOS
Psalms 107 in the SBIPS
Psalms 107 in the SBISS
Psalms 107 in the SBITS
Psalms 107 in the SBITS2
Psalms 107 in the SBITS3
Psalms 107 in the SBITS4
Psalms 107 in the SBIUS
Psalms 107 in the SBIVS
Psalms 107 in the SBT
Psalms 107 in the SBT1E
Psalms 107 in the SCHL
Psalms 107 in the SNT
Psalms 107 in the SUSU
Psalms 107 in the SUSU2
Psalms 107 in the SYNO
Psalms 107 in the TBIAOTANT
Psalms 107 in the TBT1E
Psalms 107 in the TBT1E2
Psalms 107 in the TFTIP
Psalms 107 in the TFTU
Psalms 107 in the TGNTATF3T
Psalms 107 in the THAI
Psalms 107 in the TNFD
Psalms 107 in the TNT
Psalms 107 in the TNTIK
Psalms 107 in the TNTIL
Psalms 107 in the TNTIN
Psalms 107 in the TNTIP
Psalms 107 in the TNTIZ
Psalms 107 in the TOMA
Psalms 107 in the TTENT
Psalms 107 in the UBG
Psalms 107 in the UGV
Psalms 107 in the UGV2
Psalms 107 in the UGV3
Psalms 107 in the VBL
Psalms 107 in the VDCC
Psalms 107 in the YALU
Psalms 107 in the YAPE
Psalms 107 in the YBVTP
Psalms 107 in the ZBP