Job 31 (BOKCV)

1 “Nimefanya agano na macho yanguyasimtazame msichana kwa kumtamani. 2 Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu,urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu? 3 Je, si uharibifu kwa watu waovu,maangamizi kwa wale watendao mabaya? 4 Je, yeye hazioni njia zanguna kuihesabu kila hatua yangu? 5 “Kama nimeishi katika uongoau mguu wangu umekimbilia udanganyifu, 6 Mungu na anipime katika mizani za uaminifu,naye atajua kwamba sina hatia: 7 kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia,kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu,au kama mikono yangu imetiwa unajisi, 8 basi wengine na wale nilichokipanda,nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe. 9 “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke,au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu, 10 basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine,nao wanaume wengine walale naye. 11 Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu,naam, dhambi ya kuhukumiwa. 12 Ni moto uwakao kwa Uharibifu;ungekuwa umengʼoa mavuno yangu. 13 “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu,walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu, 14 nitafanya nini Mungu atakaponikabili?Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu? 15 Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu,si ndiye aliwaumba?Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sotendani ya mama zetu? 16 “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike, 17 kama nimekula chakula changu mwenyewe,bila kuwashirikisha yatima; 18 lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya,nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane: 19 kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo,au mtu mhitaji asiye na mavazi 20 ambaye wala moyo wake haukunibarikikwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu, 21 na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima,nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani, 22 basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu,nao na uvunjike kutoka kiungio chake. 23 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu,nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo. 24 “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu,au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ 25 kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu,ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata, 26 kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwakeau mwezi ukienda kwa fahari yake, 27 hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri,au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu, 28 basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa,kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana. 29 “Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu,au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia, 30 lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambikwa kuomba laana dhidi ya maisha yake; 31 kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema,‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’ 32 Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani,kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri; 33 kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo,kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, 34 kwa sababu ya kuogopa umati wa watu,na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa,nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: 35 (“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia!Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu:Mwenyezi na anijibu;mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. 36 Hakika ningeyavaa begani mwangu,ningeyavaa kama taji. 37 Ningempa hesabu ya kila hatua yangu,ningemwendea kama mwana wa mfalme.) 38 “Kama nchi yangu inalia dhidi yangu,na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, 39 kama nimekula mazao yake bila malipo,au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, 40 basi miiba na iote badala ya ngano,na magugu badala ya shayiri.”Mwisho wa maneno ya Ayubu.

In Other Versions

Job 31 in the ANGEFD

Job 31 in the ANTPNG2D

Job 31 in the AS21

Job 31 in the BAGH

Job 31 in the BBPNG

Job 31 in the BBT1E

Job 31 in the BDS

Job 31 in the BEV

Job 31 in the BHAD

Job 31 in the BIB

Job 31 in the BLPT

Job 31 in the BNT

Job 31 in the BNTABOOT

Job 31 in the BNTLV

Job 31 in the BOATCB

Job 31 in the BOATCB2

Job 31 in the BOBCV

Job 31 in the BOCNT

Job 31 in the BOECS

Job 31 in the BOGWICC

Job 31 in the BOHCB

Job 31 in the BOHCV

Job 31 in the BOHLNT

Job 31 in the BOHNTLTAL

Job 31 in the BOICB

Job 31 in the BOILNTAP

Job 31 in the BOITCV

Job 31 in the BOKCV2

Job 31 in the BOKHWOG

Job 31 in the BOKSSV

Job 31 in the BOLCB

Job 31 in the BOLCB2

Job 31 in the BOMCV

Job 31 in the BONAV

Job 31 in the BONCB

Job 31 in the BONLT

Job 31 in the BONUT2

Job 31 in the BOPLNT

Job 31 in the BOSCB

Job 31 in the BOSNC

Job 31 in the BOTLNT

Job 31 in the BOVCB

Job 31 in the BOYCB

Job 31 in the BPBB

Job 31 in the BPH

Job 31 in the BSB

Job 31 in the CCB

Job 31 in the CUV

Job 31 in the CUVS

Job 31 in the DBT

Job 31 in the DGDNT

Job 31 in the DHNT

Job 31 in the DNT

Job 31 in the ELBE

Job 31 in the EMTV

Job 31 in the ESV

Job 31 in the FBV

Job 31 in the FEB

Job 31 in the GGMNT

Job 31 in the GNT

Job 31 in the HARY

Job 31 in the HNT

Job 31 in the IRVA

Job 31 in the IRVB

Job 31 in the IRVG

Job 31 in the IRVH

Job 31 in the IRVK

Job 31 in the IRVM

Job 31 in the IRVM2

Job 31 in the IRVO

Job 31 in the IRVP

Job 31 in the IRVT

Job 31 in the IRVT2

Job 31 in the IRVU

Job 31 in the ISVN

Job 31 in the JSNT

Job 31 in the KAPI

Job 31 in the KBT1ETNIK

Job 31 in the KBV

Job 31 in the KJV

Job 31 in the KNFD

Job 31 in the LBA

Job 31 in the LBLA

Job 31 in the LNT

Job 31 in the LSV

Job 31 in the MAAL

Job 31 in the MBV

Job 31 in the MBV2

Job 31 in the MHNT

Job 31 in the MKNFD

Job 31 in the MNG

Job 31 in the MNT

Job 31 in the MNT2

Job 31 in the MRS1T

Job 31 in the NAA

Job 31 in the NASB

Job 31 in the NBLA

Job 31 in the NBS

Job 31 in the NBVTP

Job 31 in the NET2

Job 31 in the NIV11

Job 31 in the NNT

Job 31 in the NNT2

Job 31 in the NNT3

Job 31 in the PDDPT

Job 31 in the PFNT

Job 31 in the RMNT

Job 31 in the SBIAS

Job 31 in the SBIBS

Job 31 in the SBIBS2

Job 31 in the SBICS

Job 31 in the SBIDS

Job 31 in the SBIGS

Job 31 in the SBIHS

Job 31 in the SBIIS

Job 31 in the SBIIS2

Job 31 in the SBIIS3

Job 31 in the SBIKS

Job 31 in the SBIKS2

Job 31 in the SBIMS

Job 31 in the SBIOS

Job 31 in the SBIPS

Job 31 in the SBISS

Job 31 in the SBITS

Job 31 in the SBITS2

Job 31 in the SBITS3

Job 31 in the SBITS4

Job 31 in the SBIUS

Job 31 in the SBIVS

Job 31 in the SBT

Job 31 in the SBT1E

Job 31 in the SCHL

Job 31 in the SNT

Job 31 in the SUSU

Job 31 in the SUSU2

Job 31 in the SYNO

Job 31 in the TBIAOTANT

Job 31 in the TBT1E

Job 31 in the TBT1E2

Job 31 in the TFTIP

Job 31 in the TFTU

Job 31 in the TGNTATF3T

Job 31 in the THAI

Job 31 in the TNFD

Job 31 in the TNT

Job 31 in the TNTIK

Job 31 in the TNTIL

Job 31 in the TNTIN

Job 31 in the TNTIP

Job 31 in the TNTIZ

Job 31 in the TOMA

Job 31 in the TTENT

Job 31 in the UBG

Job 31 in the UGV

Job 31 in the UGV2

Job 31 in the UGV3

Job 31 in the VBL

Job 31 in the VDCC

Job 31 in the YALU

Job 31 in the YAPE

Job 31 in the YBVTP

Job 31 in the ZBP